BREAKING NEWS:WATU SITA WAFARIKI AJALINI


 Watu sita wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali iliyotokea leo asubuhi Machi 29, 2022 baada ya gari aina ya fuso (T 239 AFD) kuacha njia na kutumbukia korongoni katika barabara ya Soni – Mombo wilayani Lushoto mkoani Tanga.


 

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Safia Jongo amewataka watumiaji wa vyombo vya moto mkoani Tanga kuendelea kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.

 

Miili ya watu waliofariki dunia katika ajali hiyo imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Lushoto na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.

Comments

Popular posts from this blog

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

CONSTRUCTION OF THE ISONGOLE-ISOKO ASPHALT ROAD IS NOW OFFICIAL, CONTRACTOR INTRODUCED TO THE PUBLIC

MBUNGE MOMBA KUTOA SHILINGI MILIONI 28 UJENZI WA OFISI ZA CCM KATA 14