WANAKWAYA WAFARIKI AJALINI NJOMBE

 

Ajali iliyohusisha basi dogo aina ya Toyota Coaster na lori lililobeba makaa ya mawe, imekatisha maisha ya watu watatu wakiwemo waimbaji wa Kwaya ya Vijana wa Kanisa Katoliki mkoani Njombe (UVIKANJO).

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa ajali hiyo imetokea usiku huu eneo la Igima wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe.

Taarifa zinaeleza kuwa wanakwaya hao walikuwa njiani kwenda kuwatembelea watoto yatima katika kituo cha Ibumila kilichopo wilayani humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamisi Issah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa kwa sasa wako eneo la tukio katika harakati za uokoaji.

“Ni kweli tukio hili limetokea kwa sasa tupo huku maporini bado tunaendelea na uokoaji, mvua ni kubwa na kazi ni ngumu taarifa kamili tutaitoa baadaye. Kuna majeruhi tumewawahisha hospitalini na vifo vipo,” amesema Issah.

Hata hivyo, habari ambazo hazijathibitishwa zinaeleza kuwa kuna idadi kubwa ya majeruhi kwenye ajali hiyo ambayo haijafahamika idadi kamili

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

MBUNGE MOMBA KUTOA SHILINGI MILIONI 28 UJENZI WA OFISI ZA CCM KATA 14

BARAZA LA MADIWANI LAWAPONGEZA WALIMU UFAULU WA DARASA LA SABA