MKUU WA MAJESHI AAMUAGA RASMI RAIS MWINYI

 

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (CDF), Jenerali Venance Mabeyo amemuaga Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Mwinyi baada ya kumaliza muda wake utumishi ndani ya Jeshi hilo.

Mabeyo amemuaga Dk Mwinyi huyo leo Jumatatu Juni 6, 2022 Ikulu ya Zanzibar.

Katika maelezo yake Mkuu huyo wa Majeshi ya Ulinzi, alieleza haja ya kumuaga pamoja na kutoa shukrani kwa Rais Mwinyi akieleza kuwa ni kiongozi ambaye amefanya naye kazi kwa muda mrefu na kumsaidia katika kutekeleza vyema majukumu yake ndani ya Jeshi hilo.

“Nakutakia afya njema na maisha marefu pamoja na familia yako….nathamini sana ushirikiano ulionipa katika kipindi chako cha uongozi tangu ukiwa Waziri wa Ulinzi hadi leo hii, ahsate sana”, amesem Jenerali Mabeyo.

Mabeyo anafikia kikomo cha utumishi mwisho wa mwezi huu akiwa amelitumikia Jeshi hilo tangu mwaka 1979 huku nafasi hiyo ya CDF akiitumikia kwa kipindi cha miaka sita tangu alipoteuliwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati John Magufuli mwaka 2017.

Naye Rais Mwinyi mbali na kumpongeza kwa kutekeleza vyema majukumu yake katika kipindi cha utumishi wake ndani ya jeshi hilo, alimtakia kila la heri katika maisha yake ya kustaafu.


Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE