UKIMYA WA RC SONGWE WAZUA MASWALI


 Kutokana na kutokuonekana kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe alieteuliwa siku za hivi karibu Mhe Waziri Kindamba toka amefika Mkoani Songwe kujitambulisha na Shughuli zake zikionekana kufanywa na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mhe Cosmas Nshenye  na kuzua hali ya maswali Kwa wadau mbalimbali.


Kutokana na uwepo wa sintofahamu hiyo kituo chetu bora Nyanda za juu kusini na Taifa kwa  jumla tulilazimika kumtafuta Mkuu wa Mkoa Kindamba lakini mawasiliano ya simu  baina ya Mwandishi wetu na Kindamba hayakuwa mazuri kutokana na Hali ya hewa.Ndipo tulipoamua kumtafuta Mkuu wa Wilaya Mbozi Mhe Cosmas Nshenye na alipopigiwa simu yake haikupokelewa lakini baada ya muda alipiga mwenyewe na tukamuelezea sintofahamu hii.


"Ni kweli Mimi nilikaimu Mkoa lakini Mkuu wetu alikuwa kwenye Shughuli zingine za kiserikali na Wanasongwe wasiwe na shaka Mkuu kati ya Leo au kesho watamuona katika Majukumu mbalimbali Mkoani Songwe akiendelea na Majukumu yake" amesema Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Nshenye 

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE