PADRI APANDISHWA KIZIMBANI KWA UDHALILISHAJI WATOTO



 Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi, Sostenes Soka amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro kwa tuhuma za udhalilishaji wa kingono kwa watoto.

Kiongozi huyo wa kiroho, amepandishwa leo Jumatatu, Septemba 26, 2022 kusomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Salome Mshasha.

Hata hivyo, waandishi wa habari wamezuiwa kuingia katika chumba cha mahakama kwa kile kilichoelezwa ni aina ya kesi inayomkabili padri huyo.

Hakimu huyo amewaeleza waandishi wa habari kuwa atazungumza nao baadaye.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMBUKUMBU YA MAISHA YA MH. ESTER ALEXANDER MAHAWE

CONSTRUCTION OF THE ISONGOLE-ISOKO ASPHALT ROAD IS NOW OFFICIAL, CONTRACTOR INTRODUCED TO THE PUBLIC

*KUNDO AGOMA KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI VWAWA-MLOWO