UKUSANYAJI WA MAPATO TUNDUMA WAMKOSHA MAJALIWA AMTAKA DED KUCHAPA KAZI

 


Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji   Tunduma  Philimon Magesa kwa ukusanyaji wake Mkubwa wa Mapato ambapo kabla ya mwaka wa fedha kukamilika amekusanya Bilioni 8 huku kukiwa na mategemeo ya kukusanya zaidi.


Pia waziri mkuu amemuagiza Mkurugenzi huyo aendelee kubana mianya ya upotevu wa fedha kwani serikali ya Rais Dkt Samia imemuamini aendelee kupiga kazi.


Majaliwa alisema anafahamu changamoto anazopitia  Mkurugenzi huyo Halmashauri ya Tunduma hivyo atambue kuwa amewekwa hapo na serikali na achape kazi  eendelee na makusanyo kwani mapato  ndani yanajenga miradi mikubwa ikiwemo shule za Ghorofa huku akiagiza kuleta fedha zaidi ili Tunduma ipae kiuchumi kuendana na msemo wa lango kuu la Sadc.


Kwa Upande wa wake Mbunge wa Jimbo la Tunduma David Silinde amemueleza Waziri Mkuu kuwa  Mkurugenzi huyo ni jembe na anawasaidia sana Wilaya Tunduma na  amemshukuru Rais Samia kwa Kuwaletea Mkurugenzi mzuri na ana imani  Tunduma itaendelea kupaa katika Mapato.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

MBUNGE MOMBA KUTOA SHILINGI MILIONI 28 UJENZI WA OFISI ZA CCM KATA 14

BARAZA LA MADIWANI LAWAPONGEZA WALIMU UFAULU WA DARASA LA SABA