APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUUZA NYAMA YA MBWA



 Mkazi wa Kijiji cha Igale, Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Semeni Shombe (19) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo Iyula kujibu shitaka la kuchinja mbwa na kuuza nyama yake kinyume na sheria.



Imedaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka, Dotto Mwita kuwa Aprili 29, mwaka huu saa 7 mchana, mtuhumiwa huyo alikamatwa  huko katika Kijiji cha Ihowa ambapo alichinja na kuuza nyama ya mbwa kwa ajili ya matumizi ya chakula kwa wanadamu kitendo ambacho ni kinyume cha kifungu cha 181 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16.


Mshtakiwa huyo amekana shitaka hilo linalomkabiri.



Kwa upande wake Hakimu wa Mahakama hiyo, Mesia Ernest amesema kesi inayomkabili mshitakiwa ni ya


kughushi chakula kwa lengo la kuuza kinyume na kifungu cha 181 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 huku akijua kufanya hivyo ni kosa.


Hata hivyo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 11 mwaka huu itakapotajwa tena na mshitakiwa ameachiwa kwa dhamana na baada ya kukidhi masharti ya dhamana kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua ya utambulisho kutoka ofisi ya mtendaji wake.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE