TAKUKURU SONGWE WANZISHA UCHUNGUZI MIRADI 5 TUNDUMA KAMANDA ASEMA TUMESHATIA TIMU KITAELEWA FEDHA YA MIRADI AICHEZEWI

 


Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa( Takukuru) Mkoa wa Songwe imetoa taarifa yake ya miezi mitatu kwa vyombo vya habari leo jumanne Mei 16   2023 ofisi zake  Mkoa wa Songwe.


Kamanda wa Takukuru Edings Mwakambonja akiongea na waandishi wa habari  amesema  katika kipindi cha miezi mitatu cha Januari hadi Mwezi Machi Takukuru imeanziasha uchunguzi katika Miradi mbalimbali inayotekelezwa na fedha za serikali ambapo halmshauri ya Tunduma jumla ya miradi mitano imeiingia katika uchunguzi kutokana na kuwa na kasoro mbalimbali za kimatumizi na kujengwa chini ya viwango

Miradi ambayo Takukuru imeanzisha uchunguzi katika halmshauri ya Tunduma ni kama ifuatavyo

SHULE YA WASICHANA NAMOLE.

Mradi huu una thamani ya shilingi 400,000,000,00 katika mradi huu Takukuru imebaini kuwepo kwa manunuzi ya bati za kiasi cha Milioni 67 na manunuzi yake hayakufuata taratibu.

UJENZI WA KITUO CHA MWAKA KATI.

Takukuru imebaini kuwepo malipo ya vifaa bila vifaa kufika eneo la mradi pia fremu na milango Takukuru wamebaini vimejengwa chini ya viwango.

UJENZI SOKO LA MACHINGA. 

Ujenzi wake haujafuata mchoro wa ramani kwa baadhi ya majengo kama vile vyoo na kupelekea ukubwa wa vyoo kuwa mdogo. Aidha Takukuru pia imebaini mkandarasi kalipwa kiasi cha milioni 62 pasipo kujali hatua ya ujenzi ilipofikia  wala kukatwa malipo mengine kama Osha, CRB na Retention money. Pia wamebaini ushindani wa haki walishindamishwawazabuni wawili tu na alieshinda hakuwa na sifa.


KITUO CHA AFYA CHAPWA.


Imebainika milango na fremu imejengwa chini ya kiwango baadhi ya milango haifungi vitasa vilivyowekwa sio vile vilivyopangwa na rangi zimepakwa pasipo kujali usafi hivyo ubora wake hauridhishi.


KITUO CHA AFYA CHIPAKA.


Milango imejengwa chini ya kiwango na haifungi.


Kamanda  Mwakambonja amesema Takukuru imeshaanza kuichunguza miradi hiyo na kutoa wito kwa wale wote wanaodhani wataweza kufanikiwa kuchezea fedha za miradi watambue Takukuru ipo na inamulika kila kona.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE