UPIGAJI FEDHA ZA MIRADI TUNDUMA KIMENUKA, MKURUGENZI ALA VICHWA WATUMISHI 13 L, RAS TUNDUMA HAKUFAI TUTANYOOKA NAO APOKEA MAAGIZO YA RC WATUMISHI KUONDOLEA MJI WA TUNDUMA

 


Ziara kukagua miradi ya serikali katika Mkoa wa Songwe iliofanyika katika halmashauri tano za Mkoa wa Songwe imemaliza ijumaa kwa kuhitimishwa katika Wilaya ya Songwe.


Ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt Fransis Michael  imeweza kupiti miradi ya Elimu, Afya, Maji na miundombinu ya barabara imetamatishwa kwa kuzipongeza baadhi ya halmashauri kwa kuteleza miradi na matumizi matumizi  sahihi ya fedha za Serikali.

Akiongea mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo katibu tawala akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa ambaye hakuweza kuhudhulia ziara ya kutamatisha Wilaya ya Songwe kutokana na kuwa na majukumu mengine nje  ya Mkoa Katibu Tawala Happiness Seneda amesema lengo la ziara hiyo ni kuangalia utekelezaji wa miradi inaofanywa na halmashauri kuona miradi hiyo inajengwa kama maelelekezo yanavyotaka na fedha za Dkt Samia zinafanya kazi vile ilivyokusudiwa?


Seneda amesema katika ziara hiyo wamebaini kasoro ya baadhi ya miradi na halmashauri ya Tunduma ndio halmashauri ambayo wamebaini  baadhi ya miradi kuchezewa nao wao watachukua hatua mbalimbali zikiwemo za kuwaondoa baadhi ya watumishi kwa kuwapeleka maeneo mengine na wengine watachukuliwa hatua za kinidhamu


" Tumezunguka halmashauri zote  wamejitahidi sana sana kwenye miradi ila halmashauri ya Tunduma tumebaini changamoto kwa baadhi ya miradi na Mkuu wa Mkoa ameshanipa maelekezo baadhi ya watumishi tuwaondoe pale Tunduma na nitafanya hivyo wiki hiyo inayoanza baada ya kumalizika hii ziara tutawaleta Mkoani kabla ya kuwapeleka vituo vingine" amesema Seneda

Aidha Seneda ameeleza kwa upande wa halmashauri ya Mbozi wamebaini hali ya wao kukosa umoja na hata walipokuwa wakiulizwa baadhi ya mambo waliishia kutupiana mpira hali ambayo inapaswa kurekebishwa lakini kwa upande wa miradi wamejitahidi.. Kwa upande wa Halmashauri za Songwe, Momba na Ileje Seneda izipongeza kwa kufanya miradi kama walivyoelekezwa na kwa matumizi sahihi ya fedha na kama kuna changamoto basi ni ndogo ndogo na zinaweza kurekebisha


Ziara hiyo ilianza katika halmashauri ya Mbozi, Ileje, Momba, Tunduma kisha Songwe na ilihusisha wataalamu mbali mbali toka Mkoani Songwe


Kwa upande wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tunduma ambayo Ziara imebaini kuna kujezewa kwa fedha za miradi Philimon Magesa amesema kwa mji wa Tunduma ni kweli hata Mkaguzi wa ndani amebaini kuwepo kwa miradi fedha zake kuchezewa na baadhi ya hatua kwa upande wake  alishaanza kuzichukua ikiwemo kuwasimamisha kazi watumishi 10 ambapo mara baada ya kumtuma mkaguzi wa ndani ripoti yake ilionyesha kuwepo kwa bei za tofauti uhalisia upande wa vifaa vya ujenzi, kufanya malipo na vifaa hazifiki eneo la kazi hivyo amewachukulia hatua jumla ya watumishi 13 za kinidhamu na 10 kati ya hao amewasimamisha kazi.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE