DC ILEJE ALITAKA JESHI LA POLISI KUTOA ELIMU SHIRIKISHI YA USALAMA BARABARANI KWA BODABODA


MKUU wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe  Farida Mgomi amelitaka jeshi la polisi wilayani humo kutoa elimu shirikishi Kwa waendeshaji wa vyombo vya moto pasipo kutumia mabavu.


Mgomi amesema hayo Julai 17,2023 katika ukumbi wa chama Cha Mapinduzi uliopo Itumba  katika kikao Cha pamoja na waendesha bodaboda na bajaji ambacho kiliandaliwa na jumuiya ya umoja wa vijana CCM wilayani humo.


Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Mgomi amekemea vikali kamatakamata ya bodaboda bila kuwapa elimu ambayo itawasidia kuzijuwa Sheria za usalama barabarani huku akiwataka ushirikiano wa ulinzi na usalama wa wilaya yetu.

"Hakikisheni hawa vijana wanapokuja kwenye ofisi za serikali muwasikilizeni na kama changamoto zao zinaweza patiwa ufumbuzi Kwa haraka wapeni bila kusahau kuwatembelea na kuwapa elimu kwenye vituo vyenu vya kazi", amesema Mhe.Mgomi.


Mhe.Mgomi amewasihi madereva hao kufuata Sheria bila shuruti Kwa kuzingatia maelekezo ya jeshi la polisi usalama barabarani bila kukimbia na kuwasihi wajenge ushirikiano na jeshi la polisi kuwasilisha changamoto zai.

Aidha Mhe.Mgomi amewasihi madereva hao kuwatumia viongozi wao kufika kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ileje na Mkurugenzi halmashauri ya Ileje kuwaksilisha changamoyo zao wakae meza Moja na kuzitafutia ufumbuzi na kupeana uelewa wa pamoja.


Katibu wa chama Cha mapinduzi wilayani humo Hassan Lyamba amesema chama hicho kimewakutanisha na viongozi wa serikali Kwa lengo la kupeana uelewa wa pamoja kutatua changamoto zinazowakabili na zile ambazo zitahitaji mda kuzipatia majibu zitataliwa kupitia wataalamu.



Mwenyekiti wa jumuiya ya vijana CCM wilayani humo Diana Ngabo amesema kundi la vijana hao wamejiajili Kwa lengo la kujiingizia kipato hivyo kukutana na viongozi hao kutawasidia kujuwa sehemu ya kuwasilisha changamoto zinazowakabili.


"Jeshi la polisi tunawaomba msitumie mda mwingi kuwakamata bali wapeni elimu vijana hawa ambao ni madereva bajaji na bodaboda  ili watambue Sheria za usalama barabarani zitakazowasaidia kuepusha ajali zinazosababishwa na wao kukosa elimu,"amesema Ngabo.


Mmoja wa waendesha bodabofa Blesi amesema wakufunzi kutoka vyuo tofauti vya veta maeneo tofauti yamekuwa yakitoa mafunzo Kwa kushirikiana na jeshi la polisi wakiamini watapewa vyeti na leseni hali ambayo ilienda ndivyo sivyo.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE