AFANDE ASP DKT SHITINDI AONGOZA HARAMBEE YA UJENZI WA NYUMBA YA MAPADRE MBOZI MKOANI SONGWE


 Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dkt. Sister Shitindi kutoka Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Septemba 30, 2023 ameongoza Harambee ya kuchangisha pesa kwa lengo la kukamilisha ujenzi wa nyumba ya  Mapadre  Jimbo kuu Katoriki la Mbeya Parokia ya Kristo Mfalme-Bara kwa Paroko Atilio Mbogela Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe.



Hivyo, ASP Dkt. Shitindi akiwa kama mgeni rasmi katika harambee hiyo  aliwezesha kupatikana kwa kiasi cha shilingi  Milioni 15   kati ya Shilingi Milion  27, zinazohitajika ili kukamilisha ujenzi wa Kanisa hilo  Pamoja na ahadi mbalimbali zilizotolewa na waumini.


Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP  Theopista Mallya alipata nafasi ya kuzungumza na waumini wa Kanisa hilo na kuwataka waumini hao na  jamii nzima kwa ujumla kipiga vita vitendo vyote vya USHOGA, USAGAJI, ULAWITI,  UBAKAJI na  RUSHWA  pamoja na vitendo vyote vya  unyanyasaji wa Kijinsia na Ukatili dhidi ya watoto.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

MBUNGE MOMBA KUTOA SHILINGI MILIONI 28 UJENZI WA OFISI ZA CCM KATA 14

BARAZA LA MADIWANI LAWAPONGEZA WALIMU UFAULU WA DARASA LA SABA