AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 7.
Mahakama ya wilaya ya Iringa imemuhukumu kifungo cha maisha jela Steve Ngusi mwenye umri wa miaka 20 baada ya kumkuta na hatia ya kubaka mtoto mwenye umri wa miaka 7 Mwanafunzi darasa la kwanza.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu Said Ally Mkasiwa amesema mahakama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo bila ya Kuacha shaka kuwa Steve ametenda Kosa hilo na ametiwa hatiani.
Siku ya tukio Julai 5, 2023 mtoto huyo alifika dukani kwa babu yake ndipo babu yake akamwambia Steve ampeleke nyumbani lakini Steve alimpitisha katika majengo chakavu alimaarufu kama pagare nakumbaka mtoto huyo.
Ilipofika jioni bibi wa mtoto huyo aligundua mjukuu wake hayupo sawa ndipo alipompeleka hospitali na baada ya uchunguzi wa matibabu ilithibitika Kuwa mtoto huyo anamichubuko sehemu za siri.
Kesi hiyo ilisimamiwa na muendesha mashtaka wa serikali Sauli Makoli pamoja na mashahidi watatu akiwepo daktri aliyemfanyia vipimo mtoto huyo, muendesha mashtaka wa serikali alishauri mtuhumiwa huyo kupewa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine.
Kwa upande wa mtuhumiwa Steve alipopewa nafasi ya kujitetea aliiambia mahakama kuwa impe adhabu ya kufanya usafi mahakamani hapo kwani anamatatizo ya kisakolojia, ndipo mahakama ikamhukumu kifungo cha maisha jela na fidia shilingi milioni 7 kwa kosa la kumbaka mtoto mdogo wa miaka saba aliyekuwa anasoma darasa la kwanza.
Comments