Popular posts from this blog
ASKARI WATATU KITUO CHA TUNDUMA MAHAKAMANI KWA KWA RUSHWA
ASKARI Polisi watatu wa kituo cha Tunduma, Wilaya ya Momba, Mkoani Songwe, wamefikishwa mahakamani kwa mashitaka ya kuomba na kupokea rushwa kiasi cha shilingi million 55. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Songwe imewafikisha askari hao, leo Juni 4, 2024 katika mahakama ya Wilaya ya Momba iliyopo eneo la Chapwa, Mjini Tunduma. Askari hao ambao tayari wameshafukuzwa kazi na jeshi la polisi kabla ya kukamatwa na Takukuru kisha kufikishwa mahakamani hapo ni Koplo Enock Marando (43), Koplo Samson Kalebe (38), pamoja na Konstebo wa polisi Zawad Malakasuka (39). Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Momba, Timoth Lyon, mwendesha mashitaka wa Takukuru Mkoa wa Songwe, Simona Mapunda, alidai kuwa washitakiwa walitenda makosa hayo, Machi 7 mwaka huu katika mpaka wa tunduma. Mapunda alidai kuwa, siku ya tukio washitakiwa wakiwa ni waajiriwa wa jeshi la polisi waliomba rushwa ya shilingi milioni 55 ambapo ni kinyume na kifungu cha 15 (1) na (2) cha...
MFANYAKAZI NMB AFARIKI KWA KUJINYONGA
MFANYAKAZI wa Benki ya NMB tawi la Nkasi katika wilaya Nkasi mkoani Rukwa John Maduhu (32) mkazi wa Majengo mjini Namanyere amekutwa amekufa nyumbani kwake kwa kujinyonga kwa kamba. Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa mtaa wa Majengo soko kuu William Katutu alisema kuwa tukio hilo limegundulika jana asubuhi ya Mei 10,2024 majira ya saa 3 asubuhi na wafanyakazi wa benki hiyo baada ya mfanyakazi mwenzao kutoonekana ofisini asubuhi. Alisema kuwa tukio hilo liligundulika baada ya kuchungulia dirishani katika nyumba aliyokuwa akiishi marehemu ndipo walipouona mwili ukining’inia kwenye mlango wa chumbani kwake katika nyumba aliyokuwa akiishi. Mwenyekiti huyo wa mtaa amedai kuwa baada ya hilo walitoa taarifa Polisi ambao walivunja mlango na kuingia ndani na kumkuta marehemu akiwa amejining’iniza juu ya mlango wa chumbani kwa kutumia kamba ya jiko la umeme. Afisa mtendaji wa mtaa huo wa Majengo Flora Mbaule amekiri kutokea kwa tukio hilo na kuwa katika vipimo vilivyotolewa na Daktari i...
Comments