WAZIRI WA MAMBO YA NJE AJIUZURU


Waziri wa Mambo ya Nje Nchini Zambia, Stanley Kakubo amejiuzulu nafasi hiyo saa chache baada ya kukumbwa na kashfa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na shutuma za kufanya biashara na mfanyabiashara mmoja ambaye ni raia wa China.

Taarifa ya kujiuzulu kwake imetolewa na Ofisi ya Rais nchini humo baada ya kuibuka kwa video iliyokuwa ikionyesha watu wawili wakihesabu pesa taslimu zilizokuwa zimetapakaa mezani na kusambaa haraka kwenye akaunti za mitandao ya kijamii nchini Zambia.

Kakubo, ambaye alikuwa waziri wa mambo ya nje tangu Septemba 2021, alisema katika barua yake kwamba anaacha kazi kwa sababu ya madai mabaya juu ya miamala ya kibiashara.

Picha ya ujumbe ulioandikwa kwa mkono mnamo Julai 08, 2022, pia iliwekwa mtandaoni. Ujumbe huo uliitaja kampuni ya uchimbaji madini ya China na kampuni ya uchimbaji madini ya Zambia na kusema kuwa walibadilishana dola 100,000.

Ingawa majina ya Kakubo na Zang yalikuwepo kwenye ujumbe huo, haikuwezekana mara moja kuthibitisha maelezo ya kina.

Rais Hakainde Hichilema amekubali kujiuzulu kwa Kakubo, taarifa rasmi imesema. Haikutoa sababu ya kujiuzulu, lakini ikaongeza: “Rais anatambua kazi nzuri na uongozi wa Kakubo katika serikali”.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE