AKAMATWA NA FUVU LA BINADAMU
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma katika kuzuia na kutanzua uhalifu kwa kipindi cha mwezi Januri,2024 tumefanikiwa kuendesha Operesheni, misako na doria mbalimbali maeneo yote ya Mkoa wa Ruvuma ambapo katika misako hiyo tarehe 07.01.2024 katika kijiji cha Nahoro, Kata ya Luegu Wilaya ya Namtumbo tulifanikiwa kumkamata mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Dayano Swaum Chowo, (49), Mkazi wa Naholo akiwa na Fuvu lidhaniwalo kuwa la binadamu na vipande vitatu (3) vya ngozi wanyama pori akiwa amevihifadhi ndani ya begi dogo la mgongoni na kuvificha katika nyumba anayoishi.
Pia katika Operesheni hiyo tulizoendesha katika Wilaya ya Namtumbo kwa kushirikiana na Askari wa TAWA Kanda ya Kusini tulifanikiwa kukamata watuhumiwa watatu (3) waliotambulika kwa majina ya Jafari Likwata (41), Mkazi wa Minazini, Nicodemus Pius Ngonyani, (60), Mkazi wa Peramiho – Songea na Jafary George Ngesela wakiwa na Nyara za Serikari ambazo ni Meno ya Tembo mazima 18 na vipande 11 wakiwa wameyahifadhi kwenye mfuko wa Salfeti na kuficha maeneo tofauti tofauti ikiwa kwenye nyumba walizokuwa wananishi.
Aidha katika kata ya Muhuwezi Tarafa ya Nakapanya Wilaya ya Tunduru kupitia Operesheni hizo tulifanikiwa kukamata silaha mbili (2) aina ya Rifle na Gobole na watuhumiwa ambao ni Ally Rashidi Mbalamula (30), Amanzi
Issa Wilium (25) na Mohamed Selemeni Omary (37) wote wakazi wa Muhuwesi – Tunduru wakiwa na silaha hizo kinyume cha sheria.
Pia katika Kijiji cha Muhukulu Wilaya Songea tulifanikiwa kuokota Silaha moja aina ya Gobole iliyokutwa imetelekezwana watu wasiofahamika katika Ofisi ya Kitongoji cha Chepukila Kijiji cha Muhukulu.
Msako mkali unaendelea kuwasaka wahusika wa silaha hiyo kwa hatua zaidi.
Sambamba na hilo tulifanikiwa kukamata, jumla ya watuhumiwa 17 wakiwa na Pombe Moshi (Gongo) Lita 20, Pikipiki tatu (3) zenye namba za usajili MC.544 AUA aina ya SANLG rangi nyekundu, MC.955 CDD aina ya Houjue, MC.293 CCN, Engene moja aina ya Houjue, Mifuko minne (4) ya Cement ya Dangote, Marumaru 48PC mali ambazo zidhaniwazo kuwa za wizi pamoja na watuhumiwa 06 wakiwa na bhangi kete 124, Mbegu za bhangi 500gm na Bhangi kavu ikiwa imehifadhiwa ndani ya Salfeti,
Comments