WIZI WA MIFUKO YA SARUJI WAMSHANGAZA WAZIRI MKUU

 


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekemea vitendo vya wizi na uzembe kwenye usimamizi wa ujenzi wa miradi ya umma nchini.


 

Waziri Mkuu amesema hayo leo Februari 26, 2024, alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mara, iliyopo kata ya Buramba, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara.


“Tumeshaibiwa mifuko zaidi ya 600 kwenye ujenzi wa Shule hii ya Sekondari ya Wasichana ya Mara. Hakuna usimamizi, hakuna anayejali. Mngeanza kuchukua hatua ninyi wenyewe halmashauri kabla hata Mkuu wa Mkoa hajaja,” amesema.


Majaliwa amesema haridhishwi na utendaji kazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda hususani suala la usimamizi wa miradi ya maendeleo.


“Watu wanaiba mara ya kwanza, mara ya pili mmeshindwa kuchukua hatua za kuwadhibiti wasirudie tena? Halafu si hapa tu, hata hospitali ya wilaya ina matatizo mengi, mmeshang’oa na milango iliyofungwa, mmeshaiba na vifaa tiba ikiwemo mashine ya X-Ray. Sasa nyie Bunda mkoje?” Amehoji Waziri Mkuu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

WAFANYABIASHARA SONGWE WALALAMIKA FOLENI YA KUSIMAMISHIA MAGARI SENJELE NA NANYALA WILAYANI MBOZI

CHONGOLO AWACHARUKIA RUWASA NA TANESCO KUTOSHIRIKI ZIARA YAKE