JELA MIKA 30 KWA KUBAKA KIKONGWE CHA MIAKA 80.



Mahakama ya Wilaya Morogoro imemuhukumu Sadick Elias (24) Mkazi Pulambili Kata ya Kidugaro Tarafa ya Ngerengere Wilaya Morogoro vijijini kwenda Jela miaka 30 kwa kosa la kumbaka kikongwe wa miaka 80.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Morogoro Mh. Robert Kasele alisema kuwa tukio hilo lilitokea Julai 29, 2023 huko Pulambili Kata ya Kidugalo Wilaya ya Morogoro Vijijini ambapo mshitakiwa alifungua komeo na kuingia ndani ya nyumba ya Kikongwe huyo kisha kutenda kosa hilo.

Julai 30, 2023 Mtuhumiwa alikamatwa na Jeshi la Polisi na ushahidi ulipo kamilika mtuhumiwa alifikishwa Mahakamani na kutiwa hatiani kwa kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 kwenda jela kwa kutenda kosa la kubaka.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE