RAIS AFANYA UTEUZI HUU
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango, Dr. Migiro aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza kabla ya mkataba wake kuisha na nafasi yake kuchukuliwa na Balozi Mbelwa Kairuki August 16,2023 akitokea China ambako alikuwa anaiwakilisha Tanzanka kama Balozi Nchini humo.
Rais amemteua Fakii Raphael Lulandala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, kabla ya uteuzi huu Lulandala alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM).
Amemteua pia Dkt. Edwin Paul Mhede kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Mhede aliwahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) na anachukua nafasi ya Agnes Kisaka Meena ambaye amehamishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji.
Wengine walioteuliwa ni Gilbert Kalima ambaye ametuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, kabla ya uteuzi huu Kalima alikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi.
Rais Samia amemuhamisha pia Mhandisi Cyprian John Luhemeja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) na amemuhamisha Mary Ngelela Maganga kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).
Amemteua pia Dkt. Suleiman Hassan Serera kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, kabla ya uteuzi huu Dkt. Serera alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro ma anachukua nafasi ya Nicholaus Mkapa ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia wa Habari na amemteua Selestine Gervas Kakele kuwa Balozi, kabla ya uteuzi huu Kakele alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Comments