SONGWE :WATANO JELA MIAKA SABA KWA WIZI WA BIA


 *WATANO JELA MIAKA SABA KWA WIZI WA BIA.*


Mbozi Songwe: Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Mbozi Machi 28, 2024

imewahukumu Wakazi 05 wa Vwawa Mkoani Songwe kifungo cha Miaka 07 Jela kila mmoja kwa kukutwa na hatia ya kuvunja na kuiba vinywaji vikali vya aina mbalimbali na Tv flat screen inch 43 kampuni ya LG mali hizo zikiwa na thamani ya shilingi 2,641,000/=


Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Chami Changwe kwa Michael Nzunda, Samson Sichala, Allen Lwinga, Asheli Mlawizi na Steve Sanga ambao walikiri kufanya kosa hilo mnamo Machi 4, 2023 katika grocery hiyo maeneo ya Vwawa Kati Wilayani Mbozi.


Watuhumiwa hao walikamatwa maeneo na tarehe tofauti tofauti mwaka 2023 ndani ya Mkoa wa Songwe, na hukumu hiyo imetolewa kwa watuhumiwa hao ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.

Comments

Popular posts from this blog

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

CONSTRUCTION OF THE ISONGOLE-ISOKO ASPHALT ROAD IS NOW OFFICIAL, CONTRACTOR INTRODUCED TO THE PUBLIC

MBUNGE MOMBA KUTOA SHILINGI MILIONI 28 UJENZI WA OFISI ZA CCM KATA 14