TISA MBARONI KWA MAUAJI YA MLINZI

 HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linawashikilia watu tisa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mlinzi, Samweli Nofola (28), mkazi wa Kijiji cha Mtewele kilichopo Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe.


Hayo yamethibitishwa leo Aprili 14, 2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga wakati akizungumza na Mwananchi Digital.

Amesema tukio hilo la mauaji limetokea katika Mtaa wa Uzunguni, Kata ya Maguvani, usiku wa kuamkia April 13, 2024, saa 8:30 usiku.

Kamanda Banga amesema marehemu alikuwa mlinzi wa kampuni ya ulinzi iliyopo mjini Makambako na siku ya tukio, watu wasiojulikana walimuua mlinzi huyo na kuvunja maduka manne na kuiba vitu mbalimbali.

Comments

Popular posts from this blog

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

CONSTRUCTION OF THE ISONGOLE-ISOKO ASPHALT ROAD IS NOW OFFICIAL, CONTRACTOR INTRODUCED TO THE PUBLIC

MBUNGE MOMBA KUTOA SHILINGI MILIONI 28 UJENZI WA OFISI ZA CCM KATA 14