WANANCHI ILEJE WAHOFU KULA PARACHICHI ZA KISASA KUHOFIA NGUVU ZA KIUME



 Diwani wa kata ya Itale Fahari Mwampashe amemueleza Mkuu wa Mkoa wa Songwe  Daniel Chongolo kuwa wananchi wa kata yake wanaogopa kutumia maparachichi  ya kisasa kwa madai kwamba yanapunguza nguvu za kiume.


Akiongea katika ziara ya Ukaguzi wa kituo cha Itale Mwampashe amesema kumekuwepo na tetesi  katani  juu ya hayo maparachichi hivyo kumtaka Mkuu wa Mkoa  wataalamu wake kuwapa ufafanuzi juu ya hilo


Akijibu Mkuu wa Mkoa Daniel Chongolo amesema kwamba hizo ni tetesi za uongo tu na hayana madhara yoyote na yeye ni mmoja kati ya wakulima wa maparachichi na ameanza miaka mingine 


" Niwatoe wasiwasi haya maparachichi msidanganyike kuleni yapo  vizuri na yanaongeza afya na kinga za mwili hizo imani potofu achaneni nazo" alisema Chongolo

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

WAFANYABIASHARA SONGWE WALALAMIKA FOLENI YA KUSIMAMISHIA MAGARI SENJELE NA NANYALA WILAYANI MBOZI

CHONGOLO AWACHARUKIA RUWASA NA TANESCO KUTOSHIRIKI ZIARA YAKE