WATUMISHI WANANDOA KUTOTENGANISHWA KIKAZI SASA KUFANYA KAZI PAMOJA
SERIKALI imesia kilio cha wabunge cha kutaka watumishi wa serikali walio katika ndoa kutotenganishwa na wenza wao sehemu wanapofanya kazi, ikisema mwaka huu wa fedha watahakikisha wenza wanapohamishwa wanakwenda na wenza wao.
“Kila mtumishi mwenye mwenza wa kweli atakwenda kufanya kazi mahali pamoja, siyo lazima kiwe kituo kimoja cha kazi kama ni walimu basi mmoja atafundisha shule hii na mwingine atafundisha shule hii. Lakini mahali ambapo jioni wanakwenda kulala pamoja.”
“Ukiwa na cheti cha ndoa na umefunga ndoa ya kweli maana kuna ndoa nyingine za uongo uongo, hili hatuwezi kulikubali, tutahakikisha mwanya huu wa msawazo basi kila mtumishi tunawaunganisha ili waweze kufanya kazi kwa raha na starehe,” amesema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene.
Amebainisha jambo hilo limekuwa likiwakera na wabunge wengi wamekuwa wakipeleka maombi katika ofisi yake na hatua hiyo itaongeza tija katika utendaji wa kazi
Comments