UTOAJI HUDUMA KITUO CHA AFYA TUNDUMA WAMKOSHA MKURUGENZI TOKA OFISI YA RAIS


 Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume, amefanya ziara katika Mkoa wa Songwe, ikiwa ni ziara ya siku mbili katika mkoa huu. Ziara hiyo ilianza tarehe 26 katika Halmashauri ya Mji Tunduma.


Dkt. Rashid ametembelea Kituo cha Afya Mpande pamoja na Hospitali ya Halmashauri ya Mji Tunduma. Aidha, Dkt. Rashid amewapongeza viongozi na wauguzi kwa usimamizi na utoaji wa huduma nzuri katika vituo hivyo vya afya.


 Dkt. Rashid, huduma bora zinazotolewa katika vituo  zinapaswa kuendelezwa ili kuboresha zaidi afya za wananchi wa Mkoa wa Songwe. Pia ametoa wito kwa viongozi wa sekta ya afya kuendelea kushirikiana kwa karibu ili kufanikisha malengo ya afya kwa Mkoa.


Ziara hii ya Dkt. Rashid inalenga kuimarisha utoaji wa huduma za afya katika mkoa na kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma bora na za uhakika.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE