MBUNGE AMKOSHA KATIBU CCM MOMBA AWAAMBIA WANAMOMBA WASIJARIBU KUKOSEA



Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Momba Ndg. Kataba Sukuru amewataka wananchi wa Jimbo la Momba kuendelea kumuamini na kumpa muda mrefu wa kuwatumikia Mbunge wao wa Jimbo la Momba Mhe.Condester Sichalwe (Mundy).


Sukuru ametoa shukrani na pongezi hizo leo Julai 7 mwaka 2024 wakati akiwa mgeni mwalikwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kata ya Msangano.


Amesema kuwa Momba ni miongoni mwa majimbo hapa nchini ambayo imebahatika kupata Mbungemchapakazi na mwenye mapenzi mema na wananchi wake.


“Wananchi wa Momba, sisi chama cha Mapinduzi tunajivunia sana kuwa na Mbunge Condester, maana anawatengea haki wananchi, kwanza anafanya kazi kwa kujituma , pili anawapenda sana wanchi, maana kila Mbunge likiisha lazima afike jimboni na kuwasalimia watu wake, hakika huyu Mbunge mwenye kupigiwa mfano” Kataba

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMBUKUMBU YA MAISHA YA MH. ESTER ALEXANDER MAHAWE

CONSTRUCTION OF THE ISONGOLE-ISOKO ASPHALT ROAD IS NOW OFFICIAL, CONTRACTOR INTRODUCED TO THE PUBLIC

*KUNDO AGOMA KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI VWAWA-MLOWO