MBUNGE SHONZA ATOA MISAADA YA ZAIDI YA MILIONI 3.KWA WAJAWAZITO NA WATOTO AKISIFU KAZI ZA RAIS SAMIA
ATOA MISAADA YA ZAIDI YA MILIONI 3.KWA WAJAWAZITO NA WATOTO AKISIFU KAZI ZA RAIS SAMIA.
Mbunge viti maalum mkoa wa Juliana Shonza (CCM) ametoa wito kwa watumishi idara ya afya mkoani Songwe kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa
Shonza aliyasema hayo jana wakati akigawa vifaa kwa kina mama wajawazito na watoto katika hospitali ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe psmoja na kukagua ujenzi wa jengo la mama na mtoto ambalo linajengwa kwa Milioni 900.
Alisema siku za nyuma akiwa na uongozi wa chama alifika hospitalini hapo na kukuta kero nyingi ikiwemo lugha za matusi kwa wajawazito wanaofika hapo kujifungua.
Alisema mgonjwa anahitaji faraja ili aweze kujifungua salama na hilo alilifikisha kwa waziri wa afya Ummy Mwalimu hali iliopelekea watumishi wengine kuhamishwa katika hospitali hiyo.
"" Nawaomba tuwe na lugha za staa kwa akina mama hawa, na ni marufuku pia kuwatoza fedha akina mama wajawazito na watoto Dkt Samia analeta fedha nyingi ili kuwasaidia Wajawazito hawa kwa kuwajengea miundo mbinu rafiki sasa tukianza kuwatoza fedha ni kuichonganisha serikali na Wananchi hawa"alisema Shonza
Comments