MIL 900 KUJENGA KITUO KIPYA CHA AFYA, MLOWO,MBOZI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Serikali itapeleka shilingi Mil 900 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kwa ajili ujenzi wa Kituo cha Afya kitakachotoa huduma kama Hospitali ya Wilaya.
Waziri Mchengerwa ameyasema hayo alipokua akizungumza na Wananchi wa Mlowo Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe wakati Mhe. Rais aliposimama kuwasalimia wananchi katika Wilaya hiyo.
Amesema Mhe. Rais katika Jimbo hili kuna Hospitali ya Wilaya pamoja na vituo vya Afya 5 lakini kutokana na wingi wa watu waliopo hapa umetuelekeza tulete fedha kwa ajili ya Kituo cha Afya kipya na sisi Mhe. Rais tunatekeleza na fedha hiyo itaingia ndani ya mwezi huu.
Ujenzi wa Kituo hiki utafanya sasa Idadi ya Vituo vya Afya katika Wilaya hii kufikia 6 na Kituo hiki kitawekewa vifaa Tiba vyote muhimu ambavyo vitawezesha upatikanaji wa huduma bora za Afya’ alisema Mhe. Mchengerwa
Comments