CHONGOLO ATOA MIEZI MIWILI KWA WAKURUGENZI SONGWE KUWEKA MAONEO YA MAONYESHO YA KILIMO MAOFISINI MWAO

 


Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo kuanzisha sehemu za maonesho ya kilimo kwenye maeneo ya ofisi au makazi yao ili wananchi waweze kujifunza.


Mhe. Chongolo ametoa maagizo hayo baada ya kutembelea na kukagua mabanda ya maonesho ya wakulima maarufu Nanenane katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.


Mhe. Chongolo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika viwanja hivyo Jumanne Agosti 6, 2024, amesema kuwa kama walivyotengeneza viunga vya mbogamboga kwenye maonesho ya Nanenane hivyohivyo wafanye kwenye maeneo yao iloi wananchi waweze kuhamasika na kujifuynza.


Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa atapita kukagua utekelezaji wa agizo hilo ndani ya miezi miwili.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE