HALMASHAURI YA MOMBA YAMKUNA RC YAOKOA MAMILIONI YA FEDHA MBICHI...RAS AKABIDHIWA RUNGU LA WADAIWA
Halmashauri ya Wilaya ya Momba katika kipindi cha Miaka 7 imekuwa inakabiliwa na changamoto ya Kutopeleka fedha za makusanyo ya Mapato Benki hadi kufikia kiasi Cha zaidi ya shillingi Milioni 800 kuanzia Mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021 hali iliyopelekea Wilaya kuwa na hoja ya kujirudia kila Mwaka. Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi.Regina Bieda ameyasema hayo katika Baraza la kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Juni 25, kuwa tangu 2021 awe katika nafasi hiyo alibaini tatizo hilo na kuchukua hatua kali dhidi ya wote waliohusika kwenye kukusanya fedha za Mapato bila kuweka Benki na hatua kadhaa zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kuajiri vibarua wapya na kupewa mashine za POS ambazo zilikuwa zinatumiwa na watendaji wenye madeni ya Fedha mbichi ili kupisha Watendaji hao kuwa huru na Kuendelea na kesi zao bila kuathiti mapato ya Halmashauri. "Kuanzia 2021 Halmashauri tumefanikiwa kudhibiti mapato yanayokusanywa bila kuweka Benki, hadi Juni 2022 hatuna