TARURA YAANZA KUREJESHA FURAHA YA WANANCHI WILAYANI MOMBA
Wananchi Wilayani Momba, Songwe wamefarijika baada ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kukamilisha maandalizi ya ujenzi wa daraja la muda katika mto Nkana Kata ya Chilulumo. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya daraja la awali kuvunjika na kusababisha mawasiliano ya Kata za Chilulumo,Nkulwe,Kamsamba,Mkomba Ivuna na makao makuu ya Wilaya ya Momba kukatika. Akitoa taarifa kwa wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya TARURA, wakati wa ziara yao mkoani Songwe, Meneja wa TARURA Mkoa wa Songwe Mhandisi Killian Haule alisema kuwa TARURA kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Songwe,Jeshii la wananchi wa Tanzania (JWTZ), wamejipanga kurejesha mawasiliano ndani ya muda mfupi kwa kujenga daraja la chuma (TRUSS Bridge) ili wananchi wapate huduma ya Usafiri na Usafirishaji. Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TARURA Mhandisi Florian Kabaka amesema kuwa daraja hilo ni muhimu sana kwa uchumi wa wananchi na amewataka wananchi kulitunza pindi litakapo kamilika. Mkurugenzi wa barabara kutoka TAR