Machapisho

MAGAZETI 26 2021

Picha
 

RC SONGWE AAGIZA WALIMU 11 KURUDISHWA ILEJE, ABAINI KUWEPO UHAMISHO HEWA

Picha
 Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba ameitaja Wilaya ya Ileje kuwa ni kinara wa Uhamisho hewa kwa Walimu ambapo zaidi ya Waalimu 17 wamehamishwa pasipo kufuata taratibu hivyo ameagiza Waalimu 11 kurejeshwa Ileje. Ameyasema hayo  katika Kikao cha ushauri cha Mkoa wa Songwe(RCC) kilichofanyika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa leo (Alhamisi).

JAMBAZI WA UPORAJI FEDHA ILEJE AKAMATWA,WANANCHI WAMUUA AKUTWA NA SILAHA YA KIVITA

Picha
Mmoja kati ya Majambazi waliohusika na tukio la uporaji wa fedha zaidi ya milioni 25 zilizokuwa zinapelekwa benki na Meneja kituo cha  Mafuta cha Hike aliejulikana kwa jina moja la Matha uliofanyika kata Isongole mapema jana asubuhi amekamatwa na kuwawa na Wananchi wenye hasira kali Jambazi huyo amekamatwa kata ya Sange, Kijiji Sange ambapo Jambazi huyo aliotambulika kwa jina la Emili Yeka Mwakayamba (39) Mkiristo na Mkazi wa Mbeya.Akizungumzia tukio la kukamatwa mtuhumiwa huyo Mkuu wa Wilaya ya Ileje Anna Gidarya amesema kuwa Mtuhumiwa aliomba lifti katika gari aina ya fuso na kutokana Wilaya kujipanga na kuweka vizuizi katika njia mbalimbali za kuingia na kutoka Ileje baada ya kulisimamisha hilo aina ya fuso dereva wa gari hilo aliwaeleza Uongozi wa Kata kuwa kuna mtu wamempakia na wanamtilia mashaka ndani ya gari lao. Ndio walipompeleka ofisi ya Mtendaji kwa ajili ya kumuhoji na kumfanyia upekuzi ambapo Jambazi huyo alidai alitoka kwa Mganga na alipoulizwa ni Kijiji gani alitoka...

MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 23 2021

Picha
 

MKUU WA MKOA WA RUKWA JOSEPH MKIRIKITI ASIKITISHWA MANISPAA YA SUMBAWANGA KUTOTEKELEZA MAAGIZO.

Picha
    NA:Juliana Nyami,Rukwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa  Joseph Mkirikiti amesikitishwa na kitendo ha Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Jacob Mtalitinya  kushindwa kutekeleza maagizo ya kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kankwale ambayo aliyatoa mwezi Julai mwaka huu alipotembelea kijiji hicho . Mkirikiti  amesema hayo leo wakati alipokwenda kukagua utekelezaji wa maagizo yake aliyotoa mwezi Julai kuwa Manispaa ikamilishe mradi huo ulioanzishwa na wananchi mwaka 1997 kujengwa kwa nguvu za wananchi . " Hapa Mkurugenzi  wa Manispaa na Mstahiki Meya hamjatenda haki kwa wananchi .Mliahidi kwangu kuwa mtakamilisha zahanati hii na kuwa ilitakiwa ianze kazi mwezi Novemba mwaka huu . Hapa ni mapuuza tu yanafanyika " alisema Mkirikiti. Mkuu huyu wa mkoa aliongeza kusema " hapa nilikuja Julai nikakuta hali hii na leo naona tena hamjatekeleza maagizo yangu. Sasa nataka Mstahiki Meya chukua hatua tuone wananchi wakiheshimika kwa zahanati hii ikamilike mwaka huu" ...

WANANCHI SONGWE WAZINGIRA KITUO CHA POLISI KUDAI MIKOBA WA RAMBARAMBA WAO

Picha
 Kundi la wananchi wa kijiji cha Chang'ombe katika wilaya ya Songwe, wamevamia kituo cha Polisi Galula wakishinikiza kurejeshewa mikoba ya waganga wa jadi (lambalamba) iliyokamatwa na askari wa kituo hicho. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Janneth Magomi amesema wananchi hao walizingira kituo hiho Leo alfajiri kufuatia askari kuvamia kijiji hicho ili kuzuia waganga hao kufanya operasheni ya kukamata wachawi. Amesema kufuatia tukio hilo Mwenyekiti wa kijiji na watu wengine 23 wanashikiriwa na jeshi hilo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

MAJAMBAZI YAMPORA MENEJA WA KITUO CHA MAFUTA ILEJE MAMILIONI AKIPELEKA BENKI

Picha
  Majambazi yenye silaha yamemvamia Meneja wa Sheli ya Hike ilioko Isongole Wilayani  aliefahamika kwa Jina moja Matha wakati akipeleka fedha hizo benki iliopo Kata Itumba. Mashuhuda wa tukio hilo wadai kuwa  Majambazi hayo yalijifanya kama wateja wa usafiri na kusimamisha bajaji aliokuwa kapanda Meneja huyo maeneo ya Isongole kitongoji cha Chumba geni B jirani na Daraja na Kisha kumtoa Meneja ndani ya Bajaji na kuanza kumporaji  na kutokomea na zaidi ya Milioni 30 walizopora kusikojulikana. (MHE ANNA GIDARYA MKUU WA WILAYA ILEJE) Mwenyekiti wa Usalama Wilayani Ileje ambae pia ndie Mkuu wa Wilaya Anna Gidarya amekiri kutokea kwa tukio hilo leo asubuhi na amesema atalizungumzia tukio hilo baadae kwani kwa sasa ameagiza Jeshi la Polisi na Vyombo vya Ulinzi vyote vya Ulinzi Ileje kufanya msako Mkali na tayari wameongeza nguvu ya vikosi vingine Wilayani humo ili waweze kuyakamata Majambazi hayo popote yalipo. Tuachie Maoni yako hapo chini

SOMA HABARI KUBWA MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 22 2021

Picha
 

AJIKATA UUME KISA ULIJALI

Picha
  Mkazi wa Kijiji cha Itolwa wilayani Chemba Mkoani Dodoma, Juma Juma (34) amelazwa katika kituo cha Afya cha Hamai wilayani Chemba akiwa hoi baada ya kujikata uume wake. Inadaiwa kuwa Juma amefikia uamuzi huo baada ya kupata ajali na kuteguke kiuno na kusababisha asiwe rijali. Akizungumzia tukio hilo leo Jumapili Novemba 19, 2021 mjomba wa Juma, Yasini Nkusa amesema tukio hilo la Juma kujikata uume lilitokea Ijumaa nyumbani kwake Kijiji cha Itolwa ambapo alitumia wembe kukata uume wake. Hali ya majeruhi huyo imeelezwa kuwa mbaya pamoja na kwamba jitihada za madaktari wa Kituo cha Afya Hamai kuendelea kuokoa maisha yake. Juma ambaye ana mke na watoto watatu alipata ajali ya gari wiki mbili zilizopita.

MZEE AVAMIWA NA NYUKI NA KUFARIKI

Picha
  Mkazi wa kijiji cha Rau River Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Mathias Mallya (75) amefariki dunia baada kushambuliwa na kundi la nyuki wakati akiwa nyumbani kwake. Nyuki hao ambao walikuwa juu ya mti walimvamia mzee huyo baada ya tawi ambalo lilikuwa na sega kuanguka kutokana ya ngedere kutua kwenye tawi hilo. Akizungumza na Mwananchi, Diwani wa Kahe, Aloyce Momburi amesema nyuki hao walimng’ata sehemu mbalimbali za mwili mzee huyo hali ambayo ilimpeleka kupoteza maisha. "Hawa nyuki walikuwa kwenye mwembe, sasa ngedere alikuwa anapita akawa amerukia kwenye tawi lenye sega la nyuki ambapo lilikatika na kudondosha nyuki," "Huyu mzee alikuwa jirani na nyumbani kwake ikabidi asogee kuangalia ni nini kimetokea baada ya kuona nyuki wakizagaa kwa wingi alipoenda kuangalia nyuki wale wakaanza kumshambulia ikabidi akimbilie ndani bado wakamfuata na kuanza kumshambulia muda mchache aliishiwa nguvu na kupoteza maisha," Alisema jitihada za kumkimbiza hospitali hazikuzaa m...

JOEL KAMINYOGE MWENYEKITI TUGHE TAIFA ZIARANI KILIMANJALO

Picha
 Mwenyekiti TUGHE Taifa Joel Kaminyoge ametelea Mkoa wa  Kilimanjaro.Kaminyoge aliweza kupita ofisini kwa RAS , DC wa Moshi, ofisi ya mganga mkuu hospitali ya Mkoa mawenzi na hospitali ya Rufaa KCMC! Uongozi na wanachama wote aliweza kukutana na kuzungumza nao. (Picha mbalimbali akiwa Mkoani KILIMANJALO)