HII HAPA BARUA ALIOANDIKA MANGULA KUNG'ATUKA CCM
BARUA YA KUNG’ATUKA NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI WA CHAMA –TANZANIA BARA Tafadhari rejea kichwa cha habari hapo juu, Kwa heshima na taadhima naomba kukujulisha kuwa, nimeamua kung’atuka nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara. Uamuzi huu umetokana na sababu zangu binafsi zikiwamo za umri na utumishi wa muda mrefu, zimesababisha kutotimiza majukumu yangu kikamilifu. Umri wangu ifikapo Machi 31, 2022 (jana) nitatimiza miaka 81. Nimeanza utumishi tangu Januari Mosi 1962. Nilianza kazi ya ualimu katika chama. Niliteuliwa kuwa mwalimu wa siasa mwaka 1968 baada ya kamati kuu ya chama kuteua makada 75 walioandaliwa kwa kazi ya kutoa mafunzo kuhusu siasa ya chama na pia kuhusu ujenzi wa chama. Mwaka 1969 niliteuliwa na chama kuwa miongoni mwa walimu katika chuo cha Tanu Kivukoni. Nilikuwa mwalimu mshauri wa wanachuo katika chuo hicho na baadaye Kamati Kuu ya Tanu iliteua kuwa makamu mkuu wa chuo kwa miaka sita. Niliteuliwa kuwa katibu wa chama wa wilaya na mkuu wa wilaya. Baadaye...