Posts

Showing posts from December, 2023

SACP MASIME AKAGUA UTAYARI WA ASKARI WA SONGWE NA UKAGUZI WA KITUO VWAWA

Image
  Matukio mbalimbali pichani  yakimuonesha Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP David Misime akikagua mazoezi ya utayari kwa askari wa Mkoa wa Songwe  na kisha kufanya ukaguzi wa kituo cha Polisi Vwawa kilichopo wilayani Mbozi kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi na kuona utekeleza wa jukumu la kulinda usalama wa raia na mali zao.  Katika ziara hiyo Msemaji wa Jeshi la Polisi SACP David Misime pia alikagua matumizi ya mifumo mbalimbali ya Kidigitali ambayo kwa sasa yameanza kutumika ndani ya Jeshi la Polisi na kuleta ufanisi zaidi katika utekelezaji wa kazi za Jeshi la Polisi.

WATELEKEZA LORI NA PIKIPIKI SITA ZILIZOBEBA BANGI

Image
  POLISI mkoani Morogoro inamsaka dereva wa lori aina ya Mitsubishi Fuso lenye namba za usajili T.301 DPQ  lenye tela namba T. 562 DNV  mali ya  Kampuni ya K.T. Abri  alilolitelekeza. Ndani yake imekutwa mifuko 30 ya dawa za kulevya aina ya bangi ikiwa na uzito wa kilo 430 kando ya Barabara Kuu ya Morogoro- Iringa katika Kata ya Mangae , Wilaya ya Mvomero. Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Alex Mkama amesema hayo Desemba 31, 2023, na kusema Polisi walikuwa wanafuatilia nyendo za gari hilo baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu usafirishaji  dawa za kulevya aina ya bangi  kwenda Dar es Salaam. “Tuliweka mtego eneo la Kijiji cha Soli, Kata ya Mangae. Katika mtego huo tumefanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya bangi mifuko 30 yenye kilo 430 na pikipiki sita ambazo zilikuwa zinatumika kusafirisha kutoka mbali inakolimwa  na kuletwa maeneo  haya ya barabarani …lakini kwa bahati mbaya waliweza kukimbia kabla ya kukamatwa  kwao, “ amesema Mkama. Mkama, amesema  wameamua kushikili

MIKOA 8 YASHINDWA LENGO MIRADI YA BOOTS

Image
  WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amesema Mradi wa Uboreshaji wa Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) umetekelezwa kwa asilimia 92. Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa kikoa kazi na wakuu wa mikoa kwa ajili ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa maagizo yake ya kusimamia ujenzi na kuona namna walivyojipanga katika kuwapokea wanafunzi wapya Januari, 2024. “Katika maelekezo yangu nilielekeza kuwa miundombinu inayojengwa katika shule za masingi na sekondari ikamilishwe na isajiliwe kabla na ifikapo tarehe 31 Desemba mwaka 2023 ili kuwezesha kupokea wanafunzi wa awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza wanaotarajia kuanza masomo Januari 6 na8 mwaka 2024.” Kati ya Aprili na Juni 2023 Serikali ilituma fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya na miundombinu ya elimu ya awali, msingi na sekondari katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Mchengerwa amesema kati ya April na Juni mwaka huu, Serikali ilituma Sh bilioni 230 kwa ajili ya ujenzi wa shul

WAKAMATWA KWA KUTENGANEZA POMBE BANDIA

Image
  mkoani Morogoro inawashilia watu wanne kwa tuhuma za kuendesha kiwanda Bubu cha kutengeneza na kusambaza bidhaa bandia ya pombe kali aina ya Smart Gin katika mtaa wa Tushikamane kata ya Lukobe ,Manispaa ya Morogoro. Watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na chupa zilizojazwa 2,544 aina ya pombe hiyo, chupa tupu 2,988 ,chupa za Konyaji zilizojazwa 65, chupa tupu mbalimbali za konyaji zikiwa ndani ya mifuko minne ya salfeti, boxi moja, madumu lita 20 yaliyojazwa spiriti na mengine yenye mchanganyiko wa spiriti na maji . Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Alex Mkama amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kufanyika kwa oparesheni na misako mbalimbali mwishoni wa Desemba mwaka huu. Mkama amesema katika opereshani hiyo, polisi walifanikiwa kuwakamata Ramadhani Mdoe ( 30) mkazi wa Msamvu, Manispaa ya Morogoro na wenzake watatu kwa tuhuma za kukutwa wakitengeneza na kusambaza bidhaa feki ya pombe kali aina ya Smart Gin. Ametaja baadhi ya vitu vingine walivyokutwa navyo ni jaba tatu kwa ajil

MWANANCHI AWAPA POLISI NYUMBA YAKE ILI KIWE KITUO CHA POLISI

Image
  Mfanyabiashara na mkazi wa Kata ya Ilangala, Kisiwa cha Gana, Wilaya ya Ukerewe, Nyamitere Ugunya,  amejitolea nyumba yake aliyokuwa anaitumia na kuikabidhi kwa Jeshi la Polisi ili iwe kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa huduma za usalama kwa wakazi zaidi ya 6,000 wa kisiwa hicho. Nyumba hiyo yenye vyumba zaidi ya 15 inatakiwa kufanyiwa ukarabati mdogo wa kuwekewa miundombinu na mifumo ya majitaka itakayokidhi hadhi ya kituo cha polisi. Akizungumza na wananchi wa kisiwa hicho, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Wilbrod Mutafungwa amesema kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha polisi katika eneo hilo kunaenda kutatua changamoto za kiusalama ambazo zimekuwa zikiwakabili kisiwani hapo. Pia kamnda  amemuomba mfanyabiashara huyo aliyejitolea kujenga kituo cha polisi kukamilisha mapema hadi ifikapo mwishoni mwa Januari 2024. Hata hivyo, wakazi wa Kisiwa hicho wamemweleza Kamanda Mutafungwa changamoto mbalimbali wanazokutana nazo na kuomba Serikali i

MTUHUMIWA MMOJA ASHIKILIWA NA DAWA ZA KULEVYA, ULINZI WAIMARISHWA MKOANI MBEYA KUELEKEA MWAKA MPYA 2024.

Image
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Kelvin Amanyisye [19] Mkazi wa Lubele- boda ya Kasumulu kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya aina ya Bhangi kilogramu 13. Akizungumza na  waandishi wa habari Desemba 30, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi wa Polisi Benjamin E.Kuzaga amesema kuwa Mtuhumiwa alikamatwa Desemba 28, 2023 katika kivuko kisicho rasmi kiitwacho boda ya zamani kilichopo Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya akiwa na bhangi hiyo ikiwa kwenye mifuko ya rambo 13 na kufichwa kwenye begi kubwa na kuisafirisha kwa kutumia Pikipiki MC 366 aina ya Boxer. Mtuhumiwa alikuwa akielekea Stendi ya Mabasi Kyela kwaajili ya kusafirisha dawa hizo za kulevya kuelekea Dar es Salaam. Atafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika. Sambamba na hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kuelekea sikukuu ya mwaka mpya 2024 limejipanga vizuri kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao. Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa mtu/watu ambao hawana kibali cha kupiga/

DEREVA SONGWE AFUTIWA LESENI YA UDEREVA, WAWILI MBARONI

Image
Kamanda wa Polisi Mkoa wa songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya Disemba 30, 2023 ameendelea na operesheni ya ukaguzi wa magari ya abiria kwenye barabara ya kwenda Mbeya Tunduma katika kituo cha ukaguzi wa magari Mahenje wilayani Mbozi. Katika opereshion hiyo kamanda Mallya alimfutia leseni dereva Ally Lugenge (56) akiwa anaendesha gari lenye namba za usajili T855 DXL Kampuni ya Masihi inayofanya safari zake Ubaruku-Mbeya-Tund na Ileje. Gari hilo aina ya Fuso yenye uwezo wa kubeba abiria 45, ambapo kondakta na dereva wa gari hilo walipakia abiria zaidi ya 66 pamoja na mizigo kitu ambacho ni kinyume na taratibu za sheria za usalama barabarani pia ni hatari kwa usalama wa abiria. Kamanda Mallya alichukua uamuzi wa kumfutia leseni dereva huyo baada ya kurudia kosa la kuzidisha abiria ambapo alipewa onyo kali kisha kutozwa faini lakini dereva huyo alirudia kosa lilelile ambalo lilimpelekea Kamanda Mallya kumfutia leseni dereva huyo. Sambamba na hilo Kamanda Mallya aliwakam

TANGAZO LA AJIRA ZA UHAMIAJI HILI HAPA

Image
 

MABASI SABA YAZUILIWA KUENDELEA NA SAFARI MKOANI RUKWA

Image
Jeshi la Polisi Mkoani Rukwa kupitia kikosi cha usalama barabarani limeyazuia mabasi saba ya abiria kuendelea na safari za mikoani baada ya kukutwa na changamoto katika mifumo mbalimbali. Mwanasheria wa kikosi cha usalama barabarani nchini Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Deusi Sokoni, Disemba 28,2023 akizungumza baada ya kuendelea na zoezi la ukaguzi wa magari, upimaji wa kilevi na utoaji elimu ya usalama barabarani kwa madereva na abilia katika stendi ya Katumba, alisema jumla ya mabasi 25 yamekaguliwa ambapo kati ya mabasi hayo saba yalikutwa na changamoto katika mifumo na hivyo kuzuiliwa kuendelea na safari.  Mabasi hayo yaliyozuiliwa ni, kampuni ya Ruchoro Express, Mbinga One express, Mwakamboja, MM8, Bubele trans, Mwasi express, Msigwa trans, yanayofanya safari ndefu kwenda mikoa mbalimbali nchini. Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na mamlaka nyingine kama vile Mamlaka ya Udhibiti wa Vyombo vya Usafiri Aridhini (LATRA) imepewa mamlaka ya kuzuia chombo cha moto kuendelea na

RPC SONGWE AINGIA AFANYA UKAGUZI WA MAGARI MBOZI

Image
 . Abiria wanaosafiri kwenda sehemu mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Songwe wametakiwa kutoa taarifa za madereva wasiofuata sheria za usalama barabarani ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao. Hayo yamesemwa Disemba 28, 2023 na Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya baada ya kufanya oparesheni ya ukaguzi wa magari ya abiria katika eneo la Chimbuya na Mahenje wilayani Mbozi. Kamanda Mallya aliwataka abiria wanaosafiri kwenye mabasi kutoka Songwe kwenda maeneo mengine kutofumbia macho vitendo vya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na badala yake aliwataka kukemea vitendo hivyo na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa. Aidha, alisisitiza na kuwataka makondakta na madereva kutokuzidisha abiria pia kutoa tiketi kwa abiria wao kama sheria na taratibu za usafirishaji abiria zinavyoelekeza. Jeshi la Polisi nchini linaendelea na operesheni za ukaguzi wa vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na kutoa elimu

DADA AUWAWA KWA RISASI KISA ZAWADI YA CHRISTMAS

Image
  Ndugu wawili wamekamatwa baada ya dada yao kupigwa risasi na kuuawa wakati wa mabishano kuhusu zawadi za Krismasi. Msichana huyo mwenye umri wa miaka 23 alipigwa risasi kifuani na kakake huku akiwa na mtoto wake wa kiume wa miezi 10 kwenye gari la kubebea mizigo, polisi mjini Florida ilisema. Mvulana huyo baadaye alipigwa risasi na kaka yake mkubwa ambaye alichukua bunduki yake mwenyewe, Ofisi ya Sheriff wa Kaunti ya Pinellas ilisema Iliongeza kuwa kisa hicho cha ufyatulianaji risasi kilifuatia mabishano juu ya nani alikuwa akipokea zawadi zaidi. Sheriff Bob Gualtieri aliwaambia waandishi wa habari kwamba kijana mkubwa, mwenye umri wa miaka 15, alikimbia kutoka eneo la tukio na kutupa bunduki yake. Ndugu mdogo, mwenye umri wa miaka 14, alipelekwa hospitalini na yuko katika hali nzuri na atawekwa chini ya ulinzi atakapotolewa hospitaliu, polisi walisema. Waendesha mashtaka wa eneo hilo watatathmini kesii hiyo ili kuamua iwapo watamfungulia mashtaka kama mtu mzima kwa mauaji ya dada ya

MCHEZAJI MPYA SIMBA KUANZA NA KOMBE LA MAPINDUZI

Image
  BAADA ya dili lake la usajili kukamilika kwa asilimia mia moja, kiungo mpya wa Simba, Ladack Chasambi anatarajiwa kukiongoza kikosi hicho katika Kombe la Mapinduzi katika msimu huu. Chasambi ni kati ya wachezaji wapya waliokuwa wanawindwa vikali na baadhi ya klabu za hapa nchini kutokana na kiwango bora ambacho anakionyesha akiwa anaichezea Mtibwa Sugar ya Turiani, Manungu mkoani Morogoro. Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kufanyika Desemba 28, mwaka huu huko Unguja, Zanzibar. Taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, ni kuwa kiungo huyo dili lake limekamilika kwa asilimia mia moja ndani ya Simba, kilichobakia kwake ni kutambulishwa pekee. Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kiungo huyo mara baada ya kutambulishwa rasmi ataanza kuichezea timu hiyo katika Kombe la Mapinduzi Aliongeza kuwa kiungo huyo anatarajwa kuwepo katika msafara wa timu hiyo, utakaosafiri kwenda Zanzibar ndani ya siku hizi mbili kujiandaa na michuano hiyo. “Ladack usajili wake umekamilika kwa asilimia kubwa, na yeye huenda a

WAZIRI WA MAMBO YA NJE AJIUZURU

Image
  Share Waziri wa Mambo ya Nje Nchini Zambia, Stanley Kakubo amejiuzulu nafasi hiyo saa chache baada ya kukumbwa na kashfa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na shutuma za kufanya biashara na mfanyabiashara mmoja ambaye ni raia wa China. Taarifa ya kujiuzulu kwake imetolewa na Ofisi ya Rais nchini humo baada ya kuibuka kwa video iliyokuwa ikionyesha watu wawili wakihesabu pesa taslimu zilizokuwa zimetapakaa mezani na kusambaa haraka kwenye akaunti za mitandao ya kijamii nchini Zambia. Kakubo, ambaye alikuwa waziri wa mambo ya nje tangu Septemba 2021, alisema katika barua yake kwamba anaacha kazi kwa sababu ya madai mabaya juu ya miamala ya kibiashara. Picha ya ujumbe ulioandikwa kwa mkono mnamo Julai 08, 2022, pia iliwekwa mtandaoni. Ujumbe huo uliitaja kampuni ya uchimbaji madini ya China na kampuni ya uchimbaji madini ya Zambia na kusema kuwa walibadilishana dola 100,000. Ingawa majina ya Kakubo na Zang yalikuwepo kwenye ujumbe huo, haikuwezekana mara moja kuthibitisha maelezo ya k

SHEHENA YA MADAWA YA KULEVYA YAKAMATWA IRINGA,DAR

Image
  DAR ES SALAAM:  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya Tanzania (DCEA) imekatama jumla ya Kilogramu 3,182 za dawa za kulevya aina ya Heroin na Methamphemine zikiwa kwenye vifungashio vya kahawa na majani ya chai. Dawa hizo zimekamatwa katika operesheni maalum iliyofanyika jijini Dar es Salaam na Iringa kati ya Desemba 5 hadi 23, 2023. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba 27, 2023 Kamishna Jenerali, Aretas Lyimo amesema, tangu udhibiti uanze DCEA hazijawahi kukamata kiasi kikubwa cha dawa  kama ilivyo sasa na iwapo zingefanikiwa kuingia sokoni watu milioni 76.3 wangeathirika. “Ukamataji huu umeokoa nguvu kazi yaani Tanzania tupo idadi ya watu milioni 60 hizi dawa zingefanikiwa kuingia sokoni basi zingeathiri si tu wanzania bali hata mataifa mengine maana nyingine zilikuwa zikisafirishwa nchi nyingine,”amesema Lyimo. Akifafanua Lyimo amesema, kiasi hicho cha dawa kinajumuisha kilogramu 2, 180.29 za dawa aina ya Methamphemine na kilogramu

SOMA MAGAZETI YA LEO 27 DISEMBA 2023

Image