IDADI YA VIFO VYA KINA MAMA NA WATOTO WAKATI WA KUJIFUNGUA VYAPUNGUA MKOANI SONGWE
Songwe - Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe amefungua rasmi kikao kazi maalum kinachofanyika Tunduma, kilicholenga kujadili vifo vya akina mama na watoto wachanga vitokanavyo na matatizo ya uzazi. Katika kikao hicho, Seneda aliwapongeza watumishi wa sekta ya afya kwa kazi kubwa wanayoifanya, ambayo imeleta matokeo chanya kwa kupunguza idadi ya vifo hivyo mkoani Songwe. “Haya ni maendeleo makubwa sana kwani hata idadi ya wagonjwa wanaopewa rufaa kwenda hospitali ya kanda imepungua kwa kiasi kikubwa,” alisema Katibu Tawala huyo. Alieleza kuwa jitihada za serikali na utendaji mzuri wa wahudumu wa afya umeanza kuonyesha matokeo chanya katika kupunguza vifo vya mama na mtoto mkoani humo. Kwa mujibu wa takwimu zilizowasilishwa kwenye kikao hicho, mwaka 2022 kulikuwa na vifo 38 vya akinamama vilivyotokana na matatizo ya uzazi, huku vifo vya watoto wachanga vikiwa 320. Hata hivyo, mwaka 2023 idadi hiyo ilishuka hadi vifo 33 vya uzazi na vifo 196 vya watoto wachanga. Hii ni sawa na uwiano wa vif