Posts

Showing posts from January, 2022

NAIBU WAZIRI WA AFYA ASHTUKIZA BARAZA LA MADIWANI MBOZI

Image
 Naibu Waziri wa Afya Dr Godwin Mollel jana tarehe 28.01.2022 alifanya Ziara katika Mkoa wa Songwe na kuongea na Watumishi afya Mkoani Songwe. Mara baada ya kumaliza ziara yake Naibu Waziri Dr Mollel aliwashtukiza Baraza la Madiwani Mbozi pale alipoingia na kuhudhulia.Akiwa ndani ya Baraza la Madiwani Dr Mollel alipata wasaha wa kuongea na Madiwani,Wataalamu na Wananchi walikuwepo ndani ya Baraza hilo. Akitoa hotuba yake Naibu Waziri alisikitishwa na hamasa ya chanjo kwa Mkoa wa Songwe ambapo amesema Mkoa wa Songwe umeshika nafasi ya pili toka mwisho na Mkoa wa Manyala ni wa Mwisho kwa kutoa huduma ya Chanjo "Watumishi wa Afya acheni ujuaji mwingi kaeni na wenzenu wawape mbinu za hamasa za Chanjo kaeni na Viongozi wa Vijiji.Madiwani na Watendaji Kata hamuwezi kujua kila kitu" alisema Naibu Waziri wa Afya Dr Godwin Mollel Aidha kulingana na takwimu pia zilizotolewa Wilaya ya Ileje imeshika Mkia Kimkoa ambapo wadau mbalimbali wameeleza kudorora kwa hamasa kunatokana na baadhi y

MBOZI WAVUNJA HISTORIA WAKABIDHI MIKOPO KWA VIJANA BODA BODA ZA KUMWAGA

Image
 Halmashauri ya Mbozi ilioyopo Mkoani Songwe imekabidhi Pikipiki 25  na Bajaji 25 kwa Vikundi 5 vya Vijana Wilayani Mbozi  kutoka kata za Mbalimbali  ambapo Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba alikuwa Mgeni Rasmi. Katika hafla hiyo iliofanyika Viwanja vya Halmashauri ya Mbozi ilihudhuliwa na Madiwani wa kata zote wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbozi George Musyani na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbozi pamoja, Wataalamu,Viongozi wa vyama vya kisiasa pamoja na Wananchi. Mkuu wa Mkoa Mgumba aliwataka Vijana kujenga uaminifu katika Mikopo walipewa kwa kurejesha kiasi cha Mkopo walichopewa bila riba ili waweze kuaminika na kukopeshwa tena "Niwasihi sana Vijana Serikali chini ya Rais Samia inawapenda sana na imeamua kuwakopesha Mikopo hii isiyo na riba nayi muweze kujikwamua kiuchumi na kuwaajili wengine lakini niwaombe sana mrejeshe Mikopo hii ili iwasaidie wengine na nyie muweze kukopa tena" alisema Mgumba Aidha Mgumba amewapongeza Halmashauri ya Mbozi kwa kutoa Mkop

WABUNGE MBEYA WAPELEKA HOJA UWANJA WA NDEGE SONGWE UBADISHWE JINA

Image
  Wabunge wa majimbo ya Mkoa wa Mbeya wamewasilisha hoja kwa  Mkuu wa Mkoa huo, Juma Homera ili aipeleka hoja hiyo kwa Wizara ya Mawasiliano na Uchukizi kuomba kubadilishwa jina la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA) wakidai kuwa umekuwa ukionyesha taswira ya kuwa  Mkoa wa Songwe na si Mbeya kwa wageni wanaoingia na kutoka. Mbunge wa Jimbo la Kyela, Ally  Jumbe amesema hayo leo Ijumaa Januari 28, 2022 kwa niaba ya wabunge wa majimbo ya Mkoa wa Mbeya kwenye kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika katika ukumbi wa Mkapa jijini hapo kupitia taarifa za miradi  ya miundombinu kwa mwaka wa fedha 2021/22. Amesema kimsingi uwanja wa Songwe baada ya mikoa kugawanywa ulipaswa kubadilishwa jina na kwamba ni wakati sasa hoja hiyo ichukuliwe na Mkuu wa Mkoa na kuwasikishwa wizarani ili liingizwe kwenye mchakato. ''Pia tutakuwa hatumtendei haki Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini dada yetu Dk Tulia Ackson kwa uwanja huo kuendelea kuitwa Songwe hivyo tuupe hadhi kwani ni mali ya Mkoa wa

ROKETI YA ELON MUSK KUGONGANA NA MWEZI

Image
  Roketi iliyorushwa na kampuni ya uvumbuzi wa anga za juu ya bilionea Elon Musk inakaribia kugonga ndani ya mwezi na kulipuka.   Chombo kinachosaidia roketi kulipuka kwa  Falcon 9  kilikwenda katika anga za juu mwaka 2015, lakini baada ya kukamilisha safari yake, hakikuwa na mafuta ya kutosha ya kukirejesha duniania na badala yake kilibakia katika anga za juu. Mtaalamu wa masuala ya anga za juu Jonathan McDowell ameiambia BBC News kuwa itakuwa mara ya kwanza kwa roketi isiyoongozwa kugongana na mwezi. Lakini anasema athari yake itakuwa ndogo.   Roketi hiyo iliachwa katika (muhimili) orbit ya juu miaka saba iliyopita baada ya kukamilisha kazi ya kutuma setilaiti ya hali ya hewa katika safari ya maili milioni.   Ilikuwa ni sehemu ya mpango wa uvumbuzi wa anga za juu wa Bw Musk – SpaceX, ambayo ni kampuni ya kibinafsi ambayo lengo lake kuu ni kuwawezesha binadamu kuishi katika sayari nyingine

HAPPY BIRTHDAY MAMA WA TAIFA RAIS SAMIA

Image
  Ni Januari 27, ya mwaka 2022, siku njema iliyopokelewa na hali ya hewa tulivu, kama kawaida watanzania wanaelekea kwenye majukumu yao ya siku ya ujenzi wa taifa imara huku wengi wakiwa na furaha juu ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. Leo amezaliwa Amri Jeshi Mkuu, mama wa taifa, Chifu Hangaya, Kiongozi na mtetezi wa watanzania na taifa kwa ujumla. Kwakutambua hilo leo TanzaniaWeb tunakusogeza karibu na historia ya maisha yake, Mfahamu Rais Samia!…..   MAISHA  YAKE Mhe. Samia Suluhu Hassan alizaliwa Januari 27, 1960 katika Kijiji cha Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja. Ameolewa na Bw. Hafidh Ameir na wamejaaliwa watoto wanne, watatu wa kiume na mmoja wa kike.   ELIMU NA MAFUNZO Mhe. Samia Suluhu Hassan alipata elimu ya msingi katika shule mbalimbali, zikiwemo Shule ya Msingi Chwaka iliyoko Unguja kuanzia 1966 hadi 1968, Shule ya Msingi Ziwani mwaka 1970 na Shule ya Msingi Mahonda mwaka 1972. Baada ya hapo, alijiunga na Shule ya Sekondari ya Ng

MAKAMBA AVUNJA IDARA YA HABARI NA MAWASILIANO TANESCO

Image
  Arusha.  Waziri wa nishati, January Makamba ameagiza kuvunjwa kwa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa kushindwa kulisemea shirika hilo Makamba ametoa agizo hilo leo Jumanne Januari 25, 2022 wakati alipotembelea kituo cha usambazaji umeme kilichopo Njiro jijini Arusha ambapo amesema amevunja idara hiyo kutokana na kushindwa kutimiza majukumu yao ikiwemo kulisemea shirika hilo pamoja na kutoa taarifa kwa wateja wao. "Sisi kama Serikali hatufurahishwi na malalamiko ya wananchi kuhusu kukatika kwa umeme pamoja na upungufu wa taarifa zitolewazo kwa wateja,"amesema Makamba 

AMUUA MJAMZITO NA WATOTO WAKE WAWILI KISA GUNIA MBILI ZA MAHINDI

Image
  JESHI la Polisi mkoani Rukwa limemkamata Philipo Vincent (22) kwa tuhuma za kumuua kwa kumkata mapanga mjamzito na watoto wake wawili. Jeshi hilo limesema wakati wa kumhoji, mtuhumiwa huyo alidai kuwa alikuwa anamdai mjamzito huyo gunia mbili za mahindi.   Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, Theopista Mallya, alisema kuwa polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo kwa kuwa alijaribu kujinyonga ndipo walimkamata, na walipomuhoji alisema kuwa anataka kujiua kwa kuwa hana amani baada ya kufanya mauaji hayo.   Mallya alisema walipomuhoji zaidi, alikiri kufanya mauaji hayo kwa kuwa alikuwa amemkopesha gunia mbili za mahindi na alipomdai alionekana kufanya ukaidi wa kumlipa.   Alisema kuwa mtuhumiwa huyo alipokuwa akienda kwa mwanamke huyo kudai fedha Sh. 100,000 alimjibu kuwa asimdai kwa nguvu kwa kuwa hakumlazimisha amkopeshe, kauli iliyomuudhi mtuhumiwa na kuamua kufanya mauaji hayo.   “Mtuhumiwa huyo alinunua panga jipya na kulinoa vizuri, na siku ya Januari 14 usiku alikwenda nyum

YANGA WAPOKELEWA MWANZA KWA MBWEMBWE

Image
  Kikosi cha Yanga kimewasili Mwanza leo Januari 27, 2022 tayari kwa maandalizi ya mchezo wetu wa Kombe la ASFC dhidi ya Mbao Fc, Jumamosi kwenye Dimba la CCM Kiruma .

HALMSHAURI YA MBOZI

Image
 Mwekezaji wa Kiwanda cha Maparachichi Wilayani Mbozi Mkoani Songwe Bwana Tinson Nzunda ameendelea kulalamika kwa kutolipwa fedha zake za Miche ya Maparachi zaidi ya Milioni 27 anazoidai Halmashauri ya Mbozi toka 2017 licha ya agizo la Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba kuipa siku 90 Halmashauri hiyo kumlipa. "Mkuu wa Mkoa alishawapa agizo na Vikao vyote zimeagiza nilipwe na hata Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbozi Mhe George Musyani alimuhakikishia Mkuu wa Mkoa kupitishwa malipo yangu ndani ya Vikao vyote sasa sijui Mpaka sasa kwanini silipwi?" Amesema Mwekezaji huyo Nzunda. Aidha Mwekezaji huyo ametoa nyaraka zake zote zenye kuonyesha makabidhiano ya Miche hiyo ya Mapachichi kwa Shule za Wilayani Mbozi ambapo nyaraka hizo zikiwa na sahihi za Wakuu wa Shule na afisa kilimo pamoja na namba za simu za wapokeaji amesema Halmashauri ya Mbozi ilimuomba kama huduma ya Miche hiyo ya Miparachichi hivyo nae alitoa kama huduma kwa bei ya chini kabisa ili kuziwesha Shule nyingi kupanda

ASKARI POLISI AFIA GESTI AKIJIBURUDISHA NA MREMBO

Image
  JESHI la Polisi nchini Kenya linafanya uchunguzi kufuatia mwanaume mmoja, ambaye ni askari wa Jeshi hilo mwenye umri wa miaka 55 kufariki dunia katika chumba cha hoteli mjini Ndhiwa Kaunti ya Homa Bay nchini humo wakati akijiburudisha na mrembo aliyetoka naye kimahaba.   Kamanda wa Polisi Kaunti Ndogo ya Ndhiwa, Paul Rioba amesema kuwa kisa hicho kilitokea usiku wa Ijumaa, Januari 21, ambapo askari huyo ambaye jina lake limehifahdiwa, alipoteza fahamu na kufariki wakati wa kushiriki tendo la ndoa na mrembo huyo mwenye umri wa miaka 25.   “Mwanaume huyo alifariki akiwa chumbani na mwanamke huyo. Kwa mujibu wa mwanamke huyo ambaye tunamshikilia, mwanaume huyo alizimia na kuaga dunia wakati wa tendo la ndoa,” Rioba alisema.   Mwanaume huyo anasemekana kuwasili wa kwanza na kulipia chumba chao cha hoteli huku mwanamke huyo akijumuika naye baadaye.   Katika taarifa aliyotolewa na polisi, mwanamke huyo alisema kuwa mwanaume huyo alipozimia. ilimlazimu kuwaarifu wasimamizi wa hoteli hiyo, n

DC MBOZI " MBOZI JENGENI KUMBI YA KISASA YA VIKAO VYENU MADIWANI

Image
 Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Cosmas Nshenye amewata Madiwani Wilayani Mbozi kwenda kujifunza na kuangalia Kumbi za Halmashauri zingine za Mikutano ili nao waweze kujenga. Akiongea katika Kikao cha Baraza la Madiwani Mbozi Nshenye amesema ni aibu kwa Halmashauri kubwa kama Mbozi kuwa na Ukumbi wa Mikutano kama uliopo sasa ambapo amesema staili ya Kuazimana visema( Mic) ilishapitwa na Wakati hivyo Madiwani wajipange na Ujenzi wa Kumbi mpya na kisasa. Aidha katika hatua nyingine Cosmas Nshenye amelishauri Baraza la Madiwani kufanya utafitii mkubwa sana kutafuta vyanzo vya mapato  baada ya kugundua vipo ambavyo havikusanywi. Amesema hayo Januari 25 ,2022 kwenye kikao Cha bajeti ya mwaka 2022 /2023 ambapo  Ofisa Mipango wa was Halmashauri  Erasto Mwasanga halmashauri itatumia zaidi ya Sh 57 bilioni  katika kipindi hicho. Mkuu wa wilaya pia amewashauri  madiwani  wake akilini suala la kujenga Ofisi na ukumbi mkubwa katika Halmashauri ya Mbozi Amewataka kuwa makini kwenye vyanzo vya mapato na pia

TAKUKURU YATHIBITISHA KUMSHIKIA TRAFIKI KWA RUSHWA

Image
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na  Rushwa mkoani Iringa imethibitisha kumkamata askari wa usalama barabarani kwa kosa  la kupokea rushwa kwenye mabasi maeneo ya Ipogolo Manispaa ya Iringa siku ya  Januari 18, 2022. Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa,Domina Mukama amesema kuwa, walimkamata Koplo Steven Mchomvu akipokea rushwa kwenye mabasi ambayo yanapita katika  barabara ya Ipogolo. Amesema kuwa, picha ambazo zimesambaa  kwenye mitandao ya kijamii zilipigwa na maafisa wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa  mara baada ya kumkamata askari huyo wa usalama barabarani akipokea   rushwa kutoka kwenye basi. Mukama amesema kuwa, polisi huyo bado  anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa na taratibu zote zikikamilika  atapelekwa, ndio watatoa taarifa nini kitafanyika kwa mujibu wa sheria  za nchi. Amesema kuwa, walimkuta na kiasi cha shilingi laki moja na nusu pesa taslimu ambazo alikuwa nazo mfukoni ambazo alikuwa akipokea rushwa kwa magari mbalimbali. Mkuu huyo ametoa onyo kwa watumishi wote wa  seri