Posts

Showing posts from February, 2022

RASMI: MABASI YA MAJINJAH KUANZA SAFARI MBEYA-KAMSAMBA KILYAMATUNDU

Image
Ziara ya Mwekezaji Mkubwa Mkoani Songwe Alnanuswe Kabungo (Majinjah) imeanza kuzaa matunda Mkoani Songwe ambapo Kampuni ya Mabasi ya Majinjah imetoa Mabasi yake Makubwa mawili  yatakayo anza safari zake mpya Mbeya,Mlowo,Ivuna ,Kamsamba hadi Rukwa Kilyanantundu. akiongea nasi Rahimu Secha ( Trade development Representative ) kutoka Majinjan amesema kuwa wametembelea Maeneno mbalimbali ya Wilaya za Mkoani Songwe na wameona fursa nyingi wakiwa kama team Majinjah wakiongozwa na Mkugenzi  Majinjah "Mkurugenzi katoa gari (Mabasi) mawili yatakayo kuwa yanafanya safari zake Kamsamba-Mbeya na yatakuwa yanabeba na abiria wetu wa Dar es Salaam lakini pia tumepokea ombi toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Songwe Mhe Simalenga kaomba tuwape basi la Mkwajuni - Dar  kwani wachimbaji na Wananchi wa Wilayani Songwe wanashauku ya kusafiri moja kwa moja mpaka Dar toka Songwe ombi hili kama Kampuni tunalifanyia kazi"amesema Rahimu

MWEKEZAJI MAJINJAH AZIDI KUVUTIWA NA ARDHI YA MBOZI

Image
 Mwekezaji kutoka Igamba  Wilayani Mbozi Mkoani Songwe Alnanuswe Kabungo ambae pia ni mmiliki wa Kampuni ya Usafirishaji ya Majinjah logistics Company amemtembelea Diwani wa Kata ya Nyimbili  ambaye pia ni mwekezaji na mzalishaji wa Miche bora ya Kahawa,Miparachichi na mikademia pamoja na Mazao mengine kutoka Kampuni ya Lima. Akiwa Kijiji cha Masangula Kabungo alifika Nyumbani kwa Mwekezaji huyo na kumpa pole yeye na Familia yake kufuatia kifo cha Mama Mzazi wa Mwekezaji huyu kilichotokea wiki iliopita Masangula. Aidha baada Tinson Nzunda alipata wasaha wa kumuonyesha baadhi ya Mashamba mchanganyiko kwa maana ya Kahawa,Miparachi,Miakademia na Migomba kupandwa pamoja hali iliopelekea kumvutia Mwekezaji Majinjah na timu aliongozana nayo ukiongozwa na Meneja Uzalishaji wa Majinjah Logistics Kampani James Mgeni. Sambamba na Shamba hilo Mwekezaji Majinjah alitembelea Shamba la kuzalisha Miche ya Kahawa,Parachichi na Mikademia  na kuona Jinsi Uzalishaji wa Miche hiyo pandikizi unavyofanyika

Mahakama Yaamuru Makonda Asakwe Mpaka Kolomije

Image
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni leo Jumanne tarehe 8 Februari 2022, imetoa amri ya kutangazwa gazetini, nyumba aliyoishi Masaki na au kijijini kwao Kolomije kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.   Lengo ni ili kumwezesha Makonda kupata taarifa za kesi iliyofunguliwa dhidi yake na Mwandishi wa Habari mwandamizi, Saed Kubenea.   Kubenea amefungua maombi ya kufungua kesi ya jinai dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Makonda mwenyewe.   Uamuzi huo umetolewa na Hakimu, Aron Lyamuya ambaye ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 2 Machi 2022.   Ametoa uamuzi huo baada ya mawakili wa Kubenea, Nyaronyo Kicheere na Hekima Mwasipu kuiomba mahakama kutoa samasi ya kumtangaza kwani jitihada za kumpata Makonda ili kupatiwa wito wa kufika mahakamani kugonga mwamba  

WANANCHI WA ISELA,MLANGALI WAREJEA KATIKA MAJUKUMU YAO

Image
 Wananchi wa kitongozi cha  isela kilichopo kata ya Mlangali Wilayani Mbozi Mkoani Songwe wamerejea katika shughuli zao za kila siku baada ya kukimbia Kitongijini kwa hofu ya kukamatwa na Jeshi la Polisi. Wananchi hao ambao siku ya Ijumaa  kundi la Wananchi lilivamia baadhi ya nyumba na kufanya uharibifu kwa kukata mazao,kubomoa nyumba na uharibifu mwingine ni baada ya Kaya zilizolengwa kudaiwa kukubali kusaminisha ardhi yao ili kulipwa fidia kupisha hifadhi Mpya ya Ngorongoro inayotarajiwa kuanzishwa maeneo hayo yalio jirani na Kimondo. Kundi ambalo haliko tayari kuondoka na kupisha hifadhi hiyo ndilo linalodaiwa kufanya uharibifu.Mara baada ya Polisi kufika katika Kitongoji hicho Wananchi walikimbilia milimani ili kukwepa kukamatwa na kuziacha Kaya zao hali iliopelekea kitongozi kukosa watu na Shughuli mbalimbali kusimama. Leo Jumapili Wananchi wa Kitongoji cha Isela wamerejea baada ya jitihada mbalimbali zilizofanywa na Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Diwani wa Kata hiyo Mhe Davi

RAIS SAMIA AREJESHA TABASAMU KWA WANAFUNZI WA KIKE WALIOKATA TAMAA

Image
 Kufuatia agizo lililotolewa na Rais wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani la Wanafunzi walioshindwa kuendelea na masomo ya Sekondari kwa sababu mbalimbali zikiwemo Ujauzito na zingine nyingi kurejea Mashuleni. Mkoani Songwe hususani Wilaya mama ya Mkoa wa Songwe ambayo ndio Makao Makuu ya Mkoa yalipo ya Mbozi Shule ya  Sekondari ya Vwawa ndio kituo maalumu cha Wanafunzi hao walioshindwa kuendelea na masomo kilipo. Habari Jamii tumeweza kufika Shuleni hapo na kuwakuta wakiendelea na Masomo yao ambapo jumla ya Wanafunzi 22 wanaendelea na Masomo na Wameonyesha wazi kufurahia nafasi hiyo wao waliita ni adimu na  kihistoria kwao na hawakutarajia kama wangeipata ingali walikwisha kukata tamaa. Wanafunzi hao huku wakiwa na nyuso zilizokuwa zimekata tamaa wameeleza kiunaga ubaga sababu zilizowafanya washindwe kuendelea na Masomo zikiwemo kupata Ujauzito,kulazimishwa kuolewa wengine ni Wazazi wao kushindwa kuwalipia ada kutokana na kutoweza kujimudu kimaisha na hata wengine w

HII NDIO CHANGAMOTO ILIOIKUMBA STENDI MPYA MLOWO

Image
 Stendi Mpya ya Forest iliopo Mji mdogo wa Mlowo ambayo hivi sasa imekumbwa na Miundo mbinu ya kutoingilika ndani kwa  ulahisi hali iliopelekea Magari ya Abiria na Shughuli zingine za kibiashara kufanyika  kando kando ya Barabara kuu ya Tanzam. Baadhi ya Madereva wa Mabasi na wafanyabiashara ndani ya Stendi hiyo inayoendelea na Ujenzi Mkubwa wa Vibanda vya biashara na Miundo mbinu mingine ndani ya Stendi hiyo na nje  wametoa wameelezea kero wapatayo wao kutokana na Shughuli nyingi kufanyika eneo hilo walilodai ni finyu na ni hatari zaidi kutokana na kuwa pembezoni mwa Barabara hiyo kubwa ya Tanzam. "Eneo hili ni dogo sana Magari ni mengi kwanini Halmashauri ya Mbozi wasifukie yale mashimo mbona ni kiasi tu kusawazisha kifusi Shughuli ziendelee" alisema Sambo Kitwana Dereva Daladala  Nae Mfanyabiashara wa pembezoni mwa maduka yaliopo jirani na Stendi hiyo Maria Mwasupila amesema wao kama Wafanyabiashara wa Maduka hivi sasa hawauzi kabisa kwani shughuli zote huishia huko huko p

BAJETI YA TARURA YAKALIWA KOONI NA MADIWANI MBOZI

Image
 Madiwani wa Baraza la Mbozi wameitaka Bajeti ya Wakala wa Barabara TARURA kuzingatia Majimbo ya Mbozi na Vwawa.Katika baraza maalumu la Madiwani na TARURA kilichofanyika leo Jumanne ya tarehe 01,02,2021 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mbozi.Madiwani hayo wameshangazwa baada ya kusomewa Taarifa ya Bajeti hiyo na Meneja wa Tarura Wilaya ya Mbozi ambapo Jimbo la Mbozi limetengewa kiasi Cha shilingi bilioni 1 na Jimbo la Vwawa lenye kata nyingi limetengewa tu kiasi cha shilingi milioni 500. DIWANI wa kata ya Nyimbili  Tinson Nzunda ameomba fedha za utengenezaji wa barabara  Mjini na vijijini  TARULA Sh bilioni 1.5 za Jimbo la Vwawa na Jimbo la Mbozi   zichanganywe na zigawiwe kwa usawa katika kata zote  Yamesemwa hayo  Februari1   kwenye  Baraza la usomaji wa bajeti ya mwaka  wa fedha 2021/2022ya Utengenezaji wa barabara za vijijini na mjini Akichangia hoja hiyo diwani wa kata ya Harungu Maarifa Mwashitete kwa kusema nikweli kabsa sio sahihi kwa Jimbo lingine lipewe Sh Bilioni 1 na lingin

TAKUKURU SONGWE YABAINI KUWEPO KWA RUSHWA YA NGONO SEKTA YA ELIMU SONGWE

Image
 Akiongea na Vyombo vya habari ofisi za TAKUKURU Mkoani Songwe Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Songwe Edings Mwakambonja amesema kuwa Takukuru wamefanya Uchambuzi wa mifumo Mitatu ambayo ni Uchambuzi katika Sekta ya Elimu ambapo wamebaini kuwepo kwa mianya mingi ya Rushwa ya Ngono sekta ya Elimu. Kamanda amesema kumekuwepo na viashiria vya Rushwa ya Ngono katika upangaji wa Vituo vya kazi,uhamisho wa ndani pamoja na utoaji wa fursa za mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu pamoja na Uteuzi wa kufanya kazi maalumu kama vile kusimamia mitihani. "Pindi zinapotoka nafasi hizi kuna viashiria vya Rushwa ya  Ngono kwa walio na mamlaka ya shughuli hizi hivyo ofisi yetu inatoa onyo na tunatarajia kufanya warsha na wadau wanaohusika na Uchambuzi huu ili kujadili namna ya kuziba mianya hii" amesema Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Songwe. Katika hatua nyingine  Takukuru Songwe wamebaini kuwa taasisi nyingi za Serikali hazifanyi manunuzi kupitia Wakala wa Manunuzi ya Taasisi za Umma (GPSA) na wao Wa