Posts

Showing posts from October, 2023

DEREVA WA DC MBOZI ADONDOKA WAKATI DC AKIENDELEA NA MKUTANO NA WANANCHI AFARIKI DUNIA HOSPITALI

Image
 Dereva wa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi anaefahamika kwa majina ya Goodluck Mbazu amefariki katika hospital ya rufaa Mkoani Mbeya ambapo alikimbizwa baada ya kudondoka wakati akitaka kushuka kwenye gari alilokuwa amepumzika wakati Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Esther Mahawe akieendelea kuwahutubia Wananchi katika Mkutano wa wa utatuzi wa mgogoro Kijiji cha Shaji kata ya Mlangali. Akiongea kwa njia ya  simu Mkuu wa Wilaya ya Mbozi ambae alishindwa kuongea vizuri kutoka na kuwa katika hali ya kushindwa kuamini kifo cha dereva wake huyo amesema alikuwa ni sehemu ya familia yake na aliishie nae kama ndugu hivyo kifo chake cha ghafla kimemuumiza  na kushindwa kuamini kwani ndie aliwapeleka katika Mkutano huo Kijiji cha Shaji na alikuwa na afya njema lakini alipomaliza Mkutano aliarifwa kuwa dereva wake amekimbizwa hospitali baada ya  kadondoka wakati akishuka katika gari alilukiwa amekaa na dereva mwenzie wakipumzika . "Nilalifiwa kuwa dereva wangu alianguka wakati akijaribu kushuka kwenye gari a

NAIBU WAZIRI WA UJENZI AFANYA ZIARA KUKAGUA MIUNDOMBINU YA BARABARA WILAYANI SONGWE

Image
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara katika Wilaya ya Songwe. Naibu Waziri akijadiliana na Mkuu wa Wilaya Songwe kushoto Waziri huyo amefanya ziara hiyo leo Jumatano Oktoba 4, 2023 ambapo ametembelea na kukagua daraja la Gulula, eneo la Zira ambalo linatarajiwa kuanza ujenzi wa tuta la kuzuia maji wakati wa mvua pamoja na kipande cha barabara ya lami cha Mkwajuni-Saza chenye urefu wa mita 400 kilichojengwa kwa thamani ya zaidi ya Sh300 milioni. Katika ziara hiyo, Mhandisi Kasekenya ameiagiza TANROADS Mkoa wa Songwe kuharakisha ujenzi wa tuta hilo katika eneo la Zira kabla msimu wa mvua haujaanza huku akiwataka wananchi kutunza miundombinu ya barabara. Waziri huyo ambaye aliambatana na wataalamu wake akiwemo Meneja wa Tanroads Mkoa wa Songwe, Suleiman Bishanga walipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Solomon Itunda, Katibu Tawala wa Wilaya ya Songwe, Reuben Chongolo, Kaimu Mkuruge

DC ILEJE ATANGAZA KIAMA KWA WAVAMIZI WA MSITU KYOSA HEKTA 600

Image
Wananchi vijiji vya Ndapwa kata Ngulilo wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe na Kijiji Cha Kiobo wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya wametakiwa kuondoka na kuacha na uvamizi kwenye hifadhi ya  msitu Kyosa uliopo Kijiji Cha Ndapwa wilayani Ileje Kwa kufuata kanuni na Sheria za misitu. Agizo hilo limetolewa Oktoba 3,2023 na mkuu wa wilaya ya Ileje Farida Mgomi wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji Cha Ndapwa kwenye mkutano wa hadhara kwenye kampeni ya oparesheni ya uhifadhi wa misitu uliondaliwa na ofisi ya wakala wa huduma za misitu Tanzania shamba la miti  Iyondo Mswima wilayani humo (TFS). Mgomi amesema uvamizi kwenye hifadhi hiyo umefanywa na wananchi kinyume na taribu na kupelekea zaidi ya hekta 600 sawa na asilimia 60 kati ya zaidi ya hekta 1000 hali ambayo inahatarisha kupoteza uoto wetu. "Kutokana na uharibifu huo nitoe tamko Kwa wananchi wote waliovamia hifadhi ya msitu wa Kihosa waondoke mara Moja licha ya kwamba shughuli zao zinafanywa usiku serikali Iko macho itawashughulikia,&q

RAIS DKT SAMIA AMEFANYA TEUZI ZA MADC NA WAKURUGENZI PIA UHAMISHO WA VITUO VYA KAZI

Image
 

BREAKING NEWS. CHIFU NZUNDA AFARIKI DUNIA

Image
Chifu wa Kimila wa kabila la Wanyiha ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Machifu Mkoa wa Songwe na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Songwe Chief Muleshwelwa Nzunda amefariki Dunia siku katika hospital ya Mkoa wa Songwe alipokuwa akipatiwa matibabu. Taarifa hii imethibitishwa na ndugu wa marehemu Chifu Nzunda na taarifa kamili itatolewa baadae

TUNDUMA TC YATENGA BILIONI MOJA KULIPA FIDIA UJENZI BANDARI KAVU

Image
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauriya Mji Tunduma, Philemon Magesa, amesema Halmaahauri hiyo imetenga kiasi cha shilingi Bilioni moja kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi watakaoachia maeneo yao katika mtaa wa . .  kata ya Mpemba ili kupisha ujenzi wa bandari kavu . Alibainisha hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari  kutoka vyombo mbalimbali ambao walifanya ziara ya siku tatu kwa lengo la kujionea utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo , ikiwemo ile ya kimkakati . Magesa alisema katika kutekeleza mradi huo wa kimkakati Halmashauri hiyo imetenga kiasi hicho cha fedha kupitia mapato yake ya ndani kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024. Akifafanua zaidi,   alisema Mradi  huo utatekelezwa kwa pamoja kati ya Halmashauri hiyo na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) . "Sisi Tunduma tunampango wetu wa kujenga  bandari kavu na tulichokifanya ni kutafuta eneo na kulipa fidia ...halafu  TPA watakapokuja kwa kuwa wao ni wataalam wa bandari ndio watakaoweka miundombinu"

AKAMATWA KWA MADAI YA KUMUUA TUPAC

Image
  Mwanaume aliyetambuliwa kwa jina la Duane “Keefe D” Davis amekamatwa na Polisi, akihusishwa moja kwa moja na mauaji ya Rapa Tupac Shakur aliyepigwa risasi Mitaa ya Las Vegas, Marekani Licha ya Mashtaka yake kutowekwa wazi, taarifa zinaeleza kuwa Mashauri yote kuhusu kesi hiyo iliyodumu kwa takriban miaka 27 yatajulikana leo Septemba 29, 2023 Tupac alizaliwa Jijini New York Mwaka 1971, alijipatia umaarufu mkubwa kupitia muziki wa Hip Hop kutoka upande wa West Coast akitamba na ‘hits’ kama Do 4 Love, Hit Em Up, Dear Mama na California Love

MFAHAMU MSEMAJI WA SERIKALI ALIETEULIWA

Image
  Julia 2 mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan alimteua Mwanahabari Mobhare Matinyi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam. Miezi mitatu baadaye amemteua Matinyi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali. Matinyi mbali na kuwahi kuwa mkufunzi katika Kituo cha Diplomasia cha Musumbiji-Tanzania amekuwa mwanahabari na mchambuzi wa maswala mbalimbali mengi yakilenga kuitetea Tanzania. Pia amewahi kuwa na ukurasa – column katika gazeti la kiingereza la ‘The Citizen’ – The Eagle’s Eye na ameandika Makala mbalimbali kupitia gazeti la Jamhuri. Wengi wanamkumbuka Matinyi kwa uchambuzi wake tunduizi wa mabendekezo ya Chadema kuhusu Katiba mpya wakati huo akiwa kama Mshauri Mwelekezi huko nchini Marekani. Hata hivyo, kabla ya kuwa Mkuu wa Wilaya, Mwanahabari huyu kitaaluma, alikuwa akitumika kwenye jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika maarufu kama SADC. Kwa sasa Matinyi anaenda kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Gerson Msigwa, aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya

VIGOGO WATATU SUMBAWANGA WASIMAMISHA,TAKUKURU WAPEWA RUNGU

Image
 

DC ATEULIWA KUWA MSEMAJI WA SERIKALI,MKURUGENZI MAELEZO

Image
 

DED MBEYA APEWA SIKU 7 KUNG'OA MILANGO ISIOENDANA NA THAMANI YA MRADI

Image
  NAIBU Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Deogratius Ndejembi ametoa siku saba kwa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya kuhakikisha kuwa  milango iliyowekwa kwenye ujenzi wa Shule ya Msingi Tonya inabadilishwa ili kuendana na thamani ya fedha iliyotumika kwenye ujenzi huo. Mhe Ndejembi ametoa agizo hilo kwenye ziara yake ya kukagua shule tatu za msingi zinazotekelezwa kupitia mradi wa BOOST na shule mbili za sekondari zinazotekelezwa kupitia mradi wa maboresho wa SEQUIP jijini humo. Akiwa shuleni hapo, Mhe.Ndejembi amesema pamoja na kuona mradi wa shule hiyo mpya umekamilika lakini hajaridhishwa na baadhi ya maeneo ikiwemo baadhi ya milango kuanza kupasuka mapema na hivyo kuagiza milango hiyo kubadilishwa haraka ndani ya siku saba. "Nimefanya ziara kwenye shule tatu za msingi na mbili za sekondari, niwapongeze Jiji la Mbeya kwa kasi kubwa mliyonayo ya kutekeleza miradi hii iliyoletwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, haya mapungufu niliyoyaona niagize yafanyiwe kazi haraka na ndani ya si

AFANDE ASP DKT SHITINDI AONGOZA HARAMBEE YA UJENZI WA NYUMBA YA MAPADRE MBOZI MKOANI SONGWE

Image
 Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dkt. Sister Shitindi kutoka Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Septemba 30, 2023 ameongoza Harambee ya kuchangisha pesa kwa lengo la kukamilisha ujenzi wa nyumba ya  Mapadre  Jimbo kuu Katoriki la Mbeya Parokia ya Kristo Mfalme-Bara kwa Paroko Atilio Mbogela Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe. Hivyo, ASP Dkt. Shitindi akiwa kama mgeni rasmi katika harambee hiyo  aliwezesha kupatikana kwa kiasi cha shilingi  Milioni 15   kati ya Shilingi Milion  27, zinazohitajika ili kukamilisha ujenzi wa Kanisa hilo  Pamoja na ahadi mbalimbali zilizotolewa na waumini. Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP  Theopista Mallya alipata nafasi ya kuzungumza na waumini wa Kanisa hilo na kuwataka waumini hao na  jamii nzima kwa ujumla kipiga vita vitendo vyote vya USHOGA, USAGAJI, ULAWITI,  UBAKAJI na  RUSHWA  pamoja na vitendo vyote vya  unyanyasaji wa Kijinsia na Ukatili dhidi ya watoto.