Posts

Showing posts from September, 2024

SONGWE YAPOKEA MADAKTARI BINGWA WA DKT SAMIA

Image
Leo, Mkoa wa Songwe umeanza kampeni maalum ya huduma za kitabibu, ukishirikiana na timu ya madaktari bingwa waliotua mkoani kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi. Hafla ya uzinduzi wa huduma hizo imefanyika mkoani hapa, ambapo Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Happiness Seneda, alimuakilisha Mkuu wa Mkoa, Mhe. Daniel Chongolo. Katika hotuba yake, Seneda amepongeza juhudi za serikali katika kuboresha huduma za afya na kuwaletea wananchi huduma bora kwa kuwafikia hata kwenye maeneo ya pembezoni mwa mkoa. Huduma hizo zinatarajiwa kufanyika katika wilaya zote za mkoa wa Songwe, zikiwalenga wananchi wenye changamoto mbalimbali za afya Ambapo Seneda amewataka Wananchi kujitokeza Hospitali mbalimbali za Wilaya zote Mkoani Songwe kupata huduma za Madaktari Bingwa kwa huduma bora zaidi.

HIZI HAPA FURSA MUHIMU ZINAZOPATIKANA WILAYANI SONGWE

Image
Wilaya ya Songwe imejaliwa rasilimali nyingi ambazo zinafungua milango kwa fursa mbalimbali za kiuchumi. Moja ya sekta kuu ni uchimbaji wa madini, hasa dhahabu. Uchimbaji wa dhahabu umekuwa ukitoa ajira kwa wakazi wa maeneo hayo na pia kucha ngia katika pato la taifa. Serikali inahimiza uwekezaji katika sekta hii ili kuongeza uzalishaji na kuhakikisha madini yanachimbwa kwa njia endelevu. Mbali na uchimbaji, kilimo ni sekta nyingine inayochangia uchumi wa Wilaya ya Songwe. Mazao kama mahindi, kahawa, tumbaku, alizeti, na maharage yanalimwa kwa wingi, huku fursa za biashara na usindikaji zikiendelea kuongezeka. Kilimo cha matunda kama parachichi na machungwa pia kinashika kasi kutokana na uhitaji mkubwa kwenye masoko ya ndani na nje. Fursa nyingine ni katika sekta ya ufugaji, ambapo ufugaji wa ng'ombe, mbuzi, na kuku ni shughuli maarufu. Hii inatoa nafasi kwa uwekezaji kwenye mazao ya mifugo kama maziwa, nyama, na ngozi. Aidha, Wilaya ya Songwe ina utalii wa ndani unaoweza kuimarish

LIJUE KABILA LA WABUNGU TOKA MKOANI SONGWE

Image
 Wabungu ni mojawapo ya makabila madogo yanayopatikana katika Mkoa wa Songwe, hususan Wilaya ya Songwe. Wabungu wana asili ya jamii za Kibantu, ambazo zinapatikana sana katika maeneo ya kusini mwa Tanzania na sehemu nyingine za Afrika Mashariki na Kati. Hata hivyo, historia ya kabila hili haijafanyiwa utafiti mkubwa ikilinganishwa na makabila makubwa kama Wanyakyusa, Wasafwa, au Wanyamwezi. Asili na Lugha Wabungu wana asili ya Kibantu, na lugha yao, ambayo ni ya Kibungu, inafanana kwa kiasi fulani na lugha nyingine za Kibantu zinazozungumzwa kusini mwa Tanzania. Lugha hii inashirikiana msamiati na lugha za makabila jirani kama vile Wasafwa na Wanyiha, kutokana na mwingiliano wa kihistoria wa kijamii na kibiashara kati ya makabila haya. 👇👇👇👇( BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI) https://www.instagram.com/p/DAfQklQIUzVgs-t3Qani5xWxScbx2nvFf3DBNc0/?igsh=MWd1azJoYmI

MTI WA ITUNDA KIVUTIO KIPYA WILAYANI SONGWE

Image
  Ndani ya Wilaya ya Songwe, mti wenye umaarufu unajuolikana kama Itunda unasimama kwa ubora wake wa kipekee. Kilichoufanya mti huu kuwa wa kipekee ni jinsi unavyoota kutoka katikati ya mwamba mkubwa, jirani na uwanja wa mpira wa Mkwajuni. Huu si mti wa kawaida bali ni maajabu ya asili, umejipatia umaarufu miongoni mwa wenyeji na una uwezo wa kuwa kivutio cha kitalii katika wilaya hii. Wilaya ya Songwe inajulikana sana kwa shughuli zake za uchimbaji wa madini ya dhahabu, lakini Itunda ni kivutio kipya kinachotoa tafsiri tofauti ya uzuri wa Songwe. Mti huu mkubwa, wenye majani kibichi na matawi yanayotanda, ni alama ya utulivu na ukimya, ukitoa kivuli kwa wakazi wa eneo hilo wanaoutembelea kutafuta pumziko kutokana na jua kali. Watoto hupanda kwenye matawi yake makubwa, wakicheza na kufurahia kama vile wanavumbua ngome ya asili iliyojaa siri Kile kinachoufanya Itunda kuwa wa kipekee zaidi si tu jinsi unavyoota juu ya mwamba, bali pia ni uwezo wake wa kuwa alama ya utalii inayoweza kufun

SONGWE:VITONGOJI 90 KUANZA KUNUFAIKA NA UMEME WA REA,BILIONI 10.8.ZATOLEWA

Image
Katika juhudi za kuboresha huduma za nishati vijijini, serikali imetenga shilingi bilioni 10.8 kwa ajili ya mradi mkubwa wa kusambaza umeme katika vitongoji 90 vilivyopo ndani ya majimbo sita ya Mkoa wa Songwe. Mradi huu unalenga kuinua hali ya maisha kwa wakazi wa maeneo hayo kwa kuwezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika. Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo, wakati wa hafla fupi ya utambulisho wa Mkandarasi aliyepata jukumu la kutekeleza mradi huo. Hafla hiyo iliofanyika Septemba 26, 2024, katika ofisi za mkoa, ambapo kampuni ya China Railway Construction Electrification Bureau Group Co. Ltd kutoka nchini China ilizinduliwa rasmi kama mtekelezaji wa mradi huo. Mhe. Chongolo alibainisha kuwa mradi huo ni sehemu ya awamu ya tatu ya Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini (REA), unaoendelea kutekelezwa na serikali kwa lengo la kuongeza wigo wa upatikanaji wa umeme katika maeneo ambayo hayajafikiwa na nishati hiyo. "Huu ni mradi muhimu ambao utafungua fursa za

CHONGOLO AWACHARUKIA RUWASA NA TANESCO KUTOSHIRIKI ZIARA YAKE

Image
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo Amekasilishwa na kitendo  cha  Kutokuwepo katika ziara yake Tunduma kwa Wakuu wa Idara za RUWASA na TANESCO kusikiliza na kutatua kero za Wananchi. Katika ziara ya kikazi iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Tunduma, hali ya sintofahamu ilijitokeza baada ya wakuu wa idara muhimu za RUWASA na TANESCO kushindwa kufika ambapo Ambapo Chongolo alieleza kutoridhishwa kwake na kitendo cha viongozi hao kutohudhuria ziara hiyo na kumuagiza Katibu Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Happiness Seneda kuhakikisha Wakuu hao ziara zake wanakuwepo na kama hawawezi kusikiliza kero za Wananchi basi watafute Mkoa mwingine wa kufanya kazi. Katika hotuba yake mbele ya maafisa na wananchi waliokuwepo, mkuu wa mkoa alisisitiza umuhimu wa viongozi wa taasisi za umma kuwajibika na kuheshimu ratiba za ziara za kikazi, hasa pale zinapohusisha masuala ya huduma za msingi kama maji na umeme, ambazo ni muhimu kwa maendeleo ya wananchi. Alieleza kwamba kitendo cha kutokuwepo kwao ki

MKUU WA MKOA WA SONGWE ZIARANI TUNDUMA

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo, amefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Mji Tunduma mnamo tarehe 24 Septemba 2024. Ziara hiyo iliangazia kutatua changamoto za wananchi na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo. Akiwa katika mkutano wa hadhara, Mhe. Chongolo alisikiliza na kutoa ufumbuzi wa kero mbalimbali, akisisitiza ushirikiano kati ya serikali na wananchi katika kuboresha huduma za kijamii. Miongoni mwa miradi aliyotembelea ni kituo cha afya cha Chiwezi, ambacho kinajengwa kwa gharama ya zaidi ya Shilingi milioni 786. Kati ya fedha hizo, milioni 500 zimetolewa na serikali kuu, milioni 286 zimetokana na mapato ya ndani, na milioni 8 zimetokana na nguvu za wananchi. Ujenzi wa kituo hicho unajumuisha majengo ya huduma muhimu kama maabara, upasuaji, wodi ya mama na mtoto, chumba cha kufulia nguo, na chumba cha kuhifadhi maiti, pamoja na njia za kupitisha wagonjwa. Kituo hiki kitahudumia wakazi 10,540 wa Kata ya Chiwezi pamoja na maeneo jirani kama Kata ya Chindi (

TANROADS SONGWE YASHIRIKI UZINDUZI WA ROUTE MATCH ILEJE

Image
Tanroads Mkoa wa Songwe wameshiriki katika Uzinduzi wa Route match Mkoa wa Songwe iliozinduliwa 21 Septemba 2024 Wilayani Ileje sambamba na uzinduzi huo pia wameshirikia kufanya usafi Stendi ya Isongole na ghala la ununuzi wa mazao ambapo uzinduzi huo uliongozwa na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Happiness Seneda. Kiongozi wa kamati ya burudani na maafa Tanroads Songwe Sally Kubetta amesema ni kawaida yao Tanroads Songwe kushiriki katika michezo mbalimbali ili kuimalisha afya zao na kujiongea ufanisi zaidi katika utendaji wa Majukumu yao ya kiofisi. "Michezo kwetu Tanroads Songwe tunachukulia ni sehemu ya majukumu yetu na tupo tayari kuunga juhudi za Mkoa kama hizi Uzinduzi wa Route match na tutashiriki mwanzo mwisho" amesema Kubetta Katika hatua nyingine Kubetta ameomba kuandaliwe mechi ya mpira wa Miguu  dhidi Temesa Songwe kwani wao wanawahitaji Temesa kwao wanaona ndio wapinzani wao kisoka wapo tayari kuwafuata popote Temesa ambapo kwa mujibu wa taarifa Mtanange huo kabambe

ILEJE IMETISHA UZINDUZI ROUTE MATCH

Image
  Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Happiness Seneda ameongoza uzinduzi wa Route match Mkoani Songwe uliofanyika Wilayani Ileje katika Viwanja vya Mwenge vilivyopo Isongole. Katika uzinduzi huo ambao ulianzia na mbio fupi shule ya sekondari ya Ileje hadi Viwanja vya Mwenge katika uzinduzi huo mamia ya wakazi wa Ileje wamejitokeza kwa wingi huku kukiwa na kila aina ya mbwembwe toka kwa wakazi wa Ileje.

DED NAMTUMBO ATOA UFAFANUZI KUPUNGUA KWA IDADI YA VIJIJI TOKA 71 HADI 66

Image
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Namtumbo Philemon Magesa amesema kupungua kwa idadi ya Vijiji Wilaya ya Namtumbo inatokana na uwepo wa Miji Midogo ya Lusewa na Namtumbo hivyo kufanya idadi ya Vijiji Namtumbo kupungua Akimjibu Mwananchi wa Namtumbo alieuliza swali kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za Wilaya ya Namtumbo bwana Edson Ndunguru alitaka kujua kama idadi ya Vijiji 71 anavyovijua yeye vimepungua ama la? Ambapo Magesa ametoa ufafanuzi. "Ni kweli kabisa kuna Vijiji  vimepungua kutokana na uwepo wa Miji Midogo ya Lusewa na Namtumbo kiutaratibu Kijiji au Kata inapopata hadhi ya kuwa Mji mdogo haiwezi kuwa na Kijiji hivyo Vijiji viwili  vilivyokuwa katika hizo Kata vilipunguzwa  Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo imebakiwa na Vijiji 66 kutoka 71" amesema Magesa. Mkurugenzi Magesa amewashukuru Wananchi wanaouliza maswali kupitia kurasa za Halmashauri ya Namtumbo na ameahidi kuendelea kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yatakayo ulizwa

MAMA JANETH MAGUFULI AWASILI MBOZI KUHANI MSIBA WA NDUGU YAKE

Image
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Bi. Happiness Seneda amefika kumpokea Mama Janeth Magufuli ambaye amekuja Mkoani Songwe kwa ajili ya kuhani Msiba wa ndugu yake tarehe 18 Septemba, 2024 Katika Mji wa Mlowo wilayani Mbozi Mkoani Songwe