Posts

Showing posts from November, 2021

MTENDAJI WA KIJIJI ATOWEKA NA MICHANGO YA WANANCHI

Image
  Buchosa . Aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Lushamba kata ya Bulyaheke  halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema Mkoa Mwanza Jonathani Nyakai ametelekeza ofisi ya  Kijiji na kutoweka kusiko julikana baada ya kutuhumiwa na wananchi kutafuta kiasi cha Sh338,900 zilizo changwa na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha darasa shule ya Sekondari Lushamba. Sakala hilo limeibuka Novemba 29 mwaka huu kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge wa  Jimbo la Buchosa Eric Shigongo kwenye Kijiji cha Lushamba alipokuwa akisikiza kero za Wananchi. Mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Lushamba ambaye anakaimu nafasi ya mtendaji wa Kijiji cha Lushamba baada ya mtendaji kutoweka na fedha za wananchi, Nyamagambo Malima wakati anawasoma taarifa ya kijiji hicho amesema changamoto ya mtendaji kutoweka na fedha za wananchi imekuwa kero kwao. Amesema mtendaji huyo ametoweka sasa ni miezi saba hawajui alipo hivyo wananchi wanaziomba mamlaka husika kuchua hatua za kumtafuta na kurejesha fedha za wananchi. " Wan

MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 30,2021

Image
 

WANAFUNZI WATEMBEA MASAA 4 KUIFIKIA SHULE MBOZI, MWENYEKITI HALMASHAURI ASIKITISHWA

Image
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbozi George Musyani amelazimika kusafiri mwendo wa Masaa Matatu kukifikia Kijiji cha Ileya kata ya Namlonga Wilayani Mbozi kuongea na kusikiliza kero za Wananchi ambapo wamemuelezea kero Mbalimbali ikiwepo umbali wa Wanafunzi wanaopata kufika Shule iliopo Malena "Nimepata wasaha wa kufika Ileya Kitongoji Malena  Kijiji Namlonga Kata Nanyala WILAYA Mbozi. Ni mwendo wa masaa matatu tokea makao makuu ya Kata kwa gari na dk 75 kutembea kwa mguu. Masaaa hayo matatu ni Nanyala-Mbalizi-Mjele. Wananchi wana kiu ya kuwa na shule Yao maana kuna umbali wa masaa manne kutembea kutoka shule ya Msingi Malena kitu ambacho ni hatari  kwa usalama wa watoto. Watanzania hawa wanahitaji huduma  Tuwasaidie"-Mwenyeki Halmashauri ya Mbozi

MBOWE NA WENZAKE WAKWAMA MAHAKAMANI,

Image
  Dar es Salaam. Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imekubali pingamizi la mawakili wa Serikali la kutopokea barua kama kielelezo cha ushahidi wa upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya ugaidi inayomkabili Mwenyeki wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu. Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu Novemba 29, 2021 na Jaji Joachim Tiganga na kueleza kuwa mshtakiwa huyo Mohamed Ling'wenya hajaweza kuieleza mahakama ni kwa nini barua hiyo inamhuri wa naibu msajili. Jaji ameeleza kuwa katika mazingira hayo mahakama imeshindwa kuelewa kama hiyo barua aliyotaka kuitoa ndio hiyo iliyopelekwa kwa RPC.

SABABU ZINAZOWAFANYA WANAWAKE WAJIHUSISHE NA UKAHABA

Image
  Tumewaona wengi mitaani wakifanya kazi ambayo wananchi wengi hawaipendi na hata kuwakosoa kila mara. Makahaba wengi hupitia mengi huku wakitafuta riziki yao ya kila siku bali wengi hawajawahi jiuliza kwanini haswa wanawake hao wameamua kufanya mambo hayo. Si kila mwanamke anapenda kuuza mwili wake kwa ajili ya pesa lakini wengi hawana kazi au mahali pa kupata riziki ndiposa wanajiunga  na kazi hiyo. Hizi hapa baadhi ya sababu kwanini wanawake wengi ujiunga na kazi ya ukahaba. 1.Utambuzi wao ni taofauti  Kuna wale wanona kazi hiyo ina leta pesa badala ya kutambua changamoto za kazi hiyo na mwishowe majuto yake. 2.Tamaa Kuna wanawake ambao wanapenda pesa sana huku wasitosheke na pesa ambazo wanapata za kila mwezi, wanaona hamna haja ya kukaa nyumbani wanajiunga na kazi ya ukahaba na kuanza kupata pesa. 3.Hamu ya kuridhika  Wanawake wengi hujipata kuwa hawawezi kutosheka na mwanamume mmoja wanaamua kutumia mwili wao vibaya na kufanya ngono na wanaume wengi ili apate kuridhika. 4.Kuishi

MAGAZETI NOVEMBA 29,2021

Image
 

WALIMU NA WANAFUNZI WAPANGA FORENI CHOO KIMOJA

Image
  Sengerema. Shule za msingi nne katika Wilaya ya Sengerema zina upungufu wa vyoo hivyo kulazimika wanafunzi kutumia choo kimoja na walimu. Shule hizo ni pamoja na Kizugwangoma, Sengerema, Nyampulukano na Mweli ni zenye upungufu wa matundu ya vyoo 60 hali inayopelekea walimu na wanafunzi kutumia choo kimoja. Shule hizo zinazokadiwa kuwa na zaidi ya wanafunzi 4500 zimekumbwa na kadhia hiyo ya upungufu wa matundu ya vyoo hivyo kuleta adha ya walimu na wanafunzi kupanga foleni kwenye choo kimoja Ili kupishana kupata huduma ya kujistiri. Diwani wa Kata ya Mishine, Mbugai Majumba ametembelea shule ya msingi Kizugwangoma leo Jumapili Novemba 28, 2021 na kubaini shule hiyo kuwa na upungufu wa matundu ya vyoo 15. Shule ya Msingi Kizugwangoma yenye wanafunzi wanafunzi 1252 na walimu 28 ina matiundu ya vyoo 8 Kutoka na kukabilia na hali hiyo wadau mbalimbali wamejitokeza kutoa msaada wa vifaa mbalimbali ili kusadia shule hizo lengo ni kuondoa foleni za walimu na wanafunzi kutumia choo kimoja.

JINSI YA KUCHANGANYA VIUNGO NA KUCHOMA KUKU

Image
C  Kuku wa kuoka Mahitaji  MAHITAJI Kuku Chumvi Tandori masala  Kotimiri  Chicken masala  Curry powder  Thoum tangawizi  Uzile  P.manga  Ndimu Kata kuku vipande vioshe vizuri kisha weka spices nilizozitaja hapo then changanya uzuri na kuacha kwa masaa 2 kisha panga kwenye trea na kuchoma kwa oven  mpaka walipoiva nikatoa tayari kwa kula..enjoy

NAPE AMSHUKIA POLEPOLE ATAKA KUWAJUA WAHUNI

Image
  Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amemtaka Mbunge wa kuteuliwa, Humphrey Polepole kuwataja watu aliowaita kuwa ni wahuni aliosema hawakushughulikiwa wakati wa utawala wa Awamu ya Tano. Kauli ya Nape imekuja kufuatia mahojiano aliyofanya Polepole na kituo cha televisheni cha Wasafi ambapo pamoja na mambo mengine, alisema udhaifu wa Serikali ya Awamu ya Tano ni kushindwa kuwamaliza wahuni. Akitoa maoni katika ukurasa wake wa Twitter, Nape alihoji kama kulikuwa na orodha ya wahuni wanaoshughulikiwa. “Duh! Kumbe kulikuwa na orodha!!Man gesturing (mtu anaashiria) ok, Natamani kujua wahuni waliopona! Rolling on the floor laughing (nabiringika sakafuni nikicheka). Hata alipoulizwa kwa simu na Mwananchi leo Jumamosi Novemba 27, 2021 Nape alikiri kuandika ujumbe huo akisema, “Mimi nadhani mchukue tu hiyo tweet. Nimeuliza, kumbe kulikuwa na orodha na hao waliobaki ni kina nani?”

Ahukumiwa Kifo Kwa Kupeleka ‘SQUID GAME’ SHULE

Image
  Taarifa za kusikitisha kutoka nchini Korea Kaskazini, ambapo jamaa mmoja aliyesafirisha kwa magendo filamu ya ‘Squid Game’ na kuuza kopi za filamu hiyo kwa wanafunzi nchini humo, amehukumiwa kifo.   ‘Squid Game’ ni filamu ya Kikorea iliyotikisa dunia ambayo inaeleza namna watu wenye hali ngumu ya kimaisha  walivyojikuta kwenye mchezo hatari wa watoto wakiwania fedha ambapo vifo vinahusika ili mshindi apatikane, Korea imegawanyika ambapo Korea Kaskazini inaongozwa na Kim Jong-un huku Korea Kusini ikiongozwa na Moon Jae-in.   Ripoti zinaeleza kuwa, hukumu hiyo ya kifo itakuwa ni ya kupigwa risasi, tayari mwanafunzi ambaye alinunua kopi ya filamu hiyo amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani, wakati huohuo wanafunzi sita waliokuwa wanaangalia filamu hiyo wamehukumiwa kifungo cha miaka mitanbo jela sambamba na kazi ngumu, huku walimu na viongozi wa shule wakifukuzwa kazi na kupewa adhabu ya kufanya kazi migodini. Hizi hukumu ni sahihi?

MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 27 2021

Image
 

RC SONGWE ASHIRIKI MISA YA SHUKRANI YA ASKOFU MSAIDIZI ILIOFANYIKA VWAWA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba ameshiriki pamoja na waumini wa Kanisa la Roma Katoliki Adhimisho la Misa Takatifu ya Shukrani ya Askofu Msaidizi Stephano Msomba  wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Misa hiyo imefanyika katika Parokia ya Mt. Patrick  Vwawa lililopo Wilaya ya Mbozi katika Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya Leo Novemba 26. Misa imeongozwa na  Mhashamu Askofu msaidizi Stephano Msomba akishirikiana na Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo kuu katoliki la Mbeya Na Raisi wa Baraza la Maaskofu Tanzania Gervas Nyaisonga. Katika hotuba yake Mkuu wa Mkoa amewaomba Maaskofu Mambo mawili kwanza ni kuhusu Lambalamba ambapo amesema kumeibuka kundi kubwa la Imani za kushirikiana Mkoani Songwe na pia wapo waumini wanaoshiriki Vitendo hivyo ameomba kupitia Maaskofu kuwakumbusha Waumini uwepo wa Mungu na kuwaonya kuacha mara moja tabia ya ramli chonganishi.aidha pia amewaomba Maaskofu kusaidia kuwaeleza Waumini kuhusiana na Janga la ukataji miti Mkoani Songwe na Uchimbaji mikaa kuwa hivi sasa vite

MJUE DEREVA WA BASI LA MAJINJAH ANAETREND NJIA YA DAR-SUMBAWANGA

Image
  Kampuni ya Mabasi ya Majinjah Special hivi sasa ndio Kampuni pekee inayosifika kwa Usafirishaji wa abiria na Mizigo Nyanda za Juu Kusini ambapo Kampuni hii inamilikiwa na Mkurugenzi wake anaefahamika kwa jina la Alnanuswe Kabungo. Leo niamua kukuangazia njia Dar es Salaam hadi Tunduma ambapo ndani ya basi namba T 961 DNE nakutana na Dereva kijana ambae anaoneka muda wote akiwa  bize na Majukumu yake. Boniface Charles Jimora ni Dereva aliejizolea umaarufu kutokana na basi lake kuwa ni moja ya basi pendwa na abiria wengi wamemuelezea Bonifce kwa mitazamo tofauti. Sakina Ally ni Mkazi wa Tunduma yeye amedai kuwa amekuwa mteja Mkongwe wa Boni toka anaiendesha T 422 BUL "Ni Dereva mcheshi sana na mtu wa stori sana hapendi kuona abiria wake wamenuna na pindi anapokuwa haendeshi gari basi hupita kila siti na kutaka kujua changamoto kama zipo kwa abiria" Nae Mzee Abiudi Mwinuka ambaje amejitambulisha kama mfanyabishara Sumbawanga amesema moja ya madereva waliotulia katika Uendeshaj