Posts

Showing posts from May, 2022

MWANDISHI WA HABARI SONGWE ANYAKUA TUZO YA UANDISHI

Image
 Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Serikali  Baraka Messa toka Mbozi Mkoani Songwe amepata  tuzo ya uandishi habari za ushirika 2021 zilizoandaliwa na EJAT. Baraka Messa ambae ni Maarufu Mkoani Songwe kwa Uandishi wa Makala Mbalimbali za Kijamii alikuwa ni Mwandishi pekee toka Mkoani Songwe aliepata nafasi ya kuteuliwa na Jopo la Majaji kushiriki Tuzo hizo na kuwa ni miongoni mwa Washiriki 6 walikuwa wakichuana nafasi Moja. Sisi kama HABARI JAMII TANZANIA tunampongeza Mwandishi Baraka Messa kwa Tuzo hiyi

WIZI WA BATA WASABABISHA KIJANA ACHOMWE MOTO MBOZI

Image
  Kijana mmoja aliefahamika kwa  jina lameck sannsumbi (25)Mkazi wa Kata ya Idiwili amechomwa moto hadi kufariki na Wananchi wenye hasira kali Kata ya Ilolo baada ya kudaiwa kuvunja banda la bata na kuiba inadaiwa kuwa Marehemu  alikwenda kumsalimia bibi yake Mkazi wa Ilolo aliefahamika kwa jina la Tabita Kayange (63)na alimjeruhi bibi huyo kwa kumpiga na kumuumiza maeneo ya jicho la kushoto. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Jannet Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema Marehemu Lameck wakati akitekeleza tukio la Uvunjanji wa Banda la kufugia bata bibi yake alipomuona alimjeruhi kwa kumpiga ndipo bibi huyo alipiga kelele na Wananchi wakajitokeza na kuanza kumshambulia Mwizi huyo na kisha kumchoma moto hadi mauti ilipomkuta. Kamanda Magomi amewataka Wakazi wa Mkoa wa Songwe kutojichukulia sheria Mkono na pindi wanapoona Vitendo vya kihalifu katika maeneo yao watoe taarifa kwa jeshi la Polisi. aidha amesema jeshi la Polisi linaendelea na Uchunguzi wa tukio hilo

POLISI SONGWE WATOA SABABU ZA MFANYABISHARA SONGWE BARAKA SANGA KUJINYONGA

Image
 Jeshi la Polisi Mkoani Songwe limetoa taarifa ya kifo cha kujinyonga cha Kijana Maarufu Mkoani Songwe na Mfanyabiashara anaefahamika kwa jina la Baraka Sanga maarufu kwa jina la  Twangara aliejinyonga kwa kutumia Shuka jeupe. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Jannet Magomi amesema Baraka  Sanga amekutwa amejinyonga mida ya saa kumi na mbili na robo asubuhi kwa kutumia Shuka. "Tumepata taarifa ya Kujinyonga kwa Kijana anaeitwa Baraka Isack Sanga Kabila lake Mkinga katika kata ya Ilolo amejinyonga na taarifa zetu za kiuchunguzi marehemu amejinyonga kutokana na Ulevi wa kupindukia baada ya kuachwa na Mkewe na Marehemu hakuacha Ujumbe wowote" amesema kamanda wa Polisi Songwe Jannet Magomi. Baraka Sanga alikuwa ni Mfanyabiashara wa Duka maeneo ya njia panda ya Kuelekea Stendi ya Starehe Wilayani Mbozi na alikuwa maarufu kutokana na Ucheshi wake mbele ya Jamii hususani Vijana. Bwana alitoa na Bwana ametwaa Pumzika Kwa Amani Baraka Sanga

GARI LILILOBEBA MAGENDO LAPATA AJALI SONGWE LIKIWAKIMBIA KIKOSI KAZI CHA MKOA WA SONGWE

Image
Gari aina ya Brevis lenye namba za usajili T 265 CYN limepata ajali maeneo ya Ichenjezya Vwawa Wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe likiwa limebeba Magendo mbalimbali vikiwemo Vipodozi na Vitenge. Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo Jumapili ambapo mashuhuda wa ajali hiyo wamedai gari hilo lilikuwa mwendo kasi na limezima taa na ndipo lilipokuta na tuta lililopoka katika barabara hiyo na kisha kupaa na kudondoka huku matairi yakielekea juu. Akitoa taarifa Meneja wa Tra Mkoa wa Songwe Dikson Qamala amesema gari hilo lilikuwa nikiwakimbia kikosi kazi cha kuzuia na kupambana na Magendo kilichoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe Omary Mgumba. "Hili gari lilikimbia kizuizi chetu tulichokiweka Oldvwawa na kukigonga ndipo lilipopasua matairi yake mawili na katika kututoroka alikimbilia njia ya Ichenjezya na ndiko alipopata hii ajali na pia kuna gari  tumelikamata aina ya Crown T 510 DYC ambalo lilikuwa likiisindikiza gari iliopata ajali na lenyewe tumelikamata na Vitenge na Vipodozi" amese

BREAKING NEWS: NCCR MAGEUZI YAMSIMAMISHA MBATIA

Image
  Halmash auri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi imemsimamisha Mwenyekiti wa Chama hicho, James Mbatia na makamu Mwenyekiti Bara, Angelina Mtahiwa kutojihusisha na shuhhuli zozote za chama hadi mkutano Mkuu utakapoitishwa ili wajieleze kuhusiana na tuhuma inazowakubali. Uwamuzi huo umefanyika leo Jumamosi Mei 21, 2022 kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kugombanisha viongozi na kulazimisha kujiuzulu. Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Mwenyekiti wa azimio hilo, Joseph Selasini amesema pamoja na kusimamishwa kwa viongozi hao pia wamelivunja Baraza la Wadhamini la NCCR  na kuteua wajumbe wapya ambao watasajiliwa kwa mujibu wa taratibu zitakazowekwa Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Sisty Nyahoza amesema walipokea barua kutoka NCCR-Mageuzi kuwa kuna mabadiliko ya wajumbe wa bodi ya wadhamini. Amesema pamoja na mabadiliko hayo kulikuwa na ajenda nyingine ambayo ni kusimamishwa kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti Bara kutokana na maazimio hayo wanasubiri barua rasmi ili kutoa taarifa. Naibu

BREAKING NEWS: CHADEMA YAWAFUKUZA RASMI UANACHAMA KINA MDEE

Image
 HALIMA MDEE NA WENZAKE 18 WAFUKUZWA RASMI CHADEMA - Baraza Kuu la CHADEMA usiku wa leo kuamkia Alhamisi (Mei 12, 2022) limezitupilia mbali Rufaa za Halima Mdee na wenzake 18 za kupinga kufukuzwa uanachama na Kamati Kuu ya chama - Baraza hilo limeunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu ya chama wa kuwafukuza uanachama Halima Mdee na wenzake kwa kukubali kwenda kuapishwa na kuwa wabunge wa Viti Maalumu bila kupata baraka za chama

SERIKALI KUTOA BILIONI 100 KUPUNGUZA MAKALI YA BEI YA MAFUTA

Image
  Waziri wa Nishati, January Makamba amesema Serikali imetoa ruzuku ya Sh100 bilioni kwa ajili ya kupunguza bei ya mafuta nchini. Akizungumza Bungeni leo Jumanne Mei 10, 2922 Waziri  Makamba amesema ruzuku hii inatolewa kwa kupunguza matumizi ya Serikali katika kipindi kilichobaki cha mwaka2021/22. Amesema Kutolewa kwa ruzuku hiyo hakutagusa miradi ya maendeleo ambayo inaendelea “Rais wetu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo kwamba mwaka ujao wa fedha ni mbali. Ahueni itafutwe mapema zaidi. Hivyo basi, kama hatua ya dharura, katika kipindi hiki kabla hatujafikia mwaka mpya wa fedha, Serikali ijibane na ijinyime na zitolewe Sh100 bilioni kwa ajili ya kupunguza bei za mafuta hapa nchini. “Ruzuku hii ya Sh100 bilioni itatolewa kwa ajili ya kupunguza bei ya mafuta kuanzia Juni 1, 2022. Hii ni kutokana na kuwa, wafanyabiashara wa jumla wamekwisha lipia gharama ya mafuta ambayo imejumuishwa katika bei hizi za Mei 2022 na wafanyabiashara wa mafuta katika vituo wamekwishanunua maf

MAGAZETI YA LEO 10 MEI 2022

Image
 

MBUNGE WA MOMBA AINGIA NA GONGO BUNGENI

Image
  Mbunge wa Momba (CCM), Condester Sichalwe ameitaka Serikali kuzipima na kuzirasimisha pombe za kienyeji ikiwamo gongo ili kuwasaidia kiuchumi wanawake wanaofanya shughuli hizo Condester hayo leo Jumatatu Mei 9, 2022 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2022/2023 huku akionyesha baadhi ya baadhi ya pombe za gongo ambazo amesema zimetoka nje ya nchi na zinauzwa hapa nchini. Mbunge huyo ameitaka Wizara hiyo kuunda bodi kama Wizara ya Kilimo ilivyounda Bodi ya Mazao Mchanganyik Amesema watu wanaonekana kunywa pombe za kienyeji wanaonekana kuwa hawana akili lakini ukinywa bia unaokena wa kisasa. Amesema hata katika balozi wamekuwa wakitenga fedha kwa ajili ya kununua pombe za bei ghali lakini ukizionja hazina ladha ya tofauti na gongo “Tunajiuliza ni kwasababu hizi zina jina la kizungu na hizi ni za kibantu. Bodi hii itakapounda itasaidia kwenda kupima viwango vya kilevi vilivyopo. TBS (shirika la Viwango Nchini),

BREAKING NEWS: GARI LA OFISI YA RC SONGWE LAKAMATWA KWA MAGENDO

Image
Magari 14 yamekamatwa katika Oparesheni Maalumu ya kupambana na magendo katika Mpaka wa Tunduma kupitia Kamati ya ulinzi na Usalama iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe. Kati ya Magari hayo 14 ambayo yamekamatwa gari moja linamilikiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe likiwemo gari ambalo limekuwa likitafutwa kwa miaka mingi bila Mafanikio. Hapa Rc Mgumba anatoa msimamo wa Serikali juu ya magari yaliyokamatwa na wale wote watakao kamatwa na magendo kwa mkoa wa Songwe. Aidha Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Songwe ametoa wito kwa Wafanyabiashara, kufuata sheria za forodha na kueleza changamoto wanazopata wakati wa kudhibiti magendo katika Mpaka wa Tunduma.

RC SONGWE AWATAKA WAKUU WA WILAYA KUJIRIDHISHA KABLA YA KUWAWEKA WATU NDANI

Image
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amewataka wakuu wa Wilaya kujiridhisha na kosa ambalo mtu yeyote au mtumishi wa umma amefanya kabla ya kuchukua hatua ya kumuweka ndani kwa saa 48. Mkuu wa Mkoa ametoa wito huo kwenye maadhimisho ya sikukuku ya wafanyakazi ambayo kwa ngazi ya Mkoa imefanyika katika Mji wa Tunduma, 1 Mei 2022. "Lazima tujiridhishe kosa linaloweza kuhatarisha Amani ya sehemu hiyo au usalama wa Taifa na ukimweka ndani kwa adhabu hiyo hakikisha anatakiwa apelekwe Mahakamani" Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba. Mkuu wa Mkoa amesema kama kuna mtumishi amefanya kosa la jinai lazima akamatwe na apelekwe Mahakamani lakini kama ni kosa la kiutumishi ni lazima lirudi katika mamlaka yake ya utumishi ili wamchukulie hatua za kinidhamu Aidhaa, Mkuu wa Mkoa amesema wakati mwingine mtu anawekwa ndani kwa sababu ya usalama wake baada ya Serikali kujiridhisha  usalama wake uko hatarini. Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa ametoa vyeti kwa Wafanyaki bora katika ka

HABARI KUBWA MAGAZETI YA LEO

Image