Posts
Showing posts from February, 2024
MADIWANI IRINGA WAOMBWA KONDOMU VILABU VYA POMBE ZA KIENYEJI
- Get link
- X
- Other Apps
ONGEZEKO la uzalishaji wa pombe ya kienyeji aina ya ulanzi na mahusiano yake na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) limewaibua baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wakitaka usambazaji wa kondomu katika vilabu vinavyouza pombe hiyo kuongezwa. Madiwani hao wameiomba kamati ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Ukimwi kuhakisha mipira hiyo ya kiume haikosekani katika maeneo hayo na mengine yote hatarishi. “Ulanzi ni moja ya kilevi ambacho tafiti mbalimbali zinaonesha kimekuwa kichocheo cha ngono zisizo salama na matokeo yake ni ongezeko la maambukizi ya VVU na magonjwa mengine ya ngono. ” alisema mmoja wa madiwani hao, Vumilia Mwenda. Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani lililofanyika leo katika ukumbi wa Halmashauri hiyo, Ihemi, Mwenda alisema kuna ongezeko kubwa la uzalishaji wa pombe hiyo katika kipindi hiki cha mvua za masika. Pombe hiyo iliyogunduliwa wakati wa utawala wa machifu wa kabila la Wabena katika Wilaya ya Njombe baada ya mti mchanga wa mwanz
MAJALIWA AMUWEKA NDANI MAHASIBU KWA UPOTEVU WA MILIONI 213
- Get link
- X
- Other Apps
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, ACP Salum Morcase kumkamata Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Saad Matunzi kwa kosa la kuhamisha fedha Sh milioni 213.748 kwa matumizi binafsi. Majaliwa ametoa agizo hilo leo jioni alipozungumza na madiwani na watumishi wa halmashauri hiyo mkoani Mara. Imeelezwa kuwa fedha hizo zilihamishwa kwa awamu nne, kwa njia ya uhamisho wa ndani, ambapo mhasibu huyo alishirikiana watumisi wa Ofisi ya Rais Tamisemi. Mkamate huyo bwana sasa hivi aende polisi akafunguliwe mashtaka, huyu ni wakupeleka mahakamani moja kwa moja, DPP aelezwe afungue jalada la mashtaka, wale wenzake tumewapeleka mahakamani tayari, kwasababu tulibaini walihusika na wizi kama huu kwenye Manispaa ya Kigoma mwaka jana”. amesema Waziri Mkuu.
MWANAJESHI WA MAREKANI AJICHOMA MOTO NJE YA UBALOZI WA ISRAEL
- Get link
- X
- Other Apps
Mwanajeshi wa jeshi la anga la Marekani aliyejichoma moto mbele ya ubalozi wa Israel mjini Washington DC amefariki dunia. Mwathiriwa, ambaye alikuwa mfanyakazi wa anga akiwa kazini, alijichoma moto katika kitendo kinachoonekana cha kupinga vita huko Gaza. Alikuwa amesema “hatashiriki tena katika mauaji ya halaiki,” kulingana na shirika la habari la AP. Msemaji wa Jeshi la Wanahewa Ann Stefanek alisema mtu huyo “alifariki kutokana na majeraha yake na kuaga dunia jana usiku.” Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa. Mwanamume huyo alienda kwenye ubalozi siku ya Jumapili na kuanza kurusha tukio hilo moja kwa moja kwenye jukwaa la utiririshaji la video Twitch, ripoti hiyo ilisema, ikimnukuu mtu anayefahamu suala hilo. Kisha akajimwagia mafuta kwa kasi na kuwasha moto, kabla ya kuanguka chini.
WAZIRI MKUU AJIUDHULU PALESTINA
- Get link
- X
- Other Apps
WAZIRI Mkuu wa Palestina, Mohammad Shtayyeh ametangaza kujiuzulu. Akitangaza uamuzi huo leo, Shtayyeh amesema uamuzi huo unatokana na serikali yake kutawala sehemu za Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu. “Ninawasilisha kujiuzulu kwa serikali kwa Rais (Mahmud Abbas),” Shtayyeh amesema, na kuongeza kuwa inakuja kutokana na vurugu katika Ukanda wa Gaza na kuongezeka kwa Ukingo wa Magharibi na Jerusalem”. “Ninaona kwamba hatua inayofuata na changamoto zake zinahitaji mipango mipya ya kiserikali na kisiasa ambayo inazingatia ukweli huko Gaza na haja ya makubaliano ya Palestina kulingana na umoja wa Palestina.” aliongeza.
WIZI WA MIFUKO YA SARUJI WAMSHANGAZA WAZIRI MKUU
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekemea vitendo vya wizi na uzembe kwenye usimamizi wa ujenzi wa miradi ya umma nchini. Waziri Mkuu amesema hayo leo Februari 26, 2024, alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mara, iliyopo kata ya Buramba, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara. “Tumeshaibiwa mifuko zaidi ya 600 kwenye ujenzi wa Shule hii ya Sekondari ya Wasichana ya Mara. Hakuna usimamizi, hakuna anayejali. Mngeanza kuchukua hatua ninyi wenyewe halmashauri kabla hata Mkuu wa Mkoa hajaja,” amesema. Majaliwa amesema haridhishwi na utendaji kazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda hususani suala la usimamizi wa miradi ya maendeleo. “Watu wanaiba mara ya kwanza, mara ya pili mmeshindwa kuchukua hatua za kuwadhibiti wasirudie tena? Halafu si hapa tu, hata hospitali ya wilaya ina matatizo mengi, mmeshang’oa na milango iliyofungwa, mmeshaiba na vifaa tiba ikiwemo mashine ya X-Ray. Sasa nyie Bunda mkoje?” Amehoji Waziri Mkuu.
ABIRIA ADAIWA KUMUUA KONDAKTA WA DALADALA KWA KUMCHOMA KISU WAKATI WAKIDAIANA TSH 100
- Get link
- X
- Other Apps
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linamshikiria Venance Patrick Ngonyani (28) Mkazi wa mtaa wa Mahenge, anayetuhumiwa kumuua Hussein Mohammed Anafı (21) Kondakta wa Daladala yenye namba za usajili T.332 BXR TOWN ACE, wakati wakidaiana Shilingi 100 ikiwa ni sehemu ya nauli katika Daladala hilo. Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Marco G. Chilya amesema kuwa tukio limetokea Febuari 25, 2024 majira ya saa 12 jioni maeneo ya Mkuzo stendi iliyopo kata ya Msamala Manispaa ya Songea, ambapo marehemu alikuwa kwenye Gari ambayo alikuwa akifanyia kazi, Mtuhumiwa alipanda Gari hiyo kama abiria wengine na wakati wa kudaiwa nauli Mtuhumiwa alilipa nauli pungufu ya Shilingi 500/= badala ya 600/= ambapo kilichopelekea marehemu kumtaka Mtuhumiwa kulipa nauli stahiki kitendo ambacho kilisababisha malumbano na ugomvi baina yao ndipo Mtuhumiwa alipochomoa kisu alichokuwa kakificha kiunoni na kumchoma shingoni na kumsababishia kifo Kondakta huyo. Aidha kamanda Chilya a
KIHENZILE:AITAKA TAA KUVUNJA MKATABA NA MKANDARASI
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile ameelekeza mamlaka wa viwanja vya ndege Tanzania (TAA) kuvunja mkataba na Mkandarasi anayejenga jengo la abiria la kiwanja cha ndege cha Ruvuma kutoka na Mkandarasi huyo kushindwa kukamilisha jengo hilo kwa wakati. Kihenzile ameyasema hayo baada ya kutembelea na kukagua maboresho makubwa yaliyofanywa katika uwanja wa Ndege wa Songea. “Serikali imewekeza bilioni 37 katika uwanja wa ndege huu, hivyo ni muhimu jengo la abiria likamilike kwa haraka. Nauelekeza uongozi wa TAA kuvunja mkataba na Mkandarasi anayejenga Jengo la Abiria kwani ameshindwa kukamisha kwa wakati ,Alisema Kihenzile Jengo hilo la abiria lilitakiwa kukamika mwezi wa sita mwaka jana lakini mkapa sasa lipo asilimia 30 na Ujenzi wake unathamani ya shilingi milioni mianne ishilini na tatu (423) lakini ujenzi umesimama kutokana na changamoto za mkandarasi Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Songea Kapenjama Ndile amesema kuwa uwanja wa Ndege wa Songea ni muhimu kwa usafishaj
MTAMBO WA KWANZA WA UMEME WAANZA KUINGIZA MEGAWATI 235 GRIDI YA TAIFA
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Mashaka Biteko leo tarehe 25 Februari 2024 ameshuhudia kuwashwa kwa mtambo wa kwanza katika Mradi wa Julius Nyerere na kungiza megawati 235 kwenye Gridi ya Taifa. Akizungumza mara baada ya zoezi hilo amesema kuwa kuingia kwa megawati 235 kunafanya mgao wa umeme kupungua kwa asilimia 85 nchini. “Ninafurahi kusema kile ambacho tuliahidi kufikia tarehe 25 Februari tutakuwa tumeingiza umeme wa mtambo namba 9 kimekamilika,” amesema Dkt. Biteko. Amesema kuwa mtambo namba 8 unatarajiwa kukamilika mwezi Machi na kufanya jumla Megawati 470 kuingia kwenye Gridi ya Taifa. Ameongeza kuwa kazi ilipaswa kukamilika mwezi wa sita lakini kutokana na msukumo uliowekwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umefanya kazi kukamilika kabla ya wakati. “Tunamshukuru sana Mhe. Rais kwani wakati anaingia madarakani mradi huu ulikuwa asilimia 33, amefanya kazi kubwa kuhakikisha fedha za Mradi zinapatikana kwa wakati,” amesema Dkt. B
SILINDE AWATAKA WATAFITI WA KILIMO KUONGEZA KASI YA UTAFITI
- Get link
- X
- Other Apps
MOROGORO: WATAFITI wa kilimo nchini wametakiwa kuongeza kasi katika kufanya tafiti za kilimo kwa kuwa upo uhitaji wa upatikanaji wa mbegu bora kwa wakulima zenye kuendana na mabadiliko ya tabia nchi. Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde ameiwaambia watafiti hao alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI), Kituo cha Ilonga kilichopo Kilosa, Morogoro. “Kuna hitaji la upatikanaji mbegu bora kwa wakulima zenye kuendana na mabadiliko ya tabia nchi na kuhimili magonjwa. “Kutokana na hitaji hilo, watafiti mnapaswa kuongeza jitihada za kufanya tafiti na usambazaji teknolojia za kilimo ili kuongeza tija katika mnyororo mzima wa sekta ya kilimo,” amesema. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Thomas Bwana amesema taasisi hiyo imejipanga kutafiti na kusambaza teknolojia za kilimo zenye kukidhi mahitaji. Ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika kuandaa wataalamu wa kufanya tafiti zinazotatua changamoto mbalimbali za kilimo. Pia amesema TARI ina miundombinu ya kisasa ambayo inaendelea kub
KATAVI WAPOKEA TANI 30 ZA SUKARI
- Get link
- X
- Other Apps
MPANDA, Katavi: MKUU wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf amewataka wafanyabiashara mkoani Katavi kuzingatia bei elekezi ya sukari Sh 3200 kwa kilo moja na asiwepo wa kumuuzia mwananchi bei zaidi ya iliyoelekezwa. Akizungumza wakati wa upokeaji wa tani 30 za sukari mkoani Katavi, mkuu huyo wa wilaya amekiri kulikuwa na changamoto kubwa ya sukari wilayani humo hivyo ujio wa tani hizo utapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto hiyo wakati sukari nyingine ikisubiriwa kuingia wilayani humo kuanzia wiki ijayo. Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf Kiongozi huyo pia amewataka wananchi kutoa taarifa endapo watauziwa bei tofauti na iliyo elekezwa na atakayebainika kuuza kinyume na bei hiyo atachukuliwa hatua za kisheria. Naye, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Katavi, Florence Chrisant amesema kuanzia wiki ijayo mkoa utapokea tani 214 ambazo zitaondoa kabisa tatizo la uhaba wa sukari kwa asilimia 100 mkoani humo. Hata hivyo wananchi wa Mpanda wam
BITEKO AFUTA LIKIZO ZA WAFANYAKAZI TANESCO
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko ametangaza kufuta likizo kwa watumishi wote wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) akiwataka wote wawe kazini kukabiliana na changamoto ya upungufu wa umeme. Amesema hakuna mtumishi wa Tanesco atatakiwa kwenda likizo wakati huu wa changamoto ya mgawo wa umeme na kwamba, kila mmoja kwenye eneo lake atatakiwa kufanya kazi kwa bidii. Dk Biteko, ambaye pia ni Waziri wa Nishati ametoa agizo hilo leo Ijumaa, Februari 23, 2024 wakati alipotembelea chanzo cha kuzalisha umeme cha Kidato mkoani Morogoro. Naibu Waziri Mkuu huyo yupo kwenye ziara kukagua vyanzo vya kuzalisha umeme, kuangalia shughuli za uzalishaji ikiwa ni mkakati kumaliza changamoto ya upungufu wa umeme nchini. Hatua hiyo ya Dk Biteko imetokana na kupewa taarifa kwamba, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Morogoro, kuwa amekwenda likizo. “Huu ni muda wa kukimbiza kutatua changamoto zilizopo mbele yetu. Nitoe wito kwa uongozi wa Tanesco kuwa hakutakuwa na likizo kipindi hiki ambacho watanzania wanakabiliw
ALIEKUWA DED MBOZI AKAMATWA NA POLISI
- Get link
- X
- Other Apps
Ndugu waaandishi wenzangu muda huu nimefika kituo kikuu cha polisi kati na mawakili wa wawili wa OJADACT kufuatilia kukamatwa kwa Mwandishi wa habari kazimbaya makwega. Kwa bahati nzuri tumemkuta hapa kituoni na nimepata nafasi ya kuongea naye ana kwa ana kama dakika 5 hivi. Wakati naongea naye wakaja maafisa waliojitambulisha kuwa wanatoka ofisi ya RCO Dodoma na wamekuja kumchukua ili waondoke naye. Makwega Katika picha na spika Dkt Tulia Nao pia walikubali kuongea na mimi pia na sio mawakili nami nikafanya hivyo tukaongea na wakaniambia wanaondoka naye kwenda dodoma saa 7 mchana. Pia wakasema kuna tuhuma huko Dodoma za kujibu hivyo tuwe na amani kwani hizo ni tuhuma. Hapo nikawauliza kuwa kama.wanatoka Dodoma mbona tumeongea na ofisi ya RPC dodoma na ikathibitisha kuwa hakuna askari wake waliokuja Mwanza. Wao wakajibu kuwa ofisi ya RPC ni kubwa ila wao wanatoka ofisi ya RCO Dodoma. Maelezo toka kwa makwega mwenyewe ni kuwa alikamatwa jana kwao Malya na akanyang'anywa laptop
TANROAD WAAGIZWA KUMUONDOA MKANDARASI
- Get link
- X
- Other Apps
MOROGORO: Wakala wa Barabara (TANROADS) ameagizwa kumuondoa Mkandarasi wa Kampuni ya Kay Bouvet Engineering Ltd ya Nchini India na kumtafuta Mkandarasi mwingine mwenye uwezo na sifa za kujenga miundombinu ya barabara katika Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa aliyedai kutoridhishwa na utendaji wa Mkandarasi huyo. Amesema “Mkandarasi huyu ni mbabaishaji na tumeamua kumuondoa kwa kuwa hana mitambo ya kutosha ya kutekeleza kazi ya ujenzi wa barabara, pia hana sifa na uzoefu wa barabara kwa kiwango cha lami.” Baada ya hatua hiyo, Bashungwa ameuagiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS kutangaza zabuni ya mradi huo huku akisisitiza kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya kiwanda hicho alichosema kimechofikia 70% na kuwa kitasaidia kuongeza uzalishaji wa Sukari Nchini
MWENYEKITI CCM SONGWE AANZA KUUNGURUMA KATA KWA KATA KUSIKILIZA KERO
- Get link
- X
- Other Apps
DKT.BITEKO AKEMEA UCHELEWESHAJI HUDUMA KWA WANANCHI
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amekemea uzembe unaofanywa na baadhi ya watumishi wanaochelewesha huduma kwa wananchi ikiwemo kubadili transfoma zinazopigwa radi hasa katika mkoa wa Njombe. Kauli hiyo ya Dkt. Biteko ameitoa katika ziara yake katika mkoa wa Njombe jimbo la Wanging'ombe kufuatia changamoto iliyowasilishwa na mbunge wa jimbo la Wanging'ombe ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange ambaye amesema mkoa wa Njombe unachangamoto ya radi ambazo zinapiga transfoma na kusababisha mgao hivyo kukwamisha shughuli za uchumi kwa wananchi wa mkoa wa Njombe hususan ni Wanging'ombe. "Tunachangamoto kubwa ya radi kwa mwaka tunaweza kubadilisha transfoma 50,60 na kuendelea na mara nyingi transfoma ikiharibika inachukua miezi kadhaa umeme kuja kwa wananchi hii inaleta kero tunaomba transfoma zinanoweza kuhimili geografia Wanging'ombe na mkoa mzima wa Njombe". Amesema Akijibu hilo Dkt. Biteko amesema "mbunge
TAKUKURU WAAGIZWA KUWAKAMATA WALIOIBA VIFAA VYA SHULE
- Get link
- X
- Other Apps
MKUU wa Mkoa Dar es Salaam Albert John Chalamila ,ameagiza TAASISI ya Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)wilaya ya Temeke kuwamata viongozi wanaodaiwa kula pesa za miradi ya shule Sekondari Lumo wilayani Temeke. Mkuu wa mkoa Albert Chalamila alisema hayo wakati wa mkutano wa hadhara Jimbo la Temeke uliofanyika Viwanja vya Lumo baada kumaliza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kutatua kero mbali mbali za wananchi. “Ninaagiza TAKUKURU Temeke na OCD wa Temeke kuwamata walioiba vifaa vya shule katika shule ya sekondari Lumo wanaodaiwa wote wakibainika na hatia waende Mahakamani sheria ifuate mkondo wake maendeleo yoyote hayana chama awe wa Chama cha Mapinduzi CCM au Chama cha Maendeleo CHADEMA wakamatwe sheria iweze kufanya kazi yake” alisema Chalamila. Mkuu wa mkoa Chalamila alisema mali ya umma katika miradi ya Rais Samia suluhu Hassan kila mmoja aone maji ya Betri hayafai kunywa na katika mkoa wangu sitaki usanii waliohujumu majina yake tunayo wakamatwe mara moja . Katika hatua nyingi
RC AKAMATA SHEHENA YA MAFUTA YA MAGENDO
- Get link
- X
- Other Apps
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila Februari 21, 2024 ameueleza umma kupitia vyombo vya habari kukamatwa kwa shehena ya bidhaa za magendo, madumu ya mafuta ya kupikia zaidi ya elfu 11 Mbweni RC Chalamila amesema Kushamiri kwa magendo ni kiashiria tosha kuwa kuna baadhi ya watumishi wa umma wanaohusika hivyo ameagiza Jeshi la polisi na TAKUKURU bila kupepesa macho kuwakamata mara moja watumishi wote wa bandari ndogo ya Mbweni wahojiwe kwa kina ili ukweli ujulikane na hatua stahiki zichukuliwe. Aidha RC Chalamila amepongeza kazi nzuri inayofanywa na kikosi kazi katika ukanda mzima wa fukwe ya bahari ya hindi ambapo amesema kikosi kazi hicho kimejipanga vizuri kudhibiti biashara hizo za magendo ambazo zinatoka Zanzibar kuja Tanzania bara . “ Hatuwezi kuruhusu bidhaa za magendo kupenya katika Mkoa huu kwa kuwa ni hatari kwa usalama wa watu na Taifa kwa Ujumla” amesistiza Chalamila Naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Saad Mtambule amesema kati ya shehena za madumu ya mafuta z
WAZIRI MKUU AJIUZURU KONGO
- Get link
- X
- Other Apps
WAZIRI Mkuu wa DR Congo, Jean-Michel Sama Lukonde amejiuzulu. Lukonde aliwasilisha ombi la kujiuzulu kwa Rais Felix Tshisekedi. Sasa atajiunga na bunge kama mjumbe wa bunge hilo. “Kujiuzulu kumekubaliwa. Hata hivyo, rais ameiomba serikali (ya Lukonde) kuendelea kushughulikia masuala yaliyopo” hadi serikali mpya itakapoundwa, ofisi ya rais ilisema katika taarifa nyingine. Taarifa hiyo haikuweka wazi sababu za kujiuzulu kwake. Lukonde aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo ya Afrika ya kati yenye utajiri wa madini mnamo Februari 2021.
AUA MKE KISHA NAE KUJINYONGA KWA KUTUMIA KILEMBA
- Get link
- X
- Other Apps
Rashidi Hussein Mkayaga mkazi wa Mtaa Gemu, Kata ya Mwanga Kusini Manispaa ya Kigoma Ujiji, amejinyonga kwa kutumia kilemba cha kiume cha kuvaa kichwani, muda mfupi baada ya kumuua mke wake Bernadeta Cosmas kwa kumnyonga shingo hadi kufa kwa kile kinachodaiwa ni mgogoro baina ya wanandoa hao. Mwenyekiti wa Mtaa Gemu, Buswalu Mkama akizungumzia na waandishi wa habari eneo la tukio, amedai chanzo ni mgogoro wa muda mrefu na kwamba mwanamke huyo aliwahi kufika kwake na kutoa taarifa ya vitendo vya mume wake kuchukua vitu vya ndani na kuuza na mara kadhaa kesi hizo alizisuluhisha. Pia Mwenyekiti huyo amedai siku moja kabla tukio, mwanamke huyo alilala nyumbani kwake baada ya kukimbia kwa mumewe kufuatia kipigo alichopata na kwamba alinusurika kuuawa baada ya kukabwa shingo na waya wa umema, lakini alipopata nafasi ya kuchomoka alikimbilia kwake, kulipopambazuka alifuatwa na kaka yake aitwaye Isack Cosmas. Kwa upande wake Isack amesema siku ya tukio asubuhi alipigiwa simu na dada yake a
VIONGOZI TAASISI ZA SERIKALI MBIONI KUKOSA MSHAHARA
- Get link
- X
- Other Apps
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara yake kuzuia mishahara ya mwezi huu ya viongozi wa taasisi na idara za serikali, ambao mpaka sasa hawajaingia kwenye Mfumo wa Kielektoniki wa Usimamizi na Upimaji wa Utendaji Kazi Serikalini (PERMIS&PIMIS). Pamoja na kuzuia mishahara hiyo, amelitaka Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma kuja na ushauri utakaowezesha kuwepo kwa uwiano wa mishahara ya watumishi wa umma tofauti na hali ilivyo hivisasa ambayo tofauti yake ni kubwa. Amesema hayo leo wakati akifungua Baraza Kuu la Tano la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma linalofanyika mjini Iringa. Akizungumzia mfumo huo pamoja na ule wa Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimali Watu (HR Assesment), Simbachawene amesema mifumo hiyo kama ilivyoelekezwa na serikali ni muhimu katika kupima utekelezaji wa majukumu ya mtumishi kwa kuzingatia weledi na uwajibikaji wake, unaoendana na malengo yaliyowekwa