Machapisho

IGP WAMBURA AFANYA MABADILIKO MAKAMANDA POLISI

Picha
  MKUU wa Jeshi la Polisi, IGP Camillus Wambura amewahamisha mikoa ya kazi baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa huku mmoja akimhamishia Makao Makuu ya Polisi Dodoma. Katika taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP David Misime, waliohamishwa ni Kamanda Henry Mwaibambe kutoka Geita kwenda Tanga, na Kamanda Safia Shomary aliyekuwa Tanga amehamishiwa Mkoa wa Geita. Aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Temeke, Richard Ngole amehamishiwa makao makuu na nafasi yake imechukuliwa na Kungu Malulu aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rufiji

SERIKALI YAFUTA TOZO

Picha
  Hatimaye Serikali imesikia kilio cha Watanzania kwa kufuta na kupunguza kiwango cha tozo za miamala ya kieletroniki. Uamuzi huo umetangazwa leo Jumanne Septemba 20, 2022 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba bungeni baada ya kipindi cha maswali na majibu. Amesema Serikali imepunguza  wigo wa tozo , kuchochea matumizi ya miamala kwa ajili ya kupunguza fedha taslimu, kurahisisha utozaji na kuzuia kutoza tozo husika mara mbili. “Marekebisho yaliyofanyika ni kufuta  tozo  ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu (pande zote) na kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja (pande zote),”amesema. Dk Mwigulu ametaja marekebisho mengine ni kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda benki nyingine (pande zote). Amesema pia wafanyabiashara (merchants) hawatahusishwa kama ilivyo kwenye kanuni za sasa. Amesema pia wamesamehe  tozo  ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benki na ATM kwa miamala yenye ...

MWENGE WA UHURU WAACHA ALAMA YA MAISHA MOMBA

Picha
Pichani ni Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba, Mkuu wa Wilaya ya Momba fakii Lulandala,Mkurugenzi Regna Bieda na Katibu wa CCM Wilaya ya Momba wakionyesha furaha  Mwenge wa Uhuru kuweka jiwe la msingi katika Kituo cha Afya Msangano, 18 Septemba 2022. Wilaya ya Momba imekuwa ni moja ya Halmashauri zilizojipanga vizuri katika Mapokezi ya Mwenge wa UHURU na kujipanga vilivyo katika miradi yake huku Wananchi wake Momba wakiiupokea Kwa hamasa kubwa.

PANYA ROAD 135 WAKAMATWA DAR

Picha
  Jumla ya wahalifu 135 wamekamatwa ndani ya siku nne jijini Dar es Salaam tangu kuanza kwa operesheni ya kuzia uhalifu iliyoanza Septemba 15, 2022.  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Amos Makalla amesema wengi waliokamatwa vijana wenye umri kati ya miaka 14 na 30 waliobainika kuhusika na matukio ya uvamizi mitaani maarufu kama Panya Road. Makala amesema baada ya kuwakamata vijana hao walipohojiwa ilibainika viongozi wa magenge hayo baadhi yao waliwahi kutumikia vifungo mbalimbali magerezani. “Nilitangaza Septemba 15 kuwa tumeongeza askari 300 lakini watu hawa hawakutaka kusikia wakaenda kujaribu kule Makongo na Ubungo. Katika siku hizi nne, tumeweza kukamata vitu mbalimbali vya wizi vikiwemo runinga 23 na watuhumiwa 135 wamekamatwa wanaendelea na mahojiano. “Wamekamatwa pia wanunuzi wakubwa watano wa bidhaa za wizi,” amesema Makala”

WALIOUA POLISI WAHUKUMIWA KUNYONGWA

Picha
  Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imewahukumu washtakiwa wanne kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya kuua askari wawili wa Jeshi la Polisi Kituo cha Usoke, wilayani Urambo mkoani Tabora. Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa Septemba 16, 2022 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Tabora, aliyekasimiwa mamlaka ya ziada, Jovin Katto, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka. Waliohukumiwa adhabu hiyo ni Shedrack Hamis Rushikama, Sylvester Mussa Kingwendu, Abel Benedict na Ramadhani Kassim Manywele ambao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka mawili ya mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha. Hakimu Katto amesema mahakama hiyo pasipo shaka imewatia hatiani washtakiwa hao baada ya kupata ushahidi usiotia shaka. Awali, upande wa mashtaka ukiongozwa na Mawakili Meroto Ukongoji na Tunosye Luketa, uliiambia mahakama hiyo kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo, Aprili 28, 2014 usiku eneo la Usoke. Uliongeza kusema kwamba siku hiyo washtakiwa waliwaua Askari polisi w...

MBARONI KWA KUJIPATIA MILIONI 2.1 KWA JINA LA LUKUVI

Picha
  Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mtu mmoja ambaye ni mkazi wa Mabibo Jijini Dar es salaam (jina linahifadhiwa) akitumia jina la Waziri wa zamani, William Lukuvi kuendesha mafunzo ya ujasiriamali mkoani Kilimanjaro na kujipatia Sh2.1 milioni kupitia mafunzo hayo. Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Simon Maigwa amethibitisha kukamatwa kwa mtu huyo, akisema alikuwa akijipatia Sh35,000 kwa kila mshiriki wa mafunzo hayo huku akiwaahidi kuwalipia kila mmoja Sh300,000 kama ada baada ya kuhitimu mafunzo hayo na kwamba atawapatia ajira. Kamanda Maigwa amesema baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema wakati akiendesha mafunzo hayo katika ukumbi wa polisi Moshi, Jeshi la Polisi lilitumia mbinu za kumnasa mtu huyo. "Baada ya kupata taarifa hizi jeshi la polisi tuliwasiliana na viongozi ambao mtuhumiwa huyu alikuwa akiwataja ambapo walimkana na kwamba hawamjui, hivyo tunaendelea kumshikilia kwa hatua zaidi," amesema Kamanda Maigwa. Mtuhumiwa huyo amekuwa akiendesha ...

MBOZI KUJENGA KITUO CHA AFYA MILIONI 500 KWA MAPATO YA NDANI,MWENGE WA UHURU WAWEKA JIWE LA MSINGI

Picha
Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la msingi katika Kituo cha Afya Halungu ambacho kinajengwa kwa fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kwa kushirikiana na wananchi wa Kata ya Halungu. Kituo hicho ambacho Kukamilika kwake kitagharimu fedha milioni 500 lakini hadi sasa Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani wametumia milioni 367,660,000 kati ya izo nguvu za wananchi ni milioni 17,660,000.

DED IGUNGA AFARIKI DUNIA KWA AJALI

Picha
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Fatuma Latu amefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari katika eneo la Inyala, Mbeya. Ajali hiyo imetokea leo Jumatano, Septemba 14, 2022 wakati akiwa anatoka kwenye kikao cha Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) jijini Mbeya. Akizungumza na Mwananchi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Igunga, Lucas Bugota amethibitisha kutokea kifo hicho. Bugota amesema kuwa walikuwa wote kwenye safari lakini kwenye magari tofauti. "Mi ndio naelekea huko kwani wao walikuwa nyuma yetu, yaani ndio hivyo tumepata msiba" amesema

HALMASHAURI SONGWE ZATAKIWA KUTENGA FEDHA KWA AJILI YA KUTATUA KERO ZA WAALIMU

Picha
Na Baraka Messa, Songwe. NAIBU Katibu Mkuu Tamisemi upande wa elimu Charles Msonde amezitaka Halmashauri za mkoa wa Songwe  kutenga baadhi ya fungu la pesa zitokanazo na mapato ya ndani kwa ajili ya kuboresha Sekta muhimu ya elimu ikiwa ni pamoja na kujikita katika kutatua upungufu wa walimu wa elimu ya awali ambapo uwiano ni wanafunzi 300 kwa mwalimu mmoja mkoani Songwe. Dokta Msonde amesema hayo  leo (jana) wakati wa ufunguzi wa jukwa la kujadili Sera, changamoto, na fursa za watoto Sekta ya afya na na elimu .ambapo jukwa hilo limeshirikisha wadau mbalmbali ndani ya Mkoa, mikoa jirani, wizara za kisekta na wadau kutoka nje ya nchi. Alisema jamii ya Songwe ikielimika changamoto mbalimbali zinazo ukuumba mkoa huo kama vile udumvu, utapia mlo, vifo vya akina mama wajawazito na watoto kutokana na ukosefu wa lishe vitapungua kwa kiasi kikubwa kwa kuwa watakuwa na elimu itakayowasaidia kutambua mambno muhimu . “Maendeleo ya Taifa lolote lile hutokea kutokana na kutatua changamoto,...

WAALIMU SONGWE WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI KUTATUA CHANGAMOTO YA WANAFUNZI KUHITIMU BILA KUJUA KUSOMA

Picha
   Na Baraka Messa , Songwe. MKUU wa Mkoa wa Songwe Waziri Kindamba amewaagiza wasimamizi wa Elimu mkoa wa Songwe kuhakikisha wanatatua changamoto ya wanafunzi kumaliza elimu ya Msingi bila kujua stadi za kusoma , kuandika na kuhesabu. Mkuu wa Mkoa alisema Hayo wakati akiongea na wakuu wa Wilaya , wakurugenzi, waratibu elimu Kata pamoja na wadhibiti ubora wa Elimu katika Hafla ya uzinduzi wa Miongozo ya kuboresha elimu Mkoa wa Songwe. Alisema miongoni mwa changamoto katika Sekta ya elimu Mkoa wa Songwe ni wanafunzi wa darasa la kwanza kuingia darasa la pili bila kumudu stadi za kujua kusoma, kuhesabu na kuandika , Hivyo kusababisha wengine kuhitumu mpaka darasa la Saba bila kujua kusoma. "Waratibu elimu kawasimamieni walimu wakaongeze nguvu ya kufundisha na kuhakikisha mwanafunzi anayefikia darasa la pili anaweza kumudu stadi tatu za kujua kusoma , kuhesabu na kuandika Aliwataka waratibu elimu Kata kwenda kusimamia walimu kwenye kata zao kuwa na malengo ambayo yatasaidia kwa k...

MUUGUZI KORTINI KWA KUMBAKA NA KUMLAWITI BINTI WA MIAKA 17 ALIEKUWA ANAMTIBU

Picha
  Muuguzi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Amana jijini Dar es Salaam, Joseph Mwaipola (50) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu mashtaka matatu, yakiwemo ya kubaka na kulawiti mtoto wa miaka 17, ambaye alikuwa anamtibu. Mwaipola amefikishwa mahakamani hapo, leo Ijumaa Septemba 9, 2022 na kusomewa mashtaka yake na wakili wa Serikali Mwandamizi, Slyvia Mitanto mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Yusto Ruboroga. Katika mashtaka yao, Mwaipola anadaiwa Februari 2022 katika Hospitali ya Rufaa ya Amana, iliyopo wilaya ya Ilala, alimbaka na kumlawiti binti wa miaka 17, kinyume cha sheria. Pia, Mei 31, 2022 katika nyumba ya kulala wageni ya Pazuri Lodge iliyopo Temeke, jiji hapa, Mwaipola anadaiwa kumbaka binti huyo. Upelelezi wa shauri hilo umekamilika na Hakimu Ruboroga ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 5, 2022, kesi hiyo itakapoitwa kwa ajili mshtakiwa kusomewa hoja za awali.

VISHIKWAMBI KUTUMIKA KUBORESHA ELIMU NCHINI

Picha
       Na Baraka Messa, Songwe. VISHIKWAMBI kutumika kufundishia kuanzia shule za awali mpaka Sekondari kwa ajili ya kurahisisha ufundishaji na kutatua changamoto ya uhaba wa walimu unaoikumba sekta ya elimu kutokna na ongezeko kubwa la uandikishaji wa wanafunzi kuanzaia elimu ya awali baada ya eserikali kuanzisha mfumo wa elimu bure nchini. Hayo yamethibitishwa na Mkurugenzi sera na Mipango Wizara ya elimu Saynsi na Teknolojia Graceana Shirima wakati akijibu hoja za wadau katika Jukwa  la kujadili Sera, changamoto, na fursa za watoto Sekta ya afya na na elimu katika mkoa wa Songwe.ambapo jukwa hilo lilishirikisha wadau mbalmbali ndani ya Mkoa, mikoa jirani, wizara za kisekta na wadau kutoka nje ya nchi. Alisema kutokana na maendeleo ya Sayansi na teknolojia Serikali imejipanga kuwapa mafunzo walimu na ujuzi mbalimbali wa kutumia vifaa vya kufundishia yakiwemo mafunzo ya namna ya kutumia vishikwambi kufundishia katika shule zote kuanzia elimu ya awali mpaka Seko...

RAIS SAMIA ATANGAZA SIKU TANO ZA MAOMBOLEZO KITAIFA

Picha
 

WAKAZI WA SONGWE WAOMBWA KUCHANJA CHANJO YA UVIKO-19

Picha
 Mkuu Mkoa wa Songwe Mhe Waziri Kindamba amewataka Wakazi  Mkoani Songwe kuchanja chanjo ya Uviko-19 na kuachana na maneno ya kizushi kuhusiana na chanjo hiyo. Kindamba ametoa rai hiyo katika Ibada ya swala ya Ijumaa iliofanyika katika msikiti wa Mkoa wa Songwe wa Masjid Nuur uliopo Wilayani Mbozi. Akizungumka mara baada ya kukaribishwa na Sheikh wa Mkoa  Husein Batuza Mkuu wa Mkoa aliwashukuru na kujitambulisha rasmi kama Mkuu wa Mkoa wa Songwe aliepata Uteuzi hivi karibu na kumbadili Mhe Omary Mgumba ambae amehamishiwa Mkoani Tanga. Nae katibu wa Bakwata Mkoa wa Songwe ANNUARY ASHRAFF KHAN amewaomba Wakazi wa Songwe kumpa ushirikino Mkuu wa Mkoa Kindamba ikiwa na pamoja na kumsaidia kuzitangaza fursa mbalimbali za Mkoa huu

MAGAZETI YA LEO

Picha
 

POLISI WASEMA BADO WANAMSUBIRI TUNDU LISSU

Picha
  Ikiwa ni miaka mitano imepita tangu Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu kushambuliwa, Jeshi la polisi limesema bado linaendelea kumsubiria mwanasiasa huyo na dereva wake.  Lissu ambaye anaishi nchini Ubelgiji alishambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 Septemba 7, 2017 nyumbani kwake Area D jijini Dodoma akitoka kuhudhuria Mkutano wa Bunge. Baada ya shambulio hilo, Lissu alipelekwa Hospitali ya rufaa ya Dodoma kabla ya kuhamishiwa Nairobi nchini Kenya siku hiyo hiyo alikoanza kufanyiwa operesheni na baadaye kuhamishiwa nchini Ubeligiji anakoishi mpaka sasa. Katika mtandao wake wa Tweeter leo Jumatano Septemba 7, 2022 Lissu ameadika risasi 16, miaka mitano na operesheni 25 baadaye, bado nimewakomalia na mapambano yanaendelea miaka mitano, nabaki kujiuliza maswali. “Ni kwanini Serikali na Jeshi la Polisi hadi leo hawafanyi uchunguzi na kwanini nimenyimwa, nimenyimwa haki zangu za msingi ikiwemo matibabu,” Mwingine aliyetoa ujumbe unaofanana na Lissu ni Katibu Mkuu wa Chade...

MAGAZETI YA LEO

Picha