WALANGUZI WADAIWA KUVAMIA MBOLEA YA RUZUKU MKOANI SONGWE WAFICHA MBOLEA YA UREA
Wakulima wa mikoa ya Songwe na Mbeya, wanalalamikia kitendo wanachodai kuwa baadhi ya mawakala wanaficha mbolea ya ruzuku, hali inayowaletea usumbufu mkubwa. Baadhi ya wakulima mkoani Songwe, wanadai kuwa wapo baadhi ya mawakala hao walioanza kulangua mbolea ya kukuzia aina ya UREA kwa kuwauzia bei ya Sh90,000 badala ya Sh70,000 iliyotangazwa na Serikali. Mwananchi jana lilishuhudia foleni kubwa ya wakulima waliofika kununua mbolea hiyo kwenye moja ya duka la wakala wilayani Mbozi mkoani Songwe. Baada ya kuzungumza nao, walionyesha hofu ya kuwapo kwa mtiririko mdogo wa uingiaji wa mbolea ambao umekuwa chanzo cha kupata watu wachache. Mmoja wa wakulima hao, John Nzunda alisema ni zaidi ya wiki moja sasa kumekuwa na uhaba wa upatikanaji mbolea, hali iliyosababisha kuzuka kwa walanguzi ambao wanauza mbolea hiyo ya ruzuku aina ya UREA kwa bei ya Sh90,000 tofauti na ile iliyotangazwa na Serikali ya Sh70,000. “Tunahisi kuna ujanja, maana tukienda kwa mawakala wengi hawana mbolea matokeo...