SONGWE: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Dkt. Francis Michael ameunda timu maalumu ambayo itakuwa na kazi ya kutatua foleni ya Malori iliyopo katika Mji wa Tunduma, timu hiyo ni kutoka kwa madereva ambao watawakilishwa na vyama vyao, TANROADS, TRA, Jeshi la Polisi (RTO) na mawakala. Mkuu wa Mkoa ameunda timu hiyo baada ya kufanyika kikao kazi cha utatauzi wa foleni ya Malori kilichowakutanisha viongozi kutoka vyama vya madereva, wamiliki wa Malori, Mawakala wanaovusha magari, Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Wakala wa Barabara (TANROADS) Songwe, Jeshi la Polisi pamoja na viongozi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Wilaya ya Momba kilichofanyika ofisini kwake, Juni 14. Mkuu wa Mkoa amesema timu aliyoiunda inatakiwa kuwasilisha mapendekezo, maoni ya muda mfupi na ya muda mrefu kuhusu utatauzi wa foleni ya Malori kwa kuwa wao ndio wanazijua changamoto vizuri. "Kuna changamoto ambazo ziko ndani ya uwezo wetu hapa, hivyo nendeni mfanye kazi kwa pamoja na mje na majibu sahihi ya nini tu...