TUNDUMA YAWATAKA WATENDAJI WA MITAA NA KATA KUSIMAMIA USAFI
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma, Belton Garigo amewataka Watendaji wa Mitaa na Watendaji wa Kata wote katika Mji huo kusimamia zoezi la usafi katika maeneo yao. Garigo ametoa agizo hilo mapema leo tarehe 30 Septemba 2023 mara baada ya kumaliza zoezi la usafi wa mwisho wa mwezi lililofanyika katika Mtaa wa Kichangani Stendi Kata Chapwa nje kidogo ya Mji wa Tunduma. ( Kaimu Mkurugenzi Belton Garigo) "Ninawaagiza Watendaji wa Mitaa na Kata wote hakikisheni mnasimamia vema suala ya usafi katika maeneo yenu, wahimizeni Wananchi kujenga utamaduni wa kufanya usafi muda wote tusisubiri kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi ndo tufanye usafi...kwa kuwa sisi Tunduma ni Lango Kuu la SADC, mji wetu unapaswa kuwa safi muda wote kwani tunapokea wageni wengi na wengine wanapita tu na ndiyo maana tukaamua kila Jumamosi tunafanya zoezi kama hili." Anasema Garigo. Aidha, Msimamizi wa Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka, Pendo Shechambo ameikumbusha jamii kuend