Posts

Showing posts from December, 2021

RC SONGWE AMEFIKA NYUMBA MSIBANI KWA ASKOFU MWENISONGOLE

Image
 Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba akiwa ameongozana na Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Songwe wamefika Ichenjezya Mbozi Msibani kwa askofu Ranwell Mwenisongole ambapo amesaini kitabu cha Maombolezo. Aidha Mkuu wa Mkoa amesema maandalizi ya kuupokea mwili wa marehemu umekamilika na Ulimzi na Usalama umeimalishwa kuhakikisha shughuli za mazishi zinakwenda kwa Amani

BABA AUA MWANAE BAADA YA KUMSUMBUA AKIWA USINGIZINI

Image
Wapelelezi kutoka Idara ya Makosa ya Jinai (DCI) wamefichua kwamba wamemkamata mzee wa miaka 73, James Tarus, kwa kumuua mwanae. Kijana huyo ambaye alikuwa mlevi alielekea chumbani kwa baba yake na kujaribu kumuamsha kwa kunyanyua kitanda jambo ambalo lilimkasirisha sana mzee huyo. Babaake kwa hasira, alichukua kipande cha mbao akampiga na kumfunga kwa kamba shingoni na kisha kwenye kochi. “Mwathiriwa ambaye alikuwa amekunywa chupa kadhaa alielekea nyumbani kisha hadi chumbani mwa babake akaanza kumuamsha huku akinyanyua kitanda. Akiwa amewaka kwa hasira, mzee huyo alimpasua kichwa mwanawe kwa kutumia mbao iliyokuwa karibu, kabla ya kumfunga kwa kamba shingoni na kidha kwenye kochi,” DCI aliripoti. DCI ilisema chifu wa eneo hilo na wananchi walifika eneo la tukio na kumkuta kijana huyo akiwa amefungwa kwenye sofa na tayari akiwa amekata kamba. Alikuwa ameaga dunia kutokana na majeraha aliyopewa na babaake, ambaye alikamatwa mara moja  

BREAKING NEWS BASI LA MANDA'S LAPATA AJALI SONGWE

Image
Basi linalofanya safari zake Mbalizi(Mbeya)-Mkwajuni(Songwe) la Manda's Express limeangua njia panda ya Galula Wilayani Songwe. RPC Jannet Magomi amethibitisha na taarifa kamili itatolewa baadae,taarifa ya Mwanzo mtu mmoja amekwisha fariki na uokoaji unaendelea.

RAIS SAMIA ATEUA MWENYEKITI MPYA TUME YA UCHAGUZI

Image
 

ALIDHANIWA KUFARI AFUFUKA AOMBA UJI..WANANCHI WATAWANYIKA

Image
MKAZI wa Kijiji cha Msikisi wilayani Masasi, mkoani Mtwara, Ayuba Mawazo (26), aliyedaiwa kufariki dunia, na wananchi kufika nyumbani kwa shughuli za mazishi, amezinduka na kuomba apewe uji.

WACHIMBA VISIMA WAANZISHA HOTEL SONGWE RC AIFUNGUA

Image
  Mkuu wa Mkoa amezindua hotel ya Forest Hill hotel iliopo kata ya Mlowo Wilayani Mbozi inayomilikiwa na Vijana wawili David Tuya na Christopher Mponzi wanaojihusha na Uchimbaji wa Visima maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Songwe na nchi mzim ya Tanzania. Kabla ya Uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa Omary Mgumba alifanya Ukaguzi wa Ujenzi wa  Wawekezaji hao na kutembezwa maeneo mbalimbali ya hotel hiyo na kisha kusomewa risala aliyoandaliwa na mmoja wa Viongozi wa Hotel hiyo Frank Ngowi ambapo katika risala hiyo walimueleza Mgumba nia na madhumuni ya kujenga hoteli hiyo ikiwemo utoaji wa ajira ambapo mpaka sasa wameweza kuajiri wafanyakazi zaidi ya 20 na hivyo kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hasani ya kazi iendelee. Aidha katika risala hiyo pia walimueleza changamoto mbalimbali ikiwemo Umeme Mdogo unaosababisha Miundo mbinu yao ya Umeme kushindwa kufanya kazi kwa uhakika.Pia waliomuomba Mkuu wa Mkoa kuwasaidia Ujenzi wa Miundo mbinu ya Barabara k

DIWANI MLOWO AUPIGA MWINGI AFUNGA MWAKA KWA STAILI YAKE

Image
 Diwani wa kata ya Mlowo kata iliobeba Makao makuu ya Mkoa wa Songwe Mheshimiwa Jackson Mwanda amefunga mwaka kwa staili yake baada ya kufanya Mkutano mkubwa wa hadhara Kijiji cha Ivanga na kukusanya mamia ya Wananchi. Mkutano huo uliohudhuliwa na Viongozi wa Chama Wilaya wakiongozwa na Katibu Mwenezi Wilaya ya Mbozi Zawadi Shombe na kwa upande wa Viongozi wa Serikali akiongozwa Teo wa Mji wa Mlowo ambae pia ni Mwenyekiti wa TUGHE Taifa Joel Kaminyoge. Mhe Mwanda alianza kwa kuyaweka bayana yale Serikali ilichokifanya katika kata yake ikiwemo Ujenzi wa Madarasa,stendi ya Wilaya ambapo amesema mamilion ya pesa Serikali imetoa kwa kata Mlowo ili kukamilisha na kuanzia miradi mbalimbali. Wakati huo huo amekemea tabia ya baadhi ya watu kubeza mafanikio yanayofanywa na Serikali ikiwemo na kumbeza yeye mwenyewe na kudai watu wa aina hiyo wapuuze na ni urafi tu wa madaraka wa baadhi ya watu ndio unaowasasumbua. Kwa upande wa Wananchi  walimpongeza Diwani wao kwa kufanya Mkutano na kuwajibu ma

KUCHOMA MATAILI MARUFUKU SONGWE

Image
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kuwapima kilevi madereva wote wa vyombo vya moto katika kipindi iki cha sikukuku za Christmas na mwaka mpya ili keupuka ajali. Mkuu wa Mkoa ametoa agizo ilo wakati akitoa salamu za sikukuu za Christmas na mwaka mpya kwa wananchi wa Songwe akiwa Tunduma, 24 Desemba 2021. "Madereva wasiendeshe vyombo vya moto wakiwa wamelewa na kama umekunywa ni bora upaki gari pembeni usubiri pombe iishe"  Omary Mgumba. Mkuu wa Mkoa amewataka madereva wa vyombo vya moto kufuata sheria za Usalama Barabarani ili kuepuka ajali za Barabarani ambazo zinaweza kugharimu maisha ya watu. Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa amepiga marufuku kuchoma mataili na kulipua milipuko ambayo inaleta taharuki kwa sababu kuna watu hawawezi kuimiri pia ametahadhali kuchukua hatua za Ugonjwa wa UVIKO-19 pindi wawapo kwenye maeneo ya kumbi za starehe na maeneo mengine ya Mkusanyiko katika kipindi hiki cha Sikukuu. Aidha Mgumba awewatakia waka

SERIKALI KUMPA TUNZO MBUNGE NEEMA MANDABILA

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba amempongeza Mbunge wa Viti maalumu Mkoa Songwe Mhe Neema Mwandabila kwa kujitolea kuwahudumia Wafungwa Magerezani kwa kuwagawia magodoro na mablanketi katika Magereza mbalimbali Mkoani Songwe. "Sisi kama Serikali tumepanga kumpatia Tunzo Mheshimiwa Neema Mwandabila iwa kitendo chake cha kuwajali na kuwahudumia Wafungwa walioko Magerezani huu ni Moyo ya kipekee sana na wakishujaa"amesema Mgumba

WAKULIMA LIMENI MAZAO YANAYOSTAHIMILI UKAME RC RUKWA

Image
Wakulima wa mkoa wa Rukwa wameshauriwa kulima mazao yanayostahimili ukame kutokana na mwenendo wa unyeshaji mvua mwaka huu si wa kuridhisha. Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti ametoa ushauri huo (22.12.2021) mjini Sumbawanga wakati akizungumza kwenye kikao cha kusimamia, kuratibu na kudhibiti mapato na matumizi ya serikali robo ya pili kilichohudhuriwa na wakurugenzi wa halmashauri zote. “Mvua zimechelewa sana. Katika wilaya zetu tumeshuhudia kiwango kidogo cha mvua hadi sasa hivyo ni wakati muafaka wataalam wa kilimo wakaelimisha wakulima kupanda mazao yanayostahimili ukame “alisisitiza Mkirikiti. Mkirikiti aliongeza kusema tayari serikali imechukua hatua kadhaa ikiwemo kugawa mbegu za soya na alizeti ili wakulima wazalishe mazao hayo ambayo haihitaji mvua nyingi na kuwa jitihada zaidi zinatakiwa ikiwemo kutumia kilimo cha umwagiliaji katika mabonde yaliyopo ili kuwa na uhakika wa mazao ya chakula. Katika hatua nyingine Mkirikiti amewagiza wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo ku

RC SONGWE AANDIKIWA BARUA YA VITISHO

Image
Mwananchi asiyefahamika Wilayani Momba Kata ya Myunga amemuandikia barua Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omari Mgumba akituhumu baadhi ya Wanakijiji kujihusisha na matukio ya Uvunjanji Amani na Vitisho kwa Wananchi. Aidha barua hiyo iliwatuhumu baadhi ya Viongozi wa jeshi la Polisi Wilayani Momba,Diwani wa kata hiyo na Mtendaji wa kata kuwa wanajihusisha na rushwa na wamekuwa wakila njama na watuhumiwa. Mkuu wa Mkoa amefanya  mkutano wa hadhara katika kata hiyo ya Miyunga na Wananchi hao ambapo aliwaeleza kuwa amepokea barua ofisini kwake isiokuwa na jina la Mwandishi wa muhuli wa la saini ya Mwandishi. Sehemu ya barua hiyo inawataja ndugu wawili ambao Majina yao tunayahifadhi kuwa wamekuwa tishio Kijiji hapo na wanawatishia Wananchi wa kata ya Myunga na ikaeleza kuwa Mauaji wa aliekuwa Weo Mbozi Protus Siame waliomua walijulikana lakini walipofikishwa Polisi kesi iliishia kwa Mkuu wa Kituo Tunduma na ikadai barua hiyo kuwa Diwani na WEO wa Miyunga walipewa pesa na watuhumiwa wakaachiwa. Akijib

SONGWE GIRLS KUANZA RASMI JANUARI

Image
Na Baraka Mwashambwa Afisa Habari Songwe S hule ya Sekondari ya Wasichana ya Songwe iliyopo Kata ya Myunga Kuanza na wanafunzi wa kutwa kwanza ifikapo Januari 2022. Afisa Elimu Mkoa wa Songwe, Mwl. Juma Kaponda  amesema kwa miundombinu iliyopo sasa wataanza na wanafunzi wa kutwa kwanza ambao ni wasichana tu ambao watatoka jirani na Myunga wakati wakisubiria kupata fedha za ujenzi wa Mabweni na Nyumba za walimu ambazo atakaa mlezi na Mkuu wa Shule. Afisa Elimu amesema hadi kukamilika kwa Shule itakuwa ni kidato cha kwanza hadi sita. Mwezi Oktoba 2021 katika kikao cha maendeleo ya Elimu Mkoa kilichongozwa na Katibu Tawala Mkoa, Ndg. Missaile Musa kikao kiliazimia Halmashauri zote za Songwe kuchangia fedha kila moja Milioni 30 ili kufanikisha Shule ianze kuchukua wanafunzi ifikapo Januari 2022. Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amemuagiza Afisa Elimu Mkoa kukamilisha miundombinu mhimu ambayo itawezesha wanafunzi kuanza kusoma ifikapo Januari 2022. "Lengo la Serikali ni ifikap

VIONGOZI CCM MBARONI KWA KUMPIGA POLISI

Image
  KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Babati, Filbert Mdaki (52) na Katibu wa Jumuiya ya vijana UVCCM wa wilaya hiyo, George Sanka (46) wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga askari polisi mateke na fimbo.   Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Benjamin Kuzaga alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea kijiji cha Kirudiki wilayani Babati Desemba 16 saa 11 jioni.   Kamanda Kuzaga alisema watuhumiwa hao walimshambulia Koplo Baraka wa Kituo kidogo cha Polisi Kiru kwa kwa mateke na fimbobaada ya kufika kwenye mkusanyiko wa wananchi wa Kijiji cha Kirudiki.   “Askari huyo baada ya kuona mkusanyiko alifika ili aulizie juu ya kibali cha mkusanyiko huo, ndipo viongozi hao wakamshambulia maeneo mbalimbali ya mwili,” alisema kamanda Kuzaga.   Alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na ukikamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani. Kada wa CCM wa mjini Babati mkoani Manyara, Cosmas Masauda, ameeleza kusikitishwa kwa kitendo cha viongozi hao kukamatwa na kupelekwa mahabusu wak

MOMBA WAMKOSHA RC SONGWE UJENZI WA MADARASA YA COVID 19

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba amefanya ziara ya siku moja Wilayani Momba.Akiwa Momba Mgumba amefanya Ukaguzi wa Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa Shule ya Sekondari Nkangamo yenye Jumla ya Wanafunzi 337 ambapo Kati ya hao wavulana ni 151 na wasichana ni 186.Shule hiyo ilioanzishwa mwaka 2009 ina jumla ya Waalimu 19 ikiwa 12 ni wakiume na 7 wakike. Awali Makamu Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Julither Awe alimueleza Mkuu wa Mkoa kuwa Shule hiyo tarehe 20.10.2021 ilipokea jumla ya fedha Milioni 60 kutoka  Hazina kama fedha za kupambana Uviko 19 kwa ajili ya Ujenzi wa Vyumba 3 vya Madarasa ambapo wamefanikiwa kujenga Vyumba 3 na ofisi moja ya Waalimu ambavyo vyote kwa pamoja vimeshakamilika. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Momba Regina Bieda amesema Ujenzi wa Vyumba hivyo na ofisi katika Shule hiyo umekamilika kwa asilimia 100 na kuwashukuru Wananchi wa Nkangamo pamoja na Diwani wao kwa ushirikiano waliouonyesha mwanzo mpaka mwisho wa Zoezi zima la Ujenzi. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Song

HABARI KUBWA MAGAZETI YA LEO

Image