ZAHANATI ILIOJENGWA KWA MAMILIONI MBOZI YADAIWA KUTELEKEZWA,
Wananchi wa Kijiji cha Isowenzya kilichopo kata ya Isansa wamedai kukosa huduma za kiafya baada ya Zahanati iliyopo Kijijini hapo kutotowa huduma Kwa muda mrefu hali iliopelekea Zahanati hiyo kufungwa muda mrefu. Wananchi hao wameishukuru Serikali Kwa kuwajengea Zahanati hiyo yenye hadhi kubwa lakini huduma kwao zimekuwa hazipatikani hivyo wanaiomba Serikali kuwasaidia kwani wanapata tabu kutokana na kukosekana huduma ya matibabu kituoni hapo. Moja ya Majirani waliokizunguka kituo hicho wamedai kuna mtoa huduma mmoja tu na Serikali imemjengea mpaka nyumba lakini vyote vimetelekezwa na hawaoni dalili ya wao kupatiwa wataalamu wa afya. "Kama mnavyoona Zahanati hii imetelekezwa mtoa huduma inaweza hata kufika miezi mitatu hajafika kutoa huduma na hatujui anaishi wapi wakati nyumba ya mamilioni kajengewa hapa lakini hayupo"alilalamika Mwananchi wa Isowenzya alifahamika kwa jina moja Mama Ima Aidha kituo hiki cha habari kimemtafuta Mganga wa Wilaya Mbozi Mponjoli Mwangosi ambapo