Posts

Showing posts from September, 2022

MTENDAJI WA KIJIJI MBARONI KWA MAUAJI

Image
Jeshi la Polisi mkoani hapa linamshikilia Mtendaji wa Kijiji cha Sangambi Wilaya ya Chunya Joseph Nangale (45) kwa tuhuma za mauaji ya Aron Mbuba (18). Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo lilitokea Septemba 17 mwaka huu baada ya marehemu kupigwa na kitu butu kichwani. "Siku hiyo Nangale akiwa ameongozana na askari mgambo wawili wa kijiji walimkamata Mbuba wakati wakiwa kwenye msako wa wauza mkaa bila kulipa ushuru wa kijiji. "Wakati wanamkamata aliwajibu “hana hela” ndipo mtendaji wa kijiji na Askari Mgambo walimpiga sehemu mbalimbali za mwili na baadae kumuweka mahabusu ya kijiji hadi Septemba 19 baada ya kudhaminiwa." Hata hivyo kutokana na kuwa na maumivu makali, Mbuba alienda kupatiwa matibabu katika Zahanati ya kijiji hicho lakini siku iliyofuata (Septemba 20) alifariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata kwa kupigwa. ADVERTISEMENT Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka watuhumiwa wengine (Mgambo) ambao walikimbia mara baada

WATUMISHI 5 HALMASHAURI WASIMAMISHWA

Image
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa amewasimamisha kazi maofisa watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara kwa kusababishia hasara na matumizi mabaya ya madaraka. Waliosimamishwa kazi ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi, Juma Mavumo, aliyekuwa Kaimu mweka hazina Ramadhan Mwakamyanda, Mweka Hazina wa sasa Respicius Kagaruki na Mkuu wa Kitengo cha Tehama Nyanda Msirikale. Bashungwa amesema watumishi hao wamesimishwa kulingana na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2020/21. Pia Mhasibu wa Mapato, David Assey amesimishwa kazi kutokana na kukopa fedha Sh6.7 milioni kwa ajili ya matumizi ya ofisi na kuzipeleka kwenye akaunti binafsi. Bashungwa ameyasema hayo leo Jumatano Septemba 28, 2022 baada ya ziara ya siku mbili mkoani Manyara. Amesema taarifa ya ukaguzi wa kawaida kwa mwaka wa fedha wa 2020/21 iliagiza Mvumo achukuliwe hatua stahiki kwa kushindwa kuandaa vyema masharti

SONGWE KILIMO CHA MBOGAMBOGA, MATUNDA CHAHIMIZWA SHULENI

Image
Na Baraka Messa, Songwe. KIKAO Cha  Kamati ya lishe Mkoa wa Songwe, kimeazimia  Shule zote za  Msingi na Sekondari kuanza kupanda Bustani za mbogamboga na matunda Ili kuimalisha lishe kwa watoto. Kamati ya Mkoa imetoa pendekezo hilo  wakati wa kikao cha robo cha lishe  kupitia utekelezaji wa Afua za lishe kilichofanyika juzi katika Ukumbi wa Mkoa wa Songwe. Mjumbe wa Kamati hiyo Charles Chenza alishauri kamati kuweka azimio la kuitaka kila shule ipande miti ya matunda kama maparachichi, maembe kulingana na hali ya hewa ya eneo la shule ilipo,   pamoja na Bustani ya mbogamboga kwa ajili ya lishe kwa wanafunzi.  Naye mwakilishi wa Kamati ya Amani Mch. Rogers Simkonda amesema jamii imekuwa ikipuuza suala la kulima mazao na bustani majumbani mwao na hata kwenye taasisi kama mashule na kuacha maeneo wazi. "Kwenye taasisi zetu kama mashule hakuna jitihada za kuzalisha chakula kwa ajili ya chakula cha  mchana lakini hayo hayafanyiki na hata  mazao kama migomba iliyopandwa kwenye maeneo h

MAUAJI YA BODABODA WANNE MBARONI SONGWE

Image
  W ATU wanne wamekamatwa na jeshi la polisi mkoa wa Songwe kufuatia mauaji ya kijana Sadick Mwashambwa aliyechinjwa na watu watatu wasio julikana mbele ya mke wake akiwa na mtoto mchanga.   Kamanda wa polis Mkoa wa Songwe ACP Alex Mukama amethibitisha kukamatwa kwa watu hao wanne ambao hawakuwataja majina kutoka na na uchunguzi kuendelea kutokana na tukio hilo ambalo lilitokea septemba 24 mwaka huu majira ya saa satano za usiku.   “Jeshi la polis mkoa wa Songwe linafanya uchunguzi wa tukio la mauaji ambalo lilitokea septemba 24, usiku katika kitongoji cha Kamficheni Kata ya Hasamba Wilaya ya Mbozi , ni kwamba Kijana Sadick Simiton Mwashambwa miaka 24 mnyiha  aliuawa na kushambuliwa na siraha yenye makali sehemu mbalimbali za mwili wake na kuchinjwa shingoni,   Watu wanne wamekamatwa tunawashikilia na  uchunguzi zaidi zaidi unaendelea “ alisema kamanda Mukama   Akizungumza na waandishi wa habari juzi, mwenyekiti wa kitongoji cha Kamficheni Justin Ngondo ambaye naye inadaiwa kuwa anashi

ALIEMZUSHIA KIFO MWAKYEMBE AKAMATWA

Image
  JESHI la Polisi   K anda Maalum ya Dar es salaam ,   linamewakamata watuhumiwa wawili  kwa makosa ya kimtandao kufuatia msako mkali unaoendelea unaofanywa na Jeshi la  Polisi   kwa   kush irikiana   na   kikosi   kazi   m aalum   cha   kupambana   na   makosa   ya k imtandao. Mtuhumiwa wa kwanza ni I nnocent Adam Chengula, Mhehe, 23, mkazi wa Kigogo  Luanga,   amekamatwa kwa tuhuma za kujinasabisha kuwa yeye ni Dkt. HASSAN  ABBAS Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni San aa na Michezo, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia mtandao na kutumia laini za simu zenye usajili usio na  majina yake. Mtuhumiwa huyu amekuwa akiweka picha na majina ya   Dkt. Hassan Abbas   katika  maelezo ya ukurasa wake mitandaoni ya kijamii (Profile) na kutuma jumbe kwa watu  akiwaomba wamtumie fedha kwenye namba tofauti za simu.   Mfano Amekuwa akituma  jumbe   zinazosomeka   “ kaka   naomba   niazime   3mil   alhamis   nitakurudishia ”   na nyingine “ kaka nin a mtoto wangu naomba umpatie kazi apo kwako

PADRI APANDISHWA KIZIMBANI KWA UDHALILISHAJI WATOTO

Image
  Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi, Sostenes Soka amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro kwa tuhuma za udhalilishaji wa kingono kwa watoto. Kiongozi huyo wa kiroho , amepandishwa leo Jumatatu, Septemba 26, 2022 kusomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Salome Mshasha. Hata hivyo, waandishi wa habari wamezuiwa kuingia katika chumba cha mahakama kwa kile kilichoelezwa ni aina ya kesi inayomkabili padri huyo. Hakimu huyo amewaeleza waandishi wa habari kuwa atazungumza nao baadaye.

BODA BODA ACHINJWA MBELE YA MKEWE SONGWE

Image
 MAUAJI ya kutisha yametokea katika kitongoji cha Kamficheni kata ya Hasamba, Wilayani Mbozi, baada ya watu wasiojulikana kudaiwa kumuua Sadick Mwashambwa (24) dereva wa Bodaboda kwa kumchinja mbele ya mke wake akiwa na mtoto mchanga. Tukio hilo linadaiwa kutokea Septemba 24 mwaka huu, majira ya saa 11:20 usiku baada ya watu wawili wote wanaume kufika nyumbani kwa marehemu kisha kuvunja mlango na kuingia hadi chumbani ambapo walimkuta marehemu akiwa amelala na mkewe na mtoto wao mchanga na kisha kumkamata na kumchinja mbele ya mkewe na mtoto wao mchanga. Wakizungumza na waandishi wa habari, Mtendaji wa kata ya Hasamba, Imma Sichinga na mwenyekiti wa kitongoji cha Kamficheni Justin Ngondo walithibitisha kutokea kwa tukio hilo. Mwenyekiti wa kitongoji Ngondo alisema siku ya tukio alipata taarifa kutoka kwa jirani wa marehemu na baada ya hapo aliwafahamisha wajumbe wa serikali ya kijiji ambao kwa pamoja walifika eneo la tukio na kujionea unyama uliofanyika. “Mke wa marehemu ambaye kwa wak

MBATIA APIGWA STOP KUONGEA NA WAANDISHI WA HABARI

Image
  Mgogoro wa NCCR Mageuzi umeibuka kwa sura tofauti baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia kuzuiwa kufanya mkutano wake na waandishi wa habari. Jana Jumamosi, mkutano mkuu wa dharura wa Kamati Kuu ya NCCR Mageuzi uliofanyika jijini Dodoma, uliazimia kumvua uenyekiti na uanachama Mbatia na wenzake. Kuvuliwa kwake uanachama kulianza na kusimamishwa kufanya shughuli zote za chama hicho, uamuzi uliofanywa Mei 21, 2022 na Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi. Katika hali ya kujibu uamuzi wa jana wa chama hicho, Mbatia aliitisha mkutano na waandishi wa Habari katika Hoteli ya Regency Park, Mikocheni jijini Dar es Salaam, leo Jumapili, Septemba 25,2022 kabla ya kuzuiwa kufanya hivyo. Alipofika hotelini hapo saa 7:07 mchana, mmoja wa maofisa wa hoteli hiyo alimwambia amepokea maelekezo ya kusitisha mkutano huo, hivyo haruhusiwi kufanya tena. Mbatia aliomba taarifa hiyo kwa maandishi na baada ya kupewa,waandishi wa habari walitakiwa kutopanda ghorofa ya nane, mahali palipopangwa

DC GODIGODI AAGIZA MMILIKI WA SHULE KUKAMATWA BAADA YA KUMPELEKA MWANAFUNZI WA KIKE POLISI KWA KUSHINDWA KULIPA ADA

Image
  Mkuu wa Wilaya ya Kilombero mkoani  Morogoro, Hanji Godigodi ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata mmiliki wa shule ya sekondari Kaozya Mlimba kwa madai ya kumpeleka kituo cha polisi mwanafunzi wa kidato cha nne baada ya mzazi wa mwanafunzi huyo kushindwa kulipa ada ya muhula wa pili wa masomo. Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumamosi Septemba 24, 2022, Hanji amemtaja  mmiliki wa shule hiyo kuwa ni, Erick Kaozya na kubainisha kwamba Serikali imetoa miongozi mbalimbali ya elimu kwa shule za msingi na sekondari juu ya uendeshaji wa shule hizo. “Kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu na maelekezo ya serikali, mwanafunzi haruhusiwi kurudishwa nyumbani au kufukuzwa shule kwa sababu mzazi kukosa ada hasa kwa madarasa ya mitihani ya darasa la nne na  la saba lakini hata kidato cha pili, nne na kidato cha sita,” amesema Hanji Hata hivyo, mkurugenzi wa shule hiyo, Erick Kaozya amesema si yeye aliyempeleka mwanafunzi huyo polisi bali ni kaka wa mwanafunzi ndiye aliyemwambia aende polisi

MWANAMKE AFIA GUEST

Image
  Mkazi mmoja wa wilayani Handeni mkoani Tanga Mariam Mbwana (35) amekutwa amefariki katika nyumba ya kulala wageni huku mwanaume aliyekuwa naye akitorokea kusikojulikana. Akielezea tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia leo Jumamosi Septemba 24, 2022 meneja wa nyumba ya kulala wageni Paradise, Christian Masawe amesema alifika mwanaume ambae hakutambulika na kulipia chumba hicho. Amesema kuwa mteja huyo wa kiume kabla ya kuingia kulala alipata huduma ya chakula na vinywaji na alikuwa peke yake na wala hawakufahamu kuwa alikuwa na mwenzake. Ameongeza kuwa asubuhi wakati mfanyakazi anakwenda kukagua chumba kwaajili ya kufanya usafi, ndio akagundua upo mwili wa mwanamke amefariki dunia na kutoa taarifa kwa uongozi.  "Aliyekuja kuchukua chumba ni mwanaume na alikuja peke yake yule mwanamke haijulikani aliingia saa ngapi majira ya usiku, ila mwanaume huyo alikula na kunywa akiwa peke yake na inaonekana alitoka asubuhi na kumuacha ndani",amesema Massawe. Mdogo wake marehemu Maimun

MBATIA AFUKUZWA NCCR-MAGEUZI

Image
  Mkutano mkuu wa Chama cha NCCR Mageuzi umemtimua uanachama aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Taifa, James Mbatia na kumvua uongozi Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Angelina Rutairwa. Aidha, mkutano huo ulitaka viongozi wote waliohusika na ubadhilifu wa mali akiwemo Mbatia kuchukuliwa hatua za kisheria. Mkutano huo unafanyika leo Jumamosi Septemba 24, 2022 jijini Dodoma na kuhudhuriwa na wajumbe 224 kati ya 368 waliopo kwa mujibu wa Katiba ya chama chao. Wajumbe hao walifanya hivyo baada ya Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho, Haji Ambari Hassan kutaja tuhuma saba zinazomkabili Mbatia na tuhuma mbili za Angelina. Miongoni mwa tuhuma hizo  Mbatia ni kuuza mali za chama, ikiwemo mashamba na nyumba katika maeneo mbalimbali. Hata hivyo, amesema kuwa hakujibu mshtaka hayo na wala hakufika katika mkutano huo  licha ya kualikwa ili aweze kujitetea mbele ya wajumbe. "Tumewaita katika mkutano huu lakini hawakutaka kuja na badala yake walikimbilia mahakamani kuzuia kwa mara nyingine mkutano

MWALIMU AFUNGWA KIFUNGO CHA MAISHA MARA 2 NA MIAKA 30 JUU KWA KULAWITI

Image
  Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma mkoani Mara, imemuhukumu kifungo cha maisha jela mwalimu Idrisa Athumani (29) wa shule ya Msingi Kyawazaru iliyopo wilayani Butiama baada ya kukutwa na hatia ya kumlawiti mwanafunzi wake (14). Hukumu hiyo iliyotolewa leo Ijumaa Septemba 23, 2022 ni ya tatu kutolewa dhidi ya mwalimu huyo ambapo hukumu ya kwanza ilitolewa Septemba 14, mwaka huu na Mahakama ya Wilaya ya Musoma mwalimu huyo alihukumiwa kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mara mbili mwanafunzi wake mwingine. Hukumu ya pili ilitolewa Septemba 16, 2022 na Mahakama hiyo hiyo ya kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mwanafunzi wake mwingine (12). Hukumu ya tatu imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Stanley Mwakihaba baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo dhidi ya mashataka yaliyokuwa yakimkabili mwalimu Athumani. Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mwakihaba amesema mwalimu huyo amefanya kosa hi

Hii HAPA TOP 3 YA WABUNGE WACHAPA KAZI MKOA WA SONGWE

Image
  Mkoa wa Songwe ni  miongoni mwa Mikoa ya mwisho kuanzishwa miaka ya hivi Karibuni Nchini Tanzania.Ikumbukwe Mkoa huu maarufu kama Lango la SADC ni Mkoa unaonekana kukua zaidi kiuchumi na Wananchi wake wanaonekana kujituma zaidi katika kujikuzia kipato chao. Leo katika jamvi letu tumekuletea orodha na tathmini ndogo ya kituo hiki upande wa wabunge waliopo Mkoani humo. Tuliamua kumuuliza Mwananchi mmoja mmoja na kuangalia utendaji wa Wabunge kwa Wananchi na umaarufu wao katika mitandao ya Kijamii katika mahojiano yetu Mbunge toka Wilaya mpya ya Songwe Mhe Philipo Mlugo  anashika namba moja kwa kutajwa kama Mbunge ambae amekuwa jirani na Wananchi wake katika shughuli za kimaendeleo na muda mwingi hutumia Jimbo mwake na hata Shughuli nyingi za Kiserikali na chama Mhe Mlugo amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kila kitu kina kwenda sawa. Pia baadhi pia ya Wananchi wameizungumzia Mlugo kama Mbunge mwepesi kuwasaidia na kiufupi hana mkono wa birika. Nafasi ya pili wamempa Mbunge wa Jimbo la

AFARIKI KWA AJALI AKIMFUKUZIA MUMEWE ALIEBEBA MCHEPUKO KWENYE GARI

Image
  MWANAMKE mmoja kutoka nchini Nigeria amefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari wakati akimfukuzia mumewe aliyekuwa na mwanamke mwingine kwenye gari hilo. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na shuhuda wa tukio hilo, mwanamke huyo alimuona mume wake huyo akitoka kwenye saluni ya kike na mwanamke huyo anayedaiwa kuwa ni mchepuko wa mwanaume huyo ambapo mara baada ya kuwaona, mwanamkehuyo alikimbia na kuingia kwenye gari lake na kisha kuliondoa kwa kasi akiwa na lengo la kuwahi ili akasimame mbele yao na kuwazuia kupita, jambo ambalo halikufanikiwa na hivyo kujikuta akipata ajali mbaya. Ajali iliyopelekea kifo Cha Mwanamke huyo Mara baada ya ajali hiyo kutokea, mwanaume huyo alisimamisha gari lake na kisha kumshusha mwanamke aliyekuwa naye na baada ya hapo ndipo alikwenda kumsaidia mke wake ambaye alikimbizwa hospitali baada ya kuokolewa, mwanamke huyo alipoteza maisha baadaye akiwa hospitalini akipatiwa matibabu Zaidi kufuatia ajali aliyoipata.

RC MGUMBA TUMEMKAMATA KIGOGO WA POLISI KWA KUTOROSHA WATUHUMIWA

Image
  Ofisa upelelezi wa Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, anashikiliwa na Polisi kwa madai ya kuwaachia huru watuhumiwa wa uhujumu uchumi. Watuhumiwa hao wanadaiwa kukamatwa na mali za magendo zenye thamani ya zaidi ya Sh1.2 bilioni. Hayo yalisemwa juzi na Mkuu wa Mkoa Tanga, Omary Mgumba alipokuwa akitoa taarifa ya ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Serikali na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kuhusu hatua zilizochukuliwa kwa watuhumiwa 24 waliokamatwa na magendo ya vitenge. Mgumba alisema alishangazwa na hatua hiyo na alipofanya kikao na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, ndipo alibaini aliyewaachia huru watuhumiwa ni ofisa upelelezi wa Wilaya Mkinga aliyedai kupokea maelekezo kutoka kwa ofisa upelelezi wa mkoa (bila kutaja majina). Alisema tayari ofisa huyo amekamatwa na yuko mahabusu uchunguzi unaendelea na ukikamilika hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. “Nimshukuru Kamanda wa Polisi Mkoa Tanga, baada ya kuona yametokea makosa haraka alichukua hatua

MAGAZETI YA LEO

Image