Posts

Showing posts from March, 2023

ILEJE YAWANOA WAFANYABIASHARA MFUMO MPYA WA TAUSI

Image
Wafanyabiashara wilayani Ileje mkoani Songwe watakiwa kutumia mfumo mpya wa TAUSI kulipia mapato Ili kuondoa ufujaji na upotevu wa fedha. Wito huo umetolewa Machi 29,2023 na mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Farida Mgomi wakati akizungumza na wafanyabiashara hao katika kikao Cha Baraza la biashara la Wilaya ambacho pamoja na agenda zingine, kulikuwa na lengo la kutoa elimu kwa wafanyabishara juu ya matumizi ya Mfumo mpya wa TAUSI. Mgomi amesema mfumo huo ni rafiki kama alivyo ndege Tausi ambapo kwa namna moja au nyingine utaweza kusaidia  kutatua chanagamoto za  ukusanyaji wa mapato sambamba na kupunguza hoja za Mkaguzi wa nje wa Hesabu za Serikali. Hata hivyo Mgomi ameitaka halmashauri kuwa tayari kuacha kutumia mfumo ule wa zamani wa LGRCIS na kuingia kwenye mfumo mpya wa TAUSI "Hakikisheni mnasajili pos zote kwenye mfumo mpya wa Tausi  na makusanyo ya fedha zote zinapelekwe benki", amesema Mgomi. Mgomi amesema serikali imekuwa ikiboresha mazingira rafiki kwa wafanyabiashara hivyo u

MADEREVA NEW FORCE NA SAULI WAKAMATWA KWA KUFUKUZANA, DEREVA SUPER FEO ALA NDUKI KUKWEPA POLISI

Image
  Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoani Iringa, Moss Ndozero baada ya kuwanasa madereva wa mabasi ya Saulu,Super Feo na New Force wakifukuzana Muktasari: Mtindo wa madereva kupeana ishara ya eneo lenye askari na hivyo kupunguza mwendo umewaponza madereva wa mabasi ya Sauli, Super Feo na New Force baada ya kuwekewa mtego. Iringa. Madereva wa mabasi ya Sauli, Super Feo na New Force wamekamatwa kwa tuhuma za kuendesha mwendo wa kasi, huku wakikimbizana baada ya Mkuu wa Usalama Barabarani (RTO) mkoani Iringa, Mosi Ndozero kuwawekea mtego. Awali, Ndozero alipata taarifa za mwendo wa kasi wa mabasi hayo, hivyo akaamua kuweka mtego uliosababisha wakamatwe licha ya madereva waliokuwa wanapishana nao kuwaambia, eneo hilo hakuna askari.  Kwa sababu hawakubaini mtego huo, ishara kutoka kwa madereva wenzao zilionyesha mbele yao hakuna askari. Akizungumza baada ya kuyakamata mabasi hayo jana Machi 29, 2023, katika Mji wa Mafinga, wilayani Mufindi, Ndozero amesema awali alipokea taarifa kwamba mabasi ha

MBOZI NA MOMBA ZAPATA HATI SAFI RIPOTI YA CAG

Image
Halmashauri za Mbozi na Momba zilizopo Mkoani Songwe ni miongoni mwa halmashauri zilipopata hati safi huku Halmashauri ya Songwe ikiwa ni halmashauri pekee iliopata hata yenye mashaka kulingana na ripoti ya CAG. Rais wa Dkt Samia Hassan amewataka Viongozi na Watendaji wa serikali kuzisoma na kuzielewa vyema taarifa za rushwa na za ukaguzi wa hesabu za serikali ili ziwasaidie kujitathimini. Kwa mujibu wa taarifa ya CAG Halmashauri  za Mbozi,Momba, Tunduma na Ileje zimefanikiwa kupata hati safi huku Halmashauri ya Songwe ikiambulia hati yenye mashaka na kuwa ni halmashauri moja tu katika Mkoa wa Songwe yenye hati yenye mashaka. Wakiongea kwa nyakati tofauti juu ya mapokeo ya hati hizo baadhi ya wakurugenzi wamewashukuru Madiwani na Watumishi wa halmashauri zao pamoja na Wananchi. "Kiukweli sisi Mbozi tumefarijika sana kwa hii hati tuliopata na kwa upande wangu binafsi hii ni hati yangu ya kwanza kupata toka nimeletwa kuwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Mbozi lakini hizi sio juhudi zan

DC AKAGUA VIFAA TIBA HOSPITALI YA WILAYA YA SONGWE

Image
Mkuu wa Wilaya ya Songwe Mhe. Solomon Itunda ameiongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Abdallah Mgonja kukagua vifaa tiba vya kisasa vinavyoendelea kuletwa katika Hospitali ya Wilaya ya Songwe. Kufuatia ukaguzi huo, Mhe. Itunda amempongeza Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan  Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Wilaya ya Songwe shilingi bilioni 3.5 za ujenzi wa Hospitali hiyo pamoja na vifaa vya kisasa vyenye thamani ya Tsh milioni 247. Mkuu wa Wilaya huyo ameielekeza Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha wanatunza vifaa na majengo hayo, sambamba na kutoa huduma kwa wananchi kwa kuzingatia utu na miiko ya kazi yao.

AFUNGWA MAISHA AKIPINGA KIFUNGO CHA MIAKA 30

Image
 Rufaa ya pili aliyokata mkazi wa Kijiji cha Mwanambaya, Wilaya ya Mkuranga, Denis Joseph, kupinga kifungo cha miaka 30 kwa kosa la kumbaka na kumlawiti mwanafunzi imegeuka msiba baada ya kujikuta akiambulia kifungo cha maisha. Mahakama ya Rufani imekubaliana na Wakili wa Serikali, Elizabeth Olomi kuwa adhabu ya kifungo cha miaka 30 alichopewa Joseph, maarufu kama Saa Moja kwa shitaka la ulawiti ilikuwa kinyume na sheria. Wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo, Olomi aliikumbusha Mahakama kuwa kifungo alichopewa Joseph kilikuwa kinyume na kifungu cha 154 (2) cha Kanuni ya Adhabu kinachotoa adhabu ya kifungo cha maisha kwa mtu yeyote anayetiwa hatiani kwa kulawiti mtoto cha umri wa chini ya miaka 18.  wanaotuhumiwa kulawiti, kumrekodi aliyelawitiwa “Katika kesi iliyo mbele yetu, kwa kuwa mwathirika wa kosa hilo alikuwa na umri wa miaka 10 siku ya tukio, kifungo sahihi kilitakiwa kiwe kama kilivyotamkwa na sheria. “Kwa hiyo, tunatumia mamlaka tuliyopewa kuweka kando kifungo cha miaka 30 na

MALAWI WARIDHISHWA NA USHIRIKISHWAJI WA JAMII KATIKA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI ILEJE

Image
Timu ya utekelezaji wa Mradi wa Bonde la Mto Songwe kutoka Wilaya ya Chitipa-Malawi imepongeza namna wananchi wanavyoshirikishwa katika mradi huo upande wa Tanzania katika wilaya ya Ileje. Pongezi hizo zimetolewa na watalaam hao wakiongozwa na Mkuu wa msafara Mhe.MaCMillan Magomero ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Chitipa wakati wa majumuisho katika Kata ya Malangali-Ileje. Mhe.Magomero amesema kuwa maelezo waliyoyapata toka kwa wananchi tangu mwanzo katika vijiji vya Ilondo,Bulanga na Malangali yanakidhi maelezo ya mezani waliyokuwa wameyapata siku ya mwanzo katika kikao kwenye Ukumbi wa VIM. Naye Franklin Mwalwanda Ofisa mmoja wa wageni hao ameeleza kufurahishwa kwake na namna  wanawake wanavyoshikishwa katika  mradi huo akisema kuwa kwa kufanya hivyo ni utekelezaji wa agenda ya kimataifa ya kuwawezesha wanawake. Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mhe.Farida Mgomi ameshukuru viongozi wa juu wa mataifa haya mawili kwa kuruhusu ushirikiano huo kuwepo akisisitiza kuwa atasimamia na kuhakikisha mahusian

BARABARA KM 5 MBIONI KUANZA KUJENGWA LANDANI-KIWIRA ILEJE.

Image
MKANDARASI aliyepewa kazi ya kujenga barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Kilomita 5 kwa gharama ya shilingi bilioni 5.7 ya Kiwira-Landani wilayani Ileje mkoani Songwe atakakiwa kumaliza mradi huo ndani ya mwaka mmoja kama mkataba unavyolekeza. Akimkabidhi mkandarasi atakayetekeleza mradi huo Machi 21,2023 kutoka Kampuni ya IRA GENERAL ENTERPRISES COMPANY LIMITED mkuu wa wilaya hiyo Farida Mgomi amemtaka mkandarasi huyo kufanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa. Mgomi amesema tayari serikali imemlipa mkandarasi huyo asilimia 15 ya fedha ili kumwezesha kuanza kazi bila kisingizio cha kukosa fedha na matarajio ni kutaka adha ya mzunguko wa kilomita 38 upungue na kuanza kutumia barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 5. “Kukamilika kwa barabara hiyo kutaongeza pato la halmasahuri na Taifa kwani uzalishaji utaongezeka mara dufu, na wawekezaji wataongezeka”, amesema Mgomi.. Meneja wa TARURA Mkoa wa Songwe Mhandisi  Kilian Daudi Haule amesema maagizo yaliyotolewa ya kuwasimaia wakandarasi

BARABARA YA ISOKO-KATENGELE KUJENGWA KWA ZEGE

Image
Kutokana na Barabara ya Isoko-Katengele kuwa na miinuko mikali pamoja na kona kali zipatazo 62, Wakala wa Barabara za vijijini na mjini (TARURA) imeanza kujenga Barabara hiyo kwa kutumia zege kwa sehemu zote ambazo zina kona kali na miinuko ili kurahisisha mawasiliano kwa watumiaji wa Barabara haswa wakazi wa Kata ya Kafule, Sange, Ibaba, Ngulugulu na lubanda ambao wamekuwa wakipata adha kipindi cha mvua kwenda katika Hospitali kongwe ya Isoko ambayo imejengwa enzi za ukoloni 1889 pamoja na kusafirisha mazao yao.   Meneja wa TARURA Wilaya ya Ileje, Mhandisi Lugano Mwambingu amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamilia  kwa dhati kuwaondolea changamoto ya mawasiliano wananchi wanaotumia Barabara kwa kutoa fedha za matengenezo milioni 649, 882,000. Mhandisi Mwambingu amesema kazi nyingine zinazofanyika ni pamoja na kukata magema ya Barabara kwa ajili ya utanuzi wa Barabara, kujenga gabion na kuumba tuta kazi zote zinaendelea. "Kwa kuzingatia u

MWALIMU ADAIWA KUMUUA MWENZIE DARASANI

Image
  Mwalimu wa Shule ya Msingi Igaka, Samwel Subi anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Geita kwa tuhuma za kumuua mwalimu mwezake Emanuel Chacha kwa kumchoma na kisu akiwa darasani. Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limetokea Machi 15 saa 3:45 asubuhi wakati walimu hao wakiandaa mtihani kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la kwanza. “Kata ya Isulwabutundwe mwanaume wa miaka 35 katika Shule ya Msingi Igaka aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kwenye chembe ya moyo na mwanaume mwingine mwenye miaka 35 ambae ni mwalimu mwenzake. Walimu wote wawili walikuwa darasani wakiandaa mtihani ndipo mtuhumiwa alitoa kisu na kumchoma mwenzake kwenye chembe cha moyo,” amesema Kamanda Jongo. Kamanda alisema chanzo cha tukio hilo inadaiwa kuwa ni ugomvi baina ya walimu hao ambao walikuwa wanagombea uongozi kwenye kitengo cha elimu ya kujitegemea. “Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea mwalimu amekamatwa na amekiri na sababu anadai aliona walimu

WATANO WAFARIKI UGONJWA USIOJULIKANA BUKOBA

Image
  Wizara ya Afya imetangaza kuzuka kwa ugonjwa wa usiojulikana katika vijiji viwili, wilayani Bukoba Vijijini mkoani Kagera nchini Tanzania ambapo watu watano wamefariki dunia huku wengine wawili wakiendelea na matibabu hospitalini. Dodoma. Watu watano kati ya saba waliougua ugonjwa usiojulikana katika Wilaya ya Bukoba Vijijini Mkoani Kagera wamefariki dunia. Taarifa iliyotolewa jana Alhamis Machi 16, 2023 na Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu amesema ugonjwa huo umetokea katika vijiji vya Bulinda na Butayaibega vilivyopo katika kata za Marua Kanyangereko wilayani humo. Profesa Nagu amesema watu hao walipata dalili za homa, kutapika, kutokwa na damu maeneo mbalimbali ya mwili na figo kushindwa kufanya kazi. “Wengine (watu) wawili wako hospitali wanaendelea matibabu. Mwenendo wa ugonjwa huo unaashiria uwezekano kuwa ni ugonjwa wa kuambukiza,” amesema Profesa Tumaini bila kusema ni ugonjwa gani. Amesema Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu kuhusu mwenendo wa ugonjwa huo n

DC ILEJE ASHIRIKI MAFUNZO YA UONGOZI KWA WAKUU WA WILAYA DODOMA.

Image
  Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mhe. Farida Mgomi katika picha akishiriki  mafunzo ya uongozi yaliyoanza leo Machi 13_18,2023 Kwa wakuu wa wilaya za Tanzania Bara wakiwa katika Ukumbi wa Mtumba Jijini Dodoma. Mafunzo hayo yamefunguliwa rasmi na makamu wa rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Philipo Mpango. Mafunzo ya wakuu wa wilaya yameandaliwa na ofisi ya Rais Taimisemi Kwa ajili ya kuwajengea uwezo wakuu wa wilaya.

DC ILEJE AWAAGIZA MAAFISA UGANI KUTOA ELIMU KWA WAKULIMA

Image
Baada ya kugawiwa pikipiki 29 Kwa maafisa Ugani wilayani Ileje mkoani Songwe mkuu wa wilaya hiyo Mhe.Farida Mgomi amewaagiza maafisa hao kuwatembelea wakulima mashambani kutoa elimu ya kilimo bora na si wakulima kuwafuata maofisini. Mhe.Mgomi ametoa maagizo hayo Machi, 11,2023 wakati akigawa pikipiki 29 Kwa maafisa ugani wanaohudumia kata 18 zenye vijiji 71 wilayani humo hafla ambayo imefanyika katika ofisi za halmashauri ya Ileje. Mhe.Mgomi amesema asilimia kubwa ya uchumi Kwa wananchi wa Ileje na mapato ya halmashauri hiyo hutokana na kilimo, hivyo pikipiki hizo zitumike kuwatembelea wakulima kubaini fursa na changamoto zinazowakabili Ili kuzipatia ufumbuzi. Mhe. Mgomi amesema Kila afisa ugani kwenye eneo lake ahakikishe anatambua fursa za mazao yanayostawi kwenye kata yake na kuweka mikakati namna ya kuwawezesha wakulima waongeze uzalishaji wa mazao hayo kibiashara ili kiwainue kiuchumi. "Pikipiki hizo hazijaja Kwa bahati mbaya bali zimekuja Kwa ajili ya kufikia 2030 kuongeza a

DC ILEJE AZIASA AMCOS KUJENGA UAMINIFU KWA WAKULIMA WA KAHAWA

Image
Wakati wilaya ya Ileje mkoani Songwe ikipambana kutengeneza mazingira rafiki Kwa wakulima wa mazao ya kimkakati ikiwepo Kahawa, Pareto, Iriki na mengine vyama vya ushirika vimeaswa kujenga uaminifu Kwa wakulima. Wito huo umetolewa Machi 8,2023  na mkuu wa wilaya hiyo Farida Mgomi wakati wa kikao Cha wadau wa kahawa kilichowakutanisha wakulima, viongozi wa Amcos na baadhi ya makampuni yanayonunuza zao la kahawa kikao kilichofanyika ukumbi wa halmashauri Ileje. Mgomi amesema viongozi wa AMCOS wanapaswa kusimamia maslahi ya wakulima wa Kahawa kuwapa fedha zao kwa wakati ili wakulima waongeze wigo wa kulima zao hilo. "Mazao yanunuliwe kupitia vyama vya ushirika Kwa mujibu wa Sheria na hairuhusiwi mtu yeyote kununua anavyotaka yeye kwa kuwarubuni wakulima na kuwadhulumu fedha zao", amesema Mgomi. Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Ileje Geodfrey Mnauye amesema ili kuongeza uzalishaji wa kahawa wazalishaji wa mbegu hiyo TACRI wanapaswa kuzalisha mbegu kwa wingi na yenye ubora ku

HIZI HAPA BARABARA ZILIZOPENDEKEZWA KUPANDISHWA HADHI MKOANI SONGWE

Image
 Kikao cha bodi ya barabara Mkoani Songwe kikiongozwa na Mwenyekiti ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe Francis Michael kilichofanyika jana 06 machi 2023 katika ukumbi mdogo Mkuu wa Mkoa wa Songwe kimependekeza na kupitisha mapendekezo ya  baadhi ya barabara kupandishwa hadhi na kuanza kuhudumiwa na Wakala wa barabara tanroads badala ya Tarura. Katika kikaoa hicho kilichohudhuliwa pia na Mbunge wa Ileje ambae pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi Godfrey Kasekenya Mwenyekiti wa CCM Mkoa Songwe Radwell Mwampashe, Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa taasisi na Wajumbe toka taasisi mbali mbali kwa pamoja walilidhia hoja ya kuzipandisha hadhi barabara 6 ambapo kabla ya kufunga hoja Mkuu wa Wilaya ya Songwe Solomoni Itanda aliomba barabara mbili toka Wilayani Songwe zipandishwe hadhi hiyo lakini kikao kiliazimia barabara moja ya Kininga-ngwala  ndio iingizwe kwenye mpango huo na nyingine iletwe kikao kijacho. Hizi hapa barabara zilizopitishwa Itumbula-Namkukwe-Galula(Momba-Songwe Galula-Itindi-Magamba( Songw

MAHAKAMA YAVUNJA NDOA YA KAFULILA

Image
  Miaka mitano tangu wanandoa waliobobea katika siasa David Kafulila na Jesca Kishoa kutengana, Kituo Jumuishi cha Mahakama kilichopo Mahakama ya Wilaya ya Temeke imetoa hukumu ya kuvunja rasmi ndoa hiyo tangu Februari 20 mwaka huu. Dar es Salaam.  Kituo Jumuishi Huduma za Kimahakama, Mirathi na Ndoa, Temeke kimeivunja rasmi ndoa kati ya wanasiasa machachari David Kafulila na Jesca Kishoa kupitia shauri la ndoa No 217 ya 2022. Ndoa hiyo iliyofungwa Aprili 22, 2014 ilivunjwa rasmi Februari 20, 2023 baada ya wanandoa hao kutengana tangu mwaka 2019 kabla Mahakama ione ndoa hiyo imevunjika kiasi cha kutorekebishika. Wakati hati ya madai ikionyesha kiini cha mgogoro huo ni ugomvi na utengano, Mahakama imevunja ndoa baina ya wawili hao huku ikitoa amri kwa mama kubaki na watoto na kila mzazi kuwa na wajibu wa kuchangia gharama za matunzo kwa asilimia 50. “Maombi ya Jesca Kishoa akiitaka Mahakama ione ndoa kati yake na David Kafulila imevunjika kiasi cha kutorekebishika na kuomba amri ya Maha