Posts

Showing posts from June, 2024

FAIDA ZA MAJANI YA MPERA

Image
1. Chai ya majani ya mpera inaponyesha kifua na kikohozi. 2. Majani ya mpera yaliyosagwa vizuri yanatumika kutibu muwasho uliotokana na mzio (allergy). 3. Pia majani haya ya mpera yakichemshwa kama chai yanaondoa cholesterol iliyozidi mwilini. 4. Chai ya majani ya mpera inapunguza kiwango cha tatizo la sukari mwilini. 5. Chai ya mpera ni dawa nzuri kwa wenye matatizo ya nguvu za kiume. 6. Pia inatumika kama scrub ya uso. Chukua majani ya mpera saga kisha tia maji kiasi na inasaidia kuondoa uchafu usoni. 7. Pia majani ya mpera yakichemshwa ni dawa ya kuponyesha tumbo la kuhara. 8. Kama umejikata kidogo unaweza kutumia majani ya mpera yalioshwa na kusagwa vizuri kwa kupunguza maumivu na kukulinda na maambukizi ya bakteria. 9. Majani ya mpera yaliyosagwa vizuri yanatumika kutibu eneo la mwili lililong'atwa na mdudu na kupunguza maumivu. 10. Chai ya majani ya mpera inaaminika kuwa ina uwezo wa kutibu tezi dume. 11. Kutokana na kuwa na vitamini C kwa wingi majani ya mpera yana uwezo mku

MBUNGE SICHALWE: TUWEKEWE GETI MPAKA WA MOMBA-ZAMBIA, TUONGEZE VYANZO VYA MAPATO

Image
Mbunge wa Jimbo la Momba Mhe Condester Sichalwe (Mundy) akiwa Bungeni Jijini Dodoma kwa mara nyingine ameiomba Serikali kufanya juu chini kufungua geti la pili katika mpaka wa Tanzania na Zambia eneo la kijiji cha Chipumpu Halmashauri ya Momba ili kupunguza mianya ya uigizwaji na utoroshaji wa bidhaa mbalimbali kupitia maeneo hayo na kuikosesha Serikali Mapato. Mhe. Sichalwe amesema tangu mwaka 2021 amekuwa akisimama mara kdhaa Bungeni hapo na kutoa wazo la kuongeza geti eneo hilo, badala ya kutegemea mpaka wa Tunduma Pekee kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kuongeza vyanzo vya mapato na kupunguza mianya ya uingizwaji na utoroshaji wa bidhaa kinyemela. “Swali langu ni kwamba je nilini Serikali itaboresha mpaka kati ya Zambia na Tanzania ili kudhibiti njia za panya ambazo mazao na bidhaa nyingine hutoroshwa bila kulipiwa kodi” Mhe.Sichalwe Naibu waziri wa Fedha Mhe.Hamad Hassan Chande akijibu swali hilo amesema kuwa katika kudhibiti utoroshaji wa bidhaa na mazao katika mpaka wa Tanzania

UPATIKANAJI WA MAJI KIBAHA ASILIMIA 78

Image
HALI ya upatikanaji wa maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kwa sasa ni asilimia 78 huku malengo yakiwa kufika asilimia 85 ifikapo Disemba, 2025. Kiwango hicho kimefikiwa kutokana na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA). Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kibaha, Mhandisi Debora Kanyika amebainisha hayo alipokuwa alitoa taarifa yake kwenye Baraza la Madiwani lililofanyika katika Halmashauri hiyo kwa ajili ya kupokea taarifa ya miradi inayotekelezwa na taasisi hiyo. Mhandisi Debora amesema hali ya upatikanaji wa maji imeongezeka hadi asilimia 78 kutoka asilimia 67.5 mwaka 2019 kulingana na miradi inayoendelea kutekelezwa. Hata hivyo, meneja huyo amesema bado kuna upungufu wa maji kwenye maeneo ya Vijijini, hususan Kata ya Gwata na katika maeneo ya Dutumi ambapo ipo miradi inalengwa kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2024/2025 ili kumaliza changamoto hiyo. Kwa mujibu wa Mhandisi Debora, katika bajeti ya mwaka 2024, utekelezaji wa mirad

POLISI YAWATAHADHALISHA BOBA BOBA NA BAJAJ DHIDI YA WANAFUNZI WA KIKE

Image
   Madereva wa Bajaji na Pikipiki maarufu Bodaboda Mkoa wa Songwe wametakiwa kuacha tabia ya kuwafanyia vitendo vya ukatili wanafunzi wa kike pindi wanapokwenda na wanaporudi shuleni ili wanafunzi waweze kutimiza malengo yao ya baadae. Wito huo ulitolewa Juni 26,2024 na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikishwaji Jamii kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dodoma Naibu kamishna wa Polisi (DCP) Herry Mwaibambe wakati akitoa elimu kwa madereva bajaji katika ukumbi wa Polisi uliopo Vwawa Wilaya ya Mbozi na kuwataka madereva hao kutoa taarifa za uhalifu na ukatili wa kijinsia kwa Jeshi la Polisi pindi waonapo mtoto au mwanafunzi anafanyiwa vitendo hivyo ili ziweze kushughulikiwa kwa haraka ikiwa ni pamoja na watuhumiwa kufikishwa mahakamani kwa hatua zaidi. Nae Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi SACP Martini Otieno kutoka Kamisheni ya Operesheni na Mafunzo amewaeleza madereva hao umuhimu wa kuwa na leseni ikiwa ni pamoja na kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu kw

MIAKA 120 JELA KWA UBAKAJI NA UNYANG'ANYI

Image
Mahakama ya Wilaya ya Mbeya imemhukumu Samwel Mpese Kilundu kifungo cha miaka 120 Jela kwa makosa manne ambapo mtuhumiwa alihukumiwa kwa makosa mawili ya unyang'anyi wa kutumia silaha pamoja na makosa mawili ya ubakaji. Akisoma hukumu hiyo, Hakimu wa Mahakama hiyo Mhe.Teddy Mlimba alisema kuwa mahakama imemtia hatiani mtuhumiwa baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha pasipo shaka tuhuma dhidi yake kwa makosa mawili ya unyang'anyi wa kutumia silaha chini ya kifungu cha 287 A cha Kanuni ya adhabu Sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo 2022 na makosa mawili ya kubaka chini ya kifungu cha 130 (1) (2) (e) kanuni ya adhabu Sura ya 16 marejeo 2022, na hatimaye mtuhumiwa kupewa adhabu ya kutumikia kifungo Jela miaka 30 kwa kila kosa moja ambapo adhabu/ kifungo hicho kitakwenda sambamba. Awali Mtuhumiwa alitenda makosa hayo yote mnamo Mei 11, 2023 huko maeneo ya Majengo mapya Jijini Mbeya ambapo alivamia nyumbani kwa mhanga na kunyang'anya vitu mbalimbali vikiwemo TV inch 55 na mali mbali

MKURUGENZI AAGIZWA KUWANUNULIA VISHIKWAMBI MADIWANI

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Kighoma Malima amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo kuwanunulia madiwani wa halmashauri hiyo vishkwambi kwa lengo la kupunguza gharama na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi zao. Malima amebainisha hayo wakati wa mkutano maalum wa Baraza la Madiwani kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali – CAG kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya hiyo. Malima amesema madiwani wanapaswa kuwa na simu hizo ambazo zitawawezesha kutekeleza majukumu yao ya kazi kwa haraka na kwa ufanisi hivyo kuongeza kasi ya utendaji kazi. Kwa sababu hiyo ameagiza vishikwambi vya madiwani hao viwe vimekwishanunuliwa kabla au ifakapo Septemba 30, 2024 ambavyo pamoja na kazi nyingine vitasaidia kupunguza gharama ya kununua karatasi kwa ajili ya vikao. “Kabla ya tarehe 30 mwezi wa tisa kikao chochote cha madiwani kitakachofanyika baada ya hapo lazima madiwani wawe na vishikwambi,” amesema Malima. Kwa upande wake

RAIS AFUNGWA MIAKA 45 MAREKANI

Image
  MAHAKAMA ya Mji wa New York nchini Marekani, imemhukumu Rais wa zamani wa Honduras, Juan Orlando Hernandez (55) kifungo cha miaka 45 jela na faini ya dola milioni nane kwa makosa ya ulanguzi wa madawa ya kulevya. Hernandez amehukumiwa kwa kuyasaidia makundi ya wauzaji wa dawa za kulevya tani 500 za cocaine kuingiza nchini Marekani. Waendesha mashitaka wa Marekani wamesema Hernandez aliigeuza Honduras kuwa taifa la dawa za kulevya wakati alipokuwa rais kuanzia mwaka wa 2014 hadi 2022. Wamesema alitumia fedha hizo kujitajirisha na kufanya udanganyifu katika uchaguzi nchini Honduras. Jaji Kevin Castel alimuelezea rais huyo wa zamani kuwa ni mwanasiasa mwenye nyuso mbili ambaye alikuwa na uchu wa madaraka.  DW imeripoti kuwa, Hernandez ameiambia mahakama kuwa hakuwa na hatia na alikuwa ameshitakiwa bila haki. Rais huyo wa zamani wa Honduras awali alidokeza kupitia mawakili wake kuwa angekata rufaa kupinga hukumu hiyo.

WATATU WAFARIKI KWA AJALI MAKETE

Image
  Watu watatu wamefariki dunia wilayani Makete mkoani Njombe kwa ajali ya lori lenye namba za usajili T 911 BHX lililokuwa limebeba viazi baada ya lori hilo  kuacha barabara na kupindukia mtoni katika eneo la Kilanzi darajani kijiji cha Ndulamo Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema imetokea Juni 27,2024 majira ya saa mbili asubuhi baada ya gari hilo kumshinda dereva na kuwataja waliofariki dunia kuwa ni Yohana Mkemanga miaka 35 (dereva), Mussa Sanga (kondakta) na Hamza mkazi wa Morogoro aliyebebwa kama abiria Daktari Vitusi Paul ni Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Makete akizungumza na Green Fm amesema wamepokea miili ya marehemu na kuwataka ndugu zao kufika hospitalini hapo kuwatambua marehemu.   Keneth Kidumage mkazi wa Usalule wilayani Wanging'ombe ni dalali ya viazi vilivyokuwa vimebebwa na lori hilo amesema mzigo huo wa viazi maroba 210 ameubeba kutoka kata ya Bulongwa na Iniho na ulikuwa na thamani ya zaid

NFRA YAKABIDHIWA SUKARI SASA KUANZA KUNUNUA NA KUHIFADHI KUKABILIANA NA UHABA WA SUKARI

Image
  Home Habari Biashara Michezo Burudani Makala Safu Maoni Maktaba EDITIONS The Guardian Nipas WAZIRI wa Fedh, Dk. Mwigulu Nchemba, amesema serikali itaanza kuutumia Wakala wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), kununua na kuhifadhi sukari ili kumaliza shida ya sukari ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara nchini. Dk. Mwigulu Nchemba  Waziri wa fedha amesema NFRA, inakwenda kutibu shida ya kupanda mara kwa mara kwa bei ya sukari nchini hali ambayo imekuwa ikiibua maswali na malalamiko kutoka kwa wananchi. "Tunakwenda kuanza kuitumia NFRA kununua sukari na kuhifadhi kama ambavyo imesaidia katika kuhifadhi mazao mengine ya chakula," amesema Dk. Mwigulu.  Aidha, amesema NFRA inatumika kutokana na kufanya vizuri katika kuhifadhi mazao mengine kwa ajili ya usalama wa chakula. "Kesho nitasoma muswada wa sheria ya fedha ambao hapa bungeni utakwenda kuruhusu kutumika kwa NFRA kununua na kuhifadhi sukari kuanzia mwaka mpya wa fedha na hii itakwenda kutibu upandaji wa bei ya sukari holela

UTOAJI HUDUMA KITUO CHA AFYA TUNDUMA WAMKOSHA MKURUGENZI TOKA OFISI YA RAIS

Image
 Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume, amefanya ziara katika Mkoa wa Songwe, ikiwa ni ziara ya siku mbili katika mkoa huu. Ziara hiyo ilianza tarehe 26 katika Halmashauri ya Mji Tunduma. Dkt. Rashid ametembelea Kituo cha Afya Mpande pamoja na Hospitali ya Halmashauri ya Mji Tunduma. Aidha, Dkt. Rashid amewapongeza viongozi na wauguzi kwa usimamizi na utoaji wa huduma nzuri katika vituo hivyo vya afya.  Dkt. Rashid, huduma bora zinazotolewa katika vituo  zinapaswa kuendelezwa ili kuboresha zaidi afya za wananchi wa Mkoa wa Songwe. Pia ametoa wito kwa viongozi wa sekta ya afya kuendelea kushirikiana kwa karibu ili kufanikisha malengo ya afya kwa Mkoa. Ziara hii ya Dkt. Rashid inalenga kuimarisha utoaji wa huduma za afya katika mkoa na kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma bora na za uhakika.

MCHENGERWA ATOA TAHADHALI KWA KIONGOZI ATAKAE WANYANYASA WANANCHI

Image
    DODOMA - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mohamed Mchengerwa amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI haitasita kuchukua hatua kwa kiongozi yeyote anayewanyanyasa wananchi kupitia ukusanyaji wa ushuru wa mazao kwani Serikali imeshakwisha kutoa Miongozo kuhusu ukusanyaji wa ushuru wa mazao. Mchengerwa ameyasema hayo wakati akichangia hoja yake bungeni jijini Dodoma katika Bunge la Bajeti ya mwaka 2024/2025 linaloendelea. “yapo maeneo ambapo tunaona kuna hitulafu katika ukusanyaji wa ushuru wa mazao, tutafika huko katika Halmashauri zenye changamoto hizo, maelekezo yangu watanzania wasiyanyasike kwenye maeneo yao na TAMISEMI hatutasita kuchukua hatua kwa kiongozi yeyote anawanyanyasa Watanzania katika maeneo yetu kwani serikali ilikwisha kutoa muongozo” Aidha Mchengerwa amesema ifikapo tarehe 30 mwezi juni maandalizi juu ya utolewaji wa Mikopo ya asilimia 10 yatokanayo na mapato ya ndani ya Halmashauri yatakuwa yamekamilika na wataalamu kutoka ofisi ya Rais TA

JELA MIAKA 3 KWA UDANGANYIFU MITIHANI YA TAIFA

Image
  MAHAKAMA ya Wilaya ya Babati, mkoani Manyara, imewahukumu watu wawili kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela kila mmoja, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kufanya udanganyifu wa kuwafanyia mitihani ya taifa wanafunzi wa kidato cha nne na kughushi nyaraka. Waliohukumiwa adhabu hiyo, ni Jacob Dezderi (21), Mkazi wa Bashneti, Wilaya ya Babati na Paschal Sikai (33), Mkazi wa Dareda, ambaye alikuwa Mwalimu wa kujitolea. Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Victor Kimario, alisema mahakama hiyo imejiridhisha kwamba washtakiwa hao walifanya udanganyifu huo mwaka 2023, kwa kuwafanyia mitihani wanafunzi wa kujitegemea, kisha kughushi nyaraka za barua ya utambulisho wa kufanyia mitihani. Kwa mujibu wa hakimu Kimario, makosa hayo waliyafanya Novemba 13 na 14 mwaka jana. Alisema washtakiwa walikamatwa Novemba 14 mwaka 2023, baada ya kukiuka Sheria ya Baraza la Mitihani la Tanzania, Kifungu cha 19 (a) na Kifungu 24 (1), Sura 107 iliyofanyiwa Marejeo Mwaka 2019. Was

RUTO AUKATAA MUSWADA ULIOLETA MACHAFUKO

Image
  RAIS wa Kenya, William Ruto amekataa kutia saini muswada ulio na utata wa fedha wa mwaka 2024, uliosababisha maandamano na vurugu nchini humo. Ruto ameurejesha tena mswada huo bungeni ili ufanyiwe marekebisho. Taarifa hiyo imekuja baada waandamanaji nchini humo wakiapa kuendelea na maandamano yao kupinga nyongeza mpya za ushuru, siku moja tu baada ya polisi kufyatua risasi na kusababisha mauaji ya watu kadhaa katika maandamano hayo yaliyogeuka kuwa vurugu. Rais William Ruto sasa anatarajiwa wakati wowote kutoka sasa kulihutubia taifa kufuatia maandamano ya kuupinga mswada huo.  Hatua hii inakuja baada ya Bunge la Kenya kuidhinisha vikosi vya jeshi la KDF kulinda usalama vikishirikiana na polisi wa Kenya kufuatia purukushani zinazoendelea nchini humo. Bunge kwa sasa limeenda likizo hadi Julai 23 mwezi ujao. DW imeripoti kuwa, Spika wa Bunge la nchi hiyo, Moses Wetangula amewasifu vijana kwa ujasiri wao ila amesisitiza kwamba malalamiko lazima yafuate mkondo wa sheria ndipo yapate kusi

MAKANDARASI WAZAWA KUPEWA MIRADI HADI YENYE THAMANI YA BILIONI 50: BASHUNGWA to

Image
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema Serikali kupitia Wizara ya Fedha imesikia kilio cha Makandarasi Wazawa na imeamua kupandisha wigo wa thamani ya miradi kwa Makandarasi hao kutoka kiasi cha Shilingi Bilioni 10 hadi kufikia Shilingi Bilioni 50. Ameeleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Wizara imetenga jumla ya kilometa 120 kwa ajili ya kutekelezwa na Makandarasi Wazawa ukilinganisha na kilometa 102 zilizotekelezwa na Wakandarasi hao kwa kipindi cha miaka 11 iliyopita. Bashungwa ameeleza hayo Bungeni jijini Dodoma leo Juni 26, 2024 wakati akichangia Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2024/2025 na kumshukuru Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba kwa kurekebisha Sheria ya Manununuzi na Kanuni zilizokuwa pingamizi za ushiriki wa Makandarasi Wazawa katika utekelezaji wa miradi nchini. “Sasa hivi thamani ya miradi imepanda hadi Bilioni 50 na baada ya Bajeti hii Wizara ya Ujenzi kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) tutajipanga na k

RC APONGEZA UTENDAJI KAZI WA DED BIEDA KIBAHA

Image
  MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema hati safi kwa Mkoa huo imekuwa jambo la kawaida na kwasasa Mkoa huo unakwenda kujikita kwenye matumizi yenye tija. Kunenge ameyasema hayo June 25 aliposhiriki katika kikao cha Baraza Maalumu la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kujadili hoja za Mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za Serikali. Amesema kinachoenda kutatua kero za wananchi ni fedha na sio asilimia, na hivyo Mkoa huo kwa sasa umelenga kutengeneza, kukusanya na kuwa na matumizi yenye tija ya mapato. Kunenge pia amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Regina Bieda kwa namna anavyofanya kazi zake kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo ilivyopangwa katika eneo lake. Naye Katibu Tawala mkoa wa Pwani Rashid Mchatta amepongeza utendaji kazi wa Mkurugenzi huyo hususani katika kusimamia makusanyo ya mapato. Mchatta amewataka Watendaji kuhakikisha wanampa ushirikiano Mkurugenzi huyo Ili kufikia malengo ya Halmashauri hiyo. Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Maka

KENYATTA ATAKA WAANDAMANAJI WASIKILIZWE

Image
  NAIROBI, Kenya - Rais wa zamani Kenya, Uhuru Kenyatta ameeleza kusikitishwa kwake juu ya hali ya taifa hilo linalokumbwa na maandamano dhidi ya Mswada wa Fedha akisisitiza kuwa ni haki ya wakenya kuandamana. Mkuu huyo wa zamani wa Nchi alituma rambirambi zake kwa Wakenya waliopoteza maisha wakati wa maandamano ya Jumanne akisema ni haki yao ya kikatiba na wanapaswa kusikilizwa na walioko madarakani. "Ninakuja kwenu nikiwa na huzuni kubwa kutokana na hali ya sasa nchini. Ni haki ya Wakenya kuandamana kama ilivyoamuliwa na Katiba ya Kenya ya mwaka 2010. Pia ni wajibu wa viongozi wasikilize wanaowaongoza," amesema Uhuru. Aidha Uhuru ametoa wito wa utulivu na kuwataka viongozi kuzungumza na wananchi. "Kama rais wenu wa zamani nimehisi uzito wa kuwaongoza Wakenya. Kwa hivyo naomba hekima na ustaarabu uimarishwe na amani na maendeleo yawe yetu sote kama watoto wa Kenya," alisema. Rais huyo wa zamani alithibitisha uungaji mkono wake kwa Wakenya na kuwataka viongozi "