Machapisho

HALMASHAURI YA MOMBA YAMKUNA RC YAOKOA MAMILIONI YA FEDHA MBICHI...RAS AKABIDHIWA RUNGU LA WADAIWA

Picha
Halmashauri ya Wilaya ya Momba katika kipindi cha Miaka 7 imekuwa inakabiliwa na changamoto ya Kutopeleka fedha za makusanyo ya  Mapato Benki hadi kufikia kiasi Cha  zaidi ya shillingi Milioni 800 kuanzia Mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021 hali iliyopelekea Wilaya kuwa na hoja ya kujirudia kila Mwaka. Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi.Regina Bieda ameyasema hayo katika Baraza la kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Juni 25, kuwa tangu  2021 awe katika nafasi hiyo alibaini tatizo hilo na kuchukua hatua kali dhidi ya wote waliohusika kwenye kukusanya fedha za Mapato bila kuweka Benki na hatua kadhaa zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kuajiri vibarua wapya na kupewa mashine za POS ambazo zilikuwa zinatumiwa na watendaji wenye madeni ya Fedha mbichi ili kupisha Watendaji hao kuwa huru na Kuendelea na kesi zao bila kuathiti mapato ya Halmashauri. "Kuanzia 2021 Halmashauri tumefanikiwa kudhibiti mapato yanayokusanywa bila kuweka Benki, hadi Juni 202...

DED ILEJE ANAEDAIWA KUJIUZIA GARI LA SERIKALI KWA MILIONI 4 AIBUKA NA MAZITO

Picha
Kufuatia Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba kumuagiza Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Missaile Musa kumuita aliekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje Haji Mnasi kwa madai ya kujiuzia gari la Serikali aina ya Toyota Hilux yenye namba za usajili DFPA 8508 kwa thamani ya milioni 4 tu gari lilotembea kilometa 900 Mkurugenzi huyo ameibuka na kutoa ufafanuzi. Akiongea Kwa njia ya Simu Mnasi ameshangazwa na madai hayo na amekiri kuyasikia  "Ni kweli nimepata simu za wadau mbalimbali zinazohusiana na tuhuma hizo kiukweli mimi sijanunua hilo gari na lipo Ileje kwenye yadi ya Wilaya na Mimi ndie niliyezuia gari hilo kununuliwa na mnunuzi mmoja aliekuja na kibari toka Wizarani na nikalieleza baraza la Madiwani uwamuzi wangu wa kulizuia gari hilo kuuzwa' amesema Mnasi Aidha Mnasi amedai kuwa mpaka yeye anaondoka Ileje gari hilo kaliacha Ileje na madai dhidi yake ni upotoshaji na hata miutasali ya Vikao vya Baraza la Madiwani vina maelezo ya alichokisema ndani ya Baraza juu ya gari hilo al...

BREAKING NEWS: MWANDISHI WA HABARI WA TBC MKOANI SONGWE ANUSURIKA KATIKA AJALI MBOZI

Picha
Mwandishi wa habari wa Shirika la utangazaji la Taifa (TBC ) Mkoani Songwe Ainess Thobias amenusurika katika ajali iliohusisha Lori na Bajaj aliokuwa amepanda maeneo ya Mbimba Wilayani Mbozi. Aines Thobias ambaye amepata michubuko ameongea na kituo chetu cha habari akiwa katika Hali ya sitofahamu kutokana na mshtuko wa ajali hiyo. Mwenzenu nimenusurika kifo Leo Ajali maeneo ya mbimba, "Gari kubwa Lori lilikuwa mbele yetu, Mimi nilipanda bajaji tuko nyuma ya lori ili kulipisha dereva wa bajaji akataka kuipita ile anaipita tu kulikuwa na daladla aina ya haisi  na ilikuwa spidi ikaja kuipiga bajaji yetu na kuisukumia kwenye Lori amina usiamini Mungu mkubwa amenitoa salama kaka ila maumivu machache hata siamini kilichotokea" Amesema Aines. Habari Jamii Tanzania tunampa pole Ainess Thobias na kumtakia afya njema na uponyaji wa haraka Ili aweze kuendelea na Majukumu yake ya kuhabarisha Umma

DED SONGWE YAMKUTA MAZITO MBELE YA RC SONGWE

Picha
 Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba ametoa masaa 12 kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Songwe kutoa maelezo kwa maandishi ya kuchelewesha mradi wa kituo cha Afya Ifwenkenya, Mgumba ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi Aidha mgumba amewakumbusha Viongozi Wilayani humo kuzingatia  maelekezo   ya Mh Rais kwa Kiongozi ambaye hatawajibika katika utekelezji wa miradi ya maendeleo kwamba kwanini asichukuliwe hatua kwa kutokamilisha hatua za ukamilishaji wa vituo vya Afya  Aidha katika Hatua nyingine Mgumba amewaaagiza Viongozi Wilayani humo kuhakikisha wanajenga mradi huo usiku na mchana  ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati pamoja na kuwasilisha taarifa ikiwa na miongozo ya ujenzi wa miradi na manunuzi ya vifaa vya ujenzi (BOQ) Ziara ya Mkuu wa mkoa huo ni muendelezo wa Ziara zake za kikazo Mkoani humo zilizolenga kukagua miradi ya maendeleo na kusikilia kero za Wananch...

AFISA ELIMU MBOZI MATATANI KWA KUMDANGANYA RC

Picha
 Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amemuonya Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Juma Tukosa kwa kumdanganya juu ya ujenzi wa Sekondari ya Ichenjezya. Afisa Elimu Sekondari alimdanganya Mkuu wa Mkoa wakati akiwa kwenye ziara ya ukaguzi wa miradi katika Sekondari ya Senye iliyopo Kata ya Vwawa baada ya Mkuu wa Mkoa kuhoji sababu iliyosababisha Halmashauri kujenga Sekondari Kata ya Vwawa na kuacha kujenga Kata ya Ichenjezya ambayo haina Sekondari na muongozo wa unataka kipaombele cha kwanza Shule ikajengwe kwenye Kata ambayo haina Sekondari. Mkuu wa Mkoa alipomuuliza kwa nini hawajajenga Kata ya Ichenjezya, Afisa Elimu akasema hawajajenga kwa sababu Ichenjezya wana eneo dogo la ekari 4, eneo ni oevu, maji yanajaa katika eneo hilo, watalamu walisema eneo halifai, eneo liko Kata ya Hasanga na sio Ichenjezya mwisho wasingeweza kupeleka fedha za Serikali kwenye ujenzi Sekondari kwa sababu hizo. Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba kukatisha ziara ya...

LUKU KUKOSEKANA MASAA MAWILI NCHI NZIMA

Picha
  Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limesema wateja wa huduma ya ununuzi wa umeme kupitia Luku watakosa huduma hiyo kwa saa mbili kwa usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi Juni 9 mwaka huu. Huduma hiyo itakosekana kuanzia saa 6 usiku hadi saa 8 usiku nchi nzima ili kupisha maboresho ya mfumo wa manunuzi ya umeme kwa wateja wanaolipia kabla ya matumizi (Luku), kupitia mifumo iliyopo katika kituo cha kujikinga na majanga (Disaster Recovery). Akizungumza leo Juni 06/2022 kwenye makao makuu ya taasisi hiyo, Meneja Mwandamizi wa Tehama, Cliff Maregeli amesema kutokana na changamoto hiyo ya kiufundi wateja wanashauri kununua umeme wa ziada ili kuepuka usumbufu ambao unaweza kujitokeza. "Maboresho ni muhimu na yanalenga kuongeza ufanisi kwenye mfumo wa manunuzi ya umeme ili kuhudumia wateja wengi ipasavyo pale inapotokea hitilafu ya aina yeyote katika kituo chetu Kikuu Cha mfumo," amesema Maregeli Kwa uapande wake Msemaji wa Shirika hilo, Martini Mwambene ameshauri wateja kuzingatia ta...

MKUU WA MAJESHI AAMUAGA RASMI RAIS MWINYI

Picha
  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (CDF), Jenerali Venance Mabeyo amemuaga Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Mwinyi baada ya kumaliza muda wake utumishi ndani ya Jeshi hilo. Mabeyo amemuaga Dk Mwinyi huyo leo Jumatatu Juni 6, 2022 Ikulu ya Zanzibar. Katika maelezo yake Mkuu huyo wa Majeshi ya Ulinzi, alieleza haja ya kumuaga pamoja na kutoa shukrani kwa Rais Mwinyi akieleza kuwa ni kiongozi ambaye amefanya naye kazi kwa muda mrefu na kumsaidia katika kutekeleza vyema majukumu yake ndani ya Jeshi hilo. “Nakutakia afya njema na maisha marefu pamoja na familia yako….nathamini sana ushirikiano ulionipa katika kipindi chako cha uongozi tangu ukiwa Waziri wa Ulinzi hadi leo hii, ahsate sana”, amesem Jenerali Mabeyo. Mabeyo anafikia kikomo cha utumishi mwisho wa mwezi huu akiwa amelitumikia Jeshi hilo tangu mwaka 1979 huku nafasi hiyo ya CDF akiitumikia kwa kipindi cha miaka sita tangu alipoteuliwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati John Magufuli ...

RC SONGWE AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI MBOZI KWA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

Picha
 Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amemuagiza Kamanda wa Jeshi la Polisi Songwe, kuwatafuta popote pale walipo watu sita (6) ambao wanatuhumiwa  kwa kuhatarisha amani na uharibifu wa mazingira katika msitu wa Namwanga uliopo Kijiji cha Namwanga Kata ya Hezya Wilaya ya Mbozi. Mkuu wa Mkoa amechukua hatua iyo Juni 1 wakati ziara yake baada ya kujionea uharibifu wa mazingira uliofanyika katika msitu wa Namwanga alipokuta miti imekatwa hovyo na uwepo matanuri ya mkaa pembezoni mwa  msitu huo. Watuhumiwa wanaotafutwa ni Eliud Shizya Mwashilindi, Rashid Charles Mwashilindi, Rasco Wiliad Mwashilindi, Michael Pondamali Msukwa, Rapheel Alnasi Mwambala na Yona Watson Mwambala. Waarifu hao wa Mazingira walitaka kuwateka waandishi wa Habari pamoja na kumkamata na kumteka mtumishi mmoja na kushinikiza wamuachie mwenzao aliyekamatwa ndipo watumishi kwa hofu ya maisha ya mwenzao wakamuachia yule muarifu Mkuu wa Mkoa amesema Serikali haiwezi kuwaacha waarifu watambe na mazingira ...

MWANDISHI WA HABARI SONGWE ANYAKUA TUZO YA UANDISHI

Picha
 Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Serikali  Baraka Messa toka Mbozi Mkoani Songwe amepata  tuzo ya uandishi habari za ushirika 2021 zilizoandaliwa na EJAT. Baraka Messa ambae ni Maarufu Mkoani Songwe kwa Uandishi wa Makala Mbalimbali za Kijamii alikuwa ni Mwandishi pekee toka Mkoani Songwe aliepata nafasi ya kuteuliwa na Jopo la Majaji kushiriki Tuzo hizo na kuwa ni miongoni mwa Washiriki 6 walikuwa wakichuana nafasi Moja. Sisi kama HABARI JAMII TANZANIA tunampongeza Mwandishi Baraka Messa kwa Tuzo hiyi

WIZI WA BATA WASABABISHA KIJANA ACHOMWE MOTO MBOZI

Picha
  Kijana mmoja aliefahamika kwa  jina lameck sannsumbi (25)Mkazi wa Kata ya Idiwili amechomwa moto hadi kufariki na Wananchi wenye hasira kali Kata ya Ilolo baada ya kudaiwa kuvunja banda la bata na kuiba inadaiwa kuwa Marehemu  alikwenda kumsalimia bibi yake Mkazi wa Ilolo aliefahamika kwa jina la Tabita Kayange (63)na alimjeruhi bibi huyo kwa kumpiga na kumuumiza maeneo ya jicho la kushoto. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Jannet Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema Marehemu Lameck wakati akitekeleza tukio la Uvunjanji wa Banda la kufugia bata bibi yake alipomuona alimjeruhi kwa kumpiga ndipo bibi huyo alipiga kelele na Wananchi wakajitokeza na kuanza kumshambulia Mwizi huyo na kisha kumchoma moto hadi mauti ilipomkuta. Kamanda Magomi amewataka Wakazi wa Mkoa wa Songwe kutojichukulia sheria Mkono na pindi wanapoona Vitendo vya kihalifu katika maeneo yao watoe taarifa kwa jeshi la Polisi. aidha amesema jeshi la Polisi linaendelea na Uchunguzi wa tukio h...

POLISI SONGWE WATOA SABABU ZA MFANYABISHARA SONGWE BARAKA SANGA KUJINYONGA

Picha
 Jeshi la Polisi Mkoani Songwe limetoa taarifa ya kifo cha kujinyonga cha Kijana Maarufu Mkoani Songwe na Mfanyabiashara anaefahamika kwa jina la Baraka Sanga maarufu kwa jina la  Twangara aliejinyonga kwa kutumia Shuka jeupe. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Jannet Magomi amesema Baraka  Sanga amekutwa amejinyonga mida ya saa kumi na mbili na robo asubuhi kwa kutumia Shuka. "Tumepata taarifa ya Kujinyonga kwa Kijana anaeitwa Baraka Isack Sanga Kabila lake Mkinga katika kata ya Ilolo amejinyonga na taarifa zetu za kiuchunguzi marehemu amejinyonga kutokana na Ulevi wa kupindukia baada ya kuachwa na Mkewe na Marehemu hakuacha Ujumbe wowote" amesema kamanda wa Polisi Songwe Jannet Magomi. Baraka Sanga alikuwa ni Mfanyabiashara wa Duka maeneo ya njia panda ya Kuelekea Stendi ya Starehe Wilayani Mbozi na alikuwa maarufu kutokana na Ucheshi wake mbele ya Jamii hususani Vijana. Bwana alitoa na Bwana ametwaa Pumzika Kwa Amani Baraka Sanga

GARI LILILOBEBA MAGENDO LAPATA AJALI SONGWE LIKIWAKIMBIA KIKOSI KAZI CHA MKOA WA SONGWE

Picha
Gari aina ya Brevis lenye namba za usajili T 265 CYN limepata ajali maeneo ya Ichenjezya Vwawa Wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe likiwa limebeba Magendo mbalimbali vikiwemo Vipodozi na Vitenge. Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo Jumapili ambapo mashuhuda wa ajali hiyo wamedai gari hilo lilikuwa mwendo kasi na limezima taa na ndipo lilipokuta na tuta lililopoka katika barabara hiyo na kisha kupaa na kudondoka huku matairi yakielekea juu. Akitoa taarifa Meneja wa Tra Mkoa wa Songwe Dikson Qamala amesema gari hilo lilikuwa nikiwakimbia kikosi kazi cha kuzuia na kupambana na Magendo kilichoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe Omary Mgumba. "Hili gari lilikimbia kizuizi chetu tulichokiweka Oldvwawa na kukigonga ndipo lilipopasua matairi yake mawili na katika kututoroka alikimbilia njia ya Ichenjezya na ndiko alipopata hii ajali na pia kuna gari  tumelikamata aina ya Crown T 510 DYC ambalo lilikuwa likiisindikiza gari iliopata ajali na lenyewe tumelikamata na Vitenge na Vipodozi" amese...

BREAKING NEWS: NCCR MAGEUZI YAMSIMAMISHA MBATIA

Picha
  Halmash auri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi imemsimamisha Mwenyekiti wa Chama hicho, James Mbatia na makamu Mwenyekiti Bara, Angelina Mtahiwa kutojihusisha na shuhhuli zozote za chama hadi mkutano Mkuu utakapoitishwa ili wajieleze kuhusiana na tuhuma inazowakubali. Uwamuzi huo umefanyika leo Jumamosi Mei 21, 2022 kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kugombanisha viongozi na kulazimisha kujiuzulu. Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Mwenyekiti wa azimio hilo, Joseph Selasini amesema pamoja na kusimamishwa kwa viongozi hao pia wamelivunja Baraza la Wadhamini la NCCR  na kuteua wajumbe wapya ambao watasajiliwa kwa mujibu wa taratibu zitakazowekwa Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Sisty Nyahoza amesema walipokea barua kutoka NCCR-Mageuzi kuwa kuna mabadiliko ya wajumbe wa bodi ya wadhamini. Amesema pamoja na mabadiliko hayo kulikuwa na ajenda nyingine ambayo ni kusimamishwa kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti Bara kutokana na maazimio hayo wanasubiri barua rasmi ili kutoa taarif...

BREAKING NEWS: CHADEMA YAWAFUKUZA RASMI UANACHAMA KINA MDEE

Picha
 HALIMA MDEE NA WENZAKE 18 WAFUKUZWA RASMI CHADEMA - Baraza Kuu la CHADEMA usiku wa leo kuamkia Alhamisi (Mei 12, 2022) limezitupilia mbali Rufaa za Halima Mdee na wenzake 18 za kupinga kufukuzwa uanachama na Kamati Kuu ya chama - Baraza hilo limeunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu ya chama wa kuwafukuza uanachama Halima Mdee na wenzake kwa kukubali kwenda kuapishwa na kuwa wabunge wa Viti Maalumu bila kupata baraka za chama

SERIKALI KUTOA BILIONI 100 KUPUNGUZA MAKALI YA BEI YA MAFUTA

Picha
  Waziri wa Nishati, January Makamba amesema Serikali imetoa ruzuku ya Sh100 bilioni kwa ajili ya kupunguza bei ya mafuta nchini. Akizungumza Bungeni leo Jumanne Mei 10, 2922 Waziri  Makamba amesema ruzuku hii inatolewa kwa kupunguza matumizi ya Serikali katika kipindi kilichobaki cha mwaka2021/22. Amesema Kutolewa kwa ruzuku hiyo hakutagusa miradi ya maendeleo ambayo inaendelea “Rais wetu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo kwamba mwaka ujao wa fedha ni mbali. Ahueni itafutwe mapema zaidi. Hivyo basi, kama hatua ya dharura, katika kipindi hiki kabla hatujafikia mwaka mpya wa fedha, Serikali ijibane na ijinyime na zitolewe Sh100 bilioni kwa ajili ya kupunguza bei za mafuta hapa nchini. “Ruzuku hii ya Sh100 bilioni itatolewa kwa ajili ya kupunguza bei ya mafuta kuanzia Juni 1, 2022. Hii ni kutokana na kuwa, wafanyabiashara wa jumla wamekwisha lipia gharama ya mafuta ambayo imejumuishwa katika bei hizi za Mei 2022 na wafanyabiashara wa mafuta katika vituo wamekwisha...

MAGAZETI YA LEO 10 MEI 2022

Picha
 

MBUNGE WA MOMBA AINGIA NA GONGO BUNGENI

Picha
  Mbunge wa Momba (CCM), Condester Sichalwe ameitaka Serikali kuzipima na kuzirasimisha pombe za kienyeji ikiwamo gongo ili kuwasaidia kiuchumi wanawake wanaofanya shughuli hizo Condester hayo leo Jumatatu Mei 9, 2022 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2022/2023 huku akionyesha baadhi ya baadhi ya pombe za gongo ambazo amesema zimetoka nje ya nchi na zinauzwa hapa nchini. Mbunge huyo ameitaka Wizara hiyo kuunda bodi kama Wizara ya Kilimo ilivyounda Bodi ya Mazao Mchanganyik Amesema watu wanaonekana kunywa pombe za kienyeji wanaonekana kuwa hawana akili lakini ukinywa bia unaokena wa kisasa. Amesema hata katika balozi wamekuwa wakitenga fedha kwa ajili ya kununua pombe za bei ghali lakini ukizionja hazina ladha ya tofauti na gongo “Tunajiuliza ni kwasababu hizi zina jina la kizungu na hizi ni za kibantu. Bodi hii itakapounda itasaidia kwenda kupima viwango vya kilevi vilivyopo. TBS (shirika la Viwango Nchi...

BREAKING NEWS: GARI LA OFISI YA RC SONGWE LAKAMATWA KWA MAGENDO

Picha
Magari 14 yamekamatwa katika Oparesheni Maalumu ya kupambana na magendo katika Mpaka wa Tunduma kupitia Kamati ya ulinzi na Usalama iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe. Kati ya Magari hayo 14 ambayo yamekamatwa gari moja linamilikiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe likiwemo gari ambalo limekuwa likitafutwa kwa miaka mingi bila Mafanikio. Hapa Rc Mgumba anatoa msimamo wa Serikali juu ya magari yaliyokamatwa na wale wote watakao kamatwa na magendo kwa mkoa wa Songwe. Aidha Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Songwe ametoa wito kwa Wafanyabiashara, kufuata sheria za forodha na kueleza changamoto wanazopata wakati wa kudhibiti magendo katika Mpaka wa Tunduma.

RC SONGWE AWATAKA WAKUU WA WILAYA KUJIRIDHISHA KABLA YA KUWAWEKA WATU NDANI

Picha
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amewataka wakuu wa Wilaya kujiridhisha na kosa ambalo mtu yeyote au mtumishi wa umma amefanya kabla ya kuchukua hatua ya kumuweka ndani kwa saa 48. Mkuu wa Mkoa ametoa wito huo kwenye maadhimisho ya sikukuku ya wafanyakazi ambayo kwa ngazi ya Mkoa imefanyika katika Mji wa Tunduma, 1 Mei 2022. "Lazima tujiridhishe kosa linaloweza kuhatarisha Amani ya sehemu hiyo au usalama wa Taifa na ukimweka ndani kwa adhabu hiyo hakikisha anatakiwa apelekwe Mahakamani" Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba. Mkuu wa Mkoa amesema kama kuna mtumishi amefanya kosa la jinai lazima akamatwe na apelekwe Mahakamani lakini kama ni kosa la kiutumishi ni lazima lirudi katika mamlaka yake ya utumishi ili wamchukulie hatua za kinidhamu Aidhaa, Mkuu wa Mkoa amesema wakati mwingine mtu anawekwa ndani kwa sababu ya usalama wake baada ya Serikali kujiridhisha  usalama wake uko hatarini. Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa ametoa vyeti kwa Wafanyaki bora katika ka...

HABARI KUBWA MAGAZETI YA LEO

Picha